Mchungaji Msigwa, Kiti cha Spika, na Kanuni za Bunge

master peace

JF-Expert Member
Joined
Dec 19, 2012
Posts
1,450
Reaction score
444
Wanabodi heshima kwenu wakuu !!
Nimefuatilia mijadala mingi hapa JF kuhusiana na hotuba ya kambi ya upinzania iliyosomwa rasmi bungeni na Kamanda Mchungaji Msigwa. Nimesikitishwa sana na baadhi ya wachangiaji either kwa kutoelewa,uvivu wa kufikiria, au kutumiwa katika hili sakata wakiwa na lengo la kupotosha ukweli uliotolewa leo bungeni tarehe 30/04/2013 na Mchungaji Msigwa. Wengine wameenda mbali zaidi wakiwemo mawaziri wa serikali ya Jakaya Mrisho Kikwete waki-mtuhumu Mchungaji Msigwa ati ni Muongo / mwongo. Kauli hii imezua sintofahamu hapa mtaani kwetu, sisi wasikilizaji na watazamaji tumejiuliza maswali mengi pasipo kuwa na majibu.

Ndugu wanabodi nawaomba tutenge mda wetu kidogo tu, ili kutafakari maswali haya ya msingi, ili mwisho wa siku tupate pa kusimamia :

  • Je ni kweli kwamba vikao vya leo vya bunge vimeendeshwa na kiti cha Spika bila kufuata kanuni na taratibu zilizopo ? Endapo jibu ni ndiyo, je kwa nini hazikufuatwa ?
  • Endapo kanuni zimefuatwa barabara, hizo kanuni zinasemaje kuhusiana na Mbunge aliye tamka maneno ya uongo bungeni ?
  • Je kiti cha Spika kimeshindwa nini kumuamru Mchungaji Msigwa kutoa ushahidi kwa yale aliyo yasoma ?
  • Je Muishiwa Nchimbi anataka kutuaminisha Kiti cha Spika kimemwogopa Mchungaji Msigwa?
Wanabodi naomba kuwasilisha,
Karibuni.
 
hawezi tena kuomba ushahidi kwa lema aliomba ushahidi akapelekewa akaingia mitini, spika hawezi kurudia kosa la kuomba ushahidi hata umshikie bunduki ni bora apindishe kanuni ili mradi kinana atetewe kwa kung'oa tembo meno huku TISS wakiendelea kung'oa binadamu kucha.
 
Simple....
Kama unaona kuna Watu wawili wanaogombana na wewe ni refa;
Mwingine kila mara anasema "Refa" unanionea,Unanionea....Mbona Huyu haumfanyii kama unavyonifanyia MIMI?
Halafu unakuta kila mmoja (Timu na Mashabiki walio wengi walio na uwezo wa kuwa Uwanjani ama kusikiliza Redio) wanapiga Kelele unamuonea...Unamuonea

Basi Refa anaamua awafundishe kwa staili ya aina yake,ili kuona kama kweli mnacholalamika ni kwamba hamtaki muonewe wote ama mnataka nyie tu ndo mpendelewe?

Basi anaamua kupeta RAFU za PANDE ZOTE
Bahati mbaya anaanza kupeta rafu zenu Kipindi cha kwanza,mpaka mnashangaa

Sasa kikiingia Kipindi cha pili inakuwa zamu ya Wapinzani wenu kuwafanyia Rafu....Mkianza kulalamika Refa anawaambia "Hapana msilalamike,subiri mnyundwe kama mlivyowanunda wenzenu"...
Ni kweli Refa anakuwa hatendi Haki
Lakini anakuwa anatoa FUNZO kwenu nyote,hasa upande wa wanaolalamika sana
Kwamba HII ndio mnataka iwe style ya MCHEZO?
Then wote mtasema HAPANAAAA
Then anasema OK....basi kuanzia Kesho mfuate sheria,kwani hakuna anayependa kuchezewa rafu....
 
Ni wazi spika amepindisha kanuni kwa sababu anazozijua yeye. Nimemsikia na hii ni mara ya pili wabunge wakiomba mwongozo anajibu 'waacheni waseme, mbona wao walikaa kimya wakati mnasema...endelea' nionacho mimi huuko ndiko kuendekeza udaku na kushushia bunge letu hadhi. Kinachomsumbua hutu mama na wenzake ni ushabiki uliopitiliza hata ukweli unaposemwa
 
sijawahi kuona mtu anatoka taifa lake na kwenda kuwa kiongozi taifa jingine na kuacha kulisaliti hilo taifa.
mifano ni mingi.
1.musa=misri.
2.yusuph=misri.
3.esther=...........
4.botha=south
5.smith=rhodesia
6......=kongo drc.
 
hawezi tena kuomba ushahidi kwa lema aliomba ushahidi akapelekewa akaingia mitini, spika hawezi kurudia kosa la kuomba ushahidi hata umshikie bunduki ni bora apindishe kanuni ili mradi kinana atetewe kwa kung'oa tembo meno huku TISS wakiendelea kung'oa binadamu kucha.

Mkuu hivyo basi ni dhahiri alicho kitamka kamanda Msigwa hakina uongo hata chembe, ndo maana Kiti cha Spika kimeshikwa na kigugumizi cha kuomba ushahidi, kwani kwa kufanya hivyo Mchungaji Msigwa anaweza kumvua Kinana nguo mbele ya kadamnasi.
 
sijawahi kuona mtu anatoka taifa lake na kwenda kuwa kiongozi taifa jingine na kuacha kulisaliti hilo taifa.
mifano ni mingi.
1.musa=misri.
2.yusuph=misri.
3.esther=...........
4.botha=south
5.smith=rhodesia
6......=kongo drc.

Mkuu, ni kweli historia inaonyesha hivyo; Ni dhahiri hata huyu Dentist yupo hapa nchini kwa maslahi yake binafsi. Je kwa nini Serikali na Bunge wanahaha kumkingia kifua ? Only in Tanzania.
 
Huo mtaa wenu ulipatwa na sintofahamu utakuwa mtaa unaopenda sana UDAKU.

Msigwa kaongea UDAKU tupu hakuna kitu pale.

Spika hawezi kupoteza muda na UDAKU...
 
Simple....
Kama unaona kuna Watu wawili wanaogombana na wewe ni refa;
Mwingine kila mara anasema "Refa" unanionea,Unanionea....Mbona Huyu haumfanyii kama unavyonifanyia MIMI?
Halafu unakuta kila mmoja (Timu na Mashabiki walio wengi walio na uwezo wa kuwa Uwanjani ama kusikiliza Redio) wanapiga Kelele unamuonea...Unamuonea

Basi Refa anaamua awafundishe kwa staili ya aina yake,ili kuona kama kweli mnacholalamika ni kwamba hamtaki muonewe wote ama mnataka nyie tu ndo mpendelewe?

Basi anaamua kupeta RAFU za PANDE ZOTE
Bahati mbaya anaanza kupeta rafu zenu Kipindi cha kwanza,mpaka mnashangaa

Sasa kikiingia Kipindi cha pili inakuwa zamu ya Wapinzani wenu kuwafanyia Rafu....Mkianza kulalamika Refa anawaambia "Hapana msilalamike,subiri mnyundwe kama mlivyowanunda wenzenu"...
Ni kweli Refa anakuwa hatendi Haki
Lakini anakuwa anatoa FUNZO kwenu nyote,hasa upande wa wanaolalamika sana
Kwamba HII ndio mnataka iwe style ya MCHEZO?
Then wote mtasema HAPANAAAA
Then anasema OK....basi kuanzia Kesho mfuate sheria,kwani hakuna anayependa kuchezewa rafu....

Mkuu, mie natofautiana na wewe ki-mtizamo; kumbuka kazi ya kiti cha spika ni kuhakikisha ya kuwa serikali iliyoko madarakani ina simamiwa vilivyo na wawakilishi wetu kwa manufaa ya taifa zima, na siyo kutetea vyama kama unavyotaka kutuaminisha katika andiko lako. Endapo ulicho kiandika ni sahahi, je kiti cha Spika kina peta hizo rafu kwa faida ya nani ? Je mwisho wa siku tutarajie nini kwa sisi tusiokuwa na vyama ?

Mkuu ni dhahiri bandiko lako laweza pelekea sisi tusiokuwa wapenzi wala washabiki wa chama chochote kile, kuanzisha umoja wetu ili tuweze kupata wawakilishi bungeni ili wakatetee maslahi yetu, na wakianza kucheza tutakiomba Kiti cha spika kiendelee kupeta kama kawa.
 
Huo mtaa wenu ulipatwa na sintofahamu utakuwa mtaa unaopenda sana UDAKU.

Msigwa kaongea UDAKU tupu hakuna kitu pale.

Spika hawezi kupoteza muda na UDAKU...

Mkuu jifunze kujenga hoja kwani hili ni jukwaa la GT, siyo kuandika kila kitu as if unajifunza kusoma na kuandika.
Na siyo lazima uchangie kila mada, wakati mwingine jifunze kuficha uwezo wako mdogo wa kufikiri kwa kukaa kimya itakusaidia maishani mwako.
 
Mkuu hivyo basi ni dhahiri alicho kitamka kamanda Msigwa hakina uongo hata chembe, ndo maana Kiti cha Spika kimeshikwa na kigugumizi cha kuomba ushahidi, kwani kwa kufanya hivyo Mchungaji Msigwa anaweza kumvua Kinana nguo mbele ya kadamnasi.

tena ktk hiyo kadamnasi na watoto,wakwe wote watakuwepo, sasa aibu hii naona Makinda ameishtukia kaamua kufunika kombe,ila kinana bingwa mimi juzi kati tu kumtoa mwanangu jino ilikuwa mbinde,Kinana anamtoa tembo mkonga!?
 
Simple....
Kama unaona kuna Watu wawili wanaogombana na wewe ni refa;
Mwingine kila mara anasema "Refa" unanionea,Unanionea....Mbona Huyu haumfanyii kama unavyonifanyia MIMI?
Halafu unakuta kila mmoja (Timu na Mashabiki walio wengi walio na uwezo wa kuwa Uwanjani ama kusikiliza Redio) wanapiga Kelele unamuonea...Unamuonea

Basi Refa anaamua awafundishe kwa staili ya aina yake,ili kuona kama kweli mnacholalamika ni kwamba hamtaki muonewe wote ama mnataka nyie tu ndo mpendelewe?

Basi anaamua kupeta RAFU za PANDE ZOTE
Bahati mbaya anaanza kupeta rafu zenu Kipindi cha kwanza,mpaka mnashangaa

Sasa kikiingia Kipindi cha pili inakuwa zamu ya Wapinzani wenu kuwafanyia Rafu....Mkianza kulalamika Refa anawaambia "Hapana msilalamike,subiri mnyundwe kama mlivyowanunda wenzenu"...
Ni kweli Refa anakuwa hatendi Haki
Lakini anakuwa anatoa FUNZO kwenu nyote,hasa upande wa wanaolalamika sana
Kwamba HII ndio mnataka iwe style ya MCHEZO?
Then wote mtasema HAPANAAAA
Then anasema OK....basi kuanzia Kesho mfuate sheria,kwani hakuna anayependa kuchezewa rafu....

Kama ingekuwa mpirani kweli, maneno yako ni mazuri; lakini hapa tunazungumza maisha ya watu na si mchezo(burudani). Speaker wetu anajua moja tu kuwa yupo katika kiti kile kuilinda serikali ya ccm kwasabu ndio waliomweka hapo. Ukiona mtu amefika mahali anaendesha chombo kama Bunge bila kufuata kanuni, miongozo na taratibu mwangalie vizuri kwani hicho ni kirusi hatari sana kwa afya ya taifa.
 
Mkuu jifunze kujenga hoja kwani hili ni jukwaa la GT, siyo kuandika kila kitu as if unajifunza kusoma na kuandika.
Na siyo lazima uchangie kila mada, wakati mwingine jifunze kuficha uwezo wako mdogo wa kufikiri kwa kukaa kimya itakusaidia maishani mwako.
Kwani ww hujui kuwa huyo jamaa yumo kwenye payroll ya Nape pale Lumumba?

Kwa hiyo malipo yake, yatategemea uwingi wa post zake kwa siku hiyo, kwa hiyo huyo jamaa 24 hours, yupo kwenye laptop, mpaka waweza kujiuliza mtu huyo, anakula saa ngapi? na je shughuli nyingine anafanya muda gani?!

Kweli sasa ndiyo tunaamini kweli, magamba wameshikwa pabaya, mpaka wanafikia kutoa ajira kwa vijana, kwa kazi moja tu, kujibu makombora mfululizo yanayomiminwa humu JF, na wazalendo wa kweli wa nchi hii, ambao CDM haiwalipi hata shilingi 10, tofauti na CCM, ambayo vijana wengi waliopata divisheni 0 mwaka jana, wameiona ndiyo kimbilio lao, kufanya kazi ya propaganda ya wanamagamba!!
 
tena ktk hiyo kadamnasi na watoto,wakwe wote watakuwepo, sasa aibu hii naona Makinda ameishtukia kaamua kufunika kombe,ila kinana bingwa mimi juzi kati tu kumtoa mwanangu jino ilikuwa mbinde,Kinana anamtoa tembo mkonga!?

Mkuu kuna mdau mmoja katutonya hapa jamvini ati huko ughaibuni huyu jangili wa kimataifa anafahamika kwa jina maarufu la DENTIST.
 
Wanabodi heshima kwenu wakuu !!
Nimefuatilia mijadala mingi hapa JF kuhusiana na hotuba ya kambi ya upinzania iliyosomwa rasmi bungeni na Kamanda Mchungaji Msigwa. Nimesikitishwa sana na baadhi ya wachangiaji either kwa kutoelewa,uvivu wa kufikiria, au kutumiwa katika hili sakata wakiwa na lengo la kupotosha ukweli uliotolewa leo bungeni tarehe 30/04/2013 na Mchungaji Msigwa. Wengine wameenda mbali zaidi wakiwemo mawaziri wa serikali ya Jakaya Mrisho Kikwete waki-mtuhumu Mchungaji Msigwa ati ni Muongo / mwongo. Kauli hii imezua sintofahamu hapa mtaani kwetu, sisi wasikilizaji na watazamaji tumejiuliza maswali mengi pasipo kuwa na majibu.

Ndugu wanabodi nawaomba tutenge mda wetu kidogo tu, ili kutafakari maswali haya ya msingi, ili mwisho wa siku tupate pa kusimamia :

  • Je ni kweli kwamba vikao vya leo vya bunge vimeendeshwa na kiti cha Spika bila kufuata kanuni na taratibu zilizopo ? Endapo jibu ni ndiyo, je kwa nini hazikufuatwa ?
  • Endapo kanuni zimefuatwa barabara, hizo kanuni zinasemaje kuhusiana na Mbunge aliye tamka maneno ya uongo bungeni ?
  • Je kiti cha Spika kimeshindwa nini kumuamru Mchungaji Msigwa kutoa ushahidi kwa yale aliyo yasoma ?
  • Je Muishiwa Nchimbi anataka kutuaminisha Kiti cha Spika kimemwogopa Mchungaji Msigwa?
Wanabodi naomba kuwasilisha,
Karibuni.

mkuu apo wameshikwa nyeti ukweni watafanyaje c unawajua magamba walivyo wangemwambia wanampga ban mwezi kw uongo wamestuka sana jamaa kapgwa mawe mbaya
 
Kwani ww hujui kuwa huyo jamaa yumo kwenye payroll ya Nape pale Lumumba?

Kwa hiyo malipo yake, yatategemea uwingi wa post zake kwa siku hiyo, kwa hiyo huyo jamaa 24 hours, yupo kwenye laptop, mpaka waweza kujiuliza mtu huyo, anakula saa ngapi? na je shughuli nyingine anafanya muda gani?!

Kweli sasa ndiyo tunaamini kweli, magamba wameshikwa pabaya, mpaka wanafikia kutoa ajira kwa vijana, kwa kazi moja tu, kujibu makombora mfululizo yanayomiminwa humu JF, na wazalendo wa kweli wa nchi hii, ambao CDM haiwalipi hata shilingi 10, tofauti na CCM, ambayo vijana wengi waliopata divisheni 0 mwaka jana, wameiona ndiyo kimbilio lao, kufanya kazi ya propaganda ya wanamagamba!!

Mkuu asante kwa kunifumbua macho, kwa nature ya post zao siamini hata kama wamefika form two. Mwanfunzi aliyemaliza form hata kama amepata zero hawezi kuwa na mawazo finyu kama hawa waliojariwa pale Lumumba, kwani hawana uwezo wa kujenga hoja hata kidogo.

Wanabodi, ni dhahiri CCM imeshindwa kila kitu, yaani hata kuwafanyia usaili vijana wao wa kukesha mitandaoni nalo linahitaji mwekezaji?
 
mkuu apo wameshikwa nyeti ukweni watafanyaje c unawajua magamba walivyo wangemwambia wanampga ban mwezi kw uongo wamestuka sana jamaa kapgwa mawe mbaya

Mkuu, nimesikia usiku wa leo walikuwa na vikao vya siri jinsi ya kumsafisha Dentist Kinana; Na sisi tunawaambia it is too late.

Hongera Kamanda Mchungaji Msigwa kwa kazi nzuri.
Mungu ibariki CHADEMA na viongozi wetu.
 
Mhudumuuu.....leta kinana baridi hapa.
Naangalia kikwete akihutubia msondo ngoma na kikundi cha ngoma.
Kwani ameshindwa kubebea wanafunzi wa shule za msingi jamani.....khaaa'
 
Wanabodi heshima kwenu wakuu !!
Nimefuatilia mijadala mingi hapa JF kuhusiana na hotuba ya kambi ya upinzania iliyosomwa rasmi bungeni na Kamanda Mchungaji Msigwa. Nimesikitishwa sana na baadhi ya wachangiaji either kwa kutoelewa,uvivu wa kufikiria, au kutumiwa katika hili sakata wakiwa na lengo la kupotosha ukweli uliotolewa leo bungeni tarehe 30/04/2013 na Mchungaji Msigwa. Wengine wameenda mbali zaidi wakiwemo mawaziri wa serikali ya Jakaya Mrisho Kikwete waki-mtuhumu Mchungaji Msigwa ati ni Muongo / mwongo. Kauli hii imezua sintofahamu hapa mtaani kwetu, sisi wasikilizaji na watazamaji tumejiuliza maswali mengi pasipo kuwa na majibu.

Ndugu wanabodi nawaomba tutenge mda wetu kidogo tu, ili kutafakari maswali haya ya msingi, ili mwisho wa siku tupate pa kusimamia :

  • Je ni kweli kwamba vikao vya leo vya bunge vimeendeshwa na kiti cha Spika bila kufuata kanuni na taratibu zilizopo ? Endapo jibu ni ndiyo, je kwa nini hazikufuatwa ?
  • Endapo kanuni zimefuatwa barabara, hizo kanuni zinasemaje kuhusiana na Mbunge aliye tamka maneno ya uongo bungeni ?
  • Je kiti cha Spika kimeshindwa nini kumuamru Mchungaji Msigwa kutoa ushahidi kwa yale aliyo yasoma ?
  • Je Muishiwa Nchimbi anataka kutuaminisha Kiti cha Spika kimemwogopa Mchungaji Msigwa?
Wanabodi naomba kuwasilisha,
Karibuni.

kitendo cha spika kukataa kupokea muongozo au taarifa ya wabunge wa kambi ya upinzani kwa kigezo kuwa wa chama tawala ni mfano dhahiri wa bunge kuongozwa bila kuzingatia kanuni zilizowekwa,
 
Wanabodi heshima kwenu wakuu !!
Nimefuatilia mijadala mingi hapa JF kuhusiana na hotuba ya kambi ya upinzania iliyosomwa rasmi bungeni na Kamanda Mchungaji Msigwa. Nimesikitishwa sana na baadhi ya wachangiaji either kwa kutoelewa,uvivu wa kufikiria, au kutumiwa katika hili sakata wakiwa na lengo la kupotosha ukweli uliotolewa leo bungeni tarehe 30/04/2013 na Mchungaji Msigwa. Wengine wameenda mbali zaidi wakiwemo mawaziri wa serikali ya Jakaya Mrisho Kikwete waki-mtuhumu Mchungaji Msigwa ati ni Muongo / mwongo. Kauli hii imezua sintofahamu hapa mtaani kwetu, sisi wasikilizaji na watazamaji tumejiuliza maswali mengi pasipo kuwa na majibu.

Ndugu wanabodi nawaomba tutenge mda wetu kidogo tu, ili kutafakari maswali haya ya msingi, ili mwisho wa siku tupate pa kusimamia :

  • Je ni kweli kwamba vikao vya leo vya bunge vimeendeshwa na kiti cha Spika bila kufuata kanuni na taratibu zilizopo ? Endapo jibu ni ndiyo, je kwa nini hazikufuatwa ?
  • Endapo kanuni zimefuatwa barabara, hizo kanuni zinasemaje kuhusiana na Mbunge aliye tamka maneno ya uongo bungeni ?
  • Je kiti cha Spika kimeshindwa nini kumuamru Mchungaji Msigwa kutoa ushahidi kwa yale aliyo yasoma ?
  • Je Muishiwa Nchimbi anataka kutuaminisha Kiti cha Spika kimemwogopa Mchungaji Msigwa?
Wanabodi naomba kuwasilisha,
Karibuni.
Mkubwa naomba kama uko Arusha nitafute au kama haupo huku basi naomba unitafute! Katika wachangiaji wakubwa katika kuijadili hotuba ya kutoka kambi ya upinzania iliyosomwa na Mchungaji Msigwa mimi nilikua number moja! sitaki kubishana na watu kuhusu hotuba ile bali ni ukweli usiofichika na uko wazi kua kuna viongozi katika taifa hili wamelihujumu sana kwakujinufaisha kwa nyara za serikali, halafu anasimama kiongozi wa kitaifa kumtetea mtu mmoja na kumuita Mchungaji Msigwa ni muongo???

Naapa kua Emanuel Nchimbi kizazi hiki kinachokuja kupiga kura mwaka 2015 kitawahukumu! Nwatakia sikukuu njema kwa waajiriwa wote! Happy Labor Day.
 
Back
Top Bottom