Huyo aliyeimba hayo anaitwa Faustin Munishi. Nadhani sihitaji kuendelea kueleza mambo yake, kwani wengi kwenye forum hii wanaelewa kuwa huyu jamaa sasa hivi yuko kwenye siasa chafu sana zinazofanana sana na wendawazimu hasa. Ni wanafiki tu hawa jamaa. Au pengine background zao, tabia walizokuwa nazo kabla hawajaanza usanii wa kutangaza "wameokoka" na kujipachika "uchungaji" na "uaskofu", tabia hizo zinawarudia upya njaa inapoisha! Wataalamu wa saikolojia, najua wako wengi kwenye hii forum, wanaweza kutueleza nadharia hizi kama zipo. Yaani aliyekuwa tapeli, malaya, teja nk mambo yakamwendea mrama huko, anapojisalimisha kanisani kutafuta faraja, akiipata bora asipate zaidi ya hiyo faraja, kwani akipata fedha na umaarufu mambo yake yote ya zamani anayarudia kwa kasi. Tumeyaona haya kwa Munishi, Rose Muhando, na wengine. Sina ushahidi wowote dhidi ya Mama Lwakatare, sijui aliingiaje kwenye fani hiyo ya uchungaji, ambapo ya kwake inaendana na ujasiriamali na siasa kwa pamoja. Hata hivyo, historia imeshatufundisha kuwa na mashaka na watu wa aina hii, kwa hiyo ana kazi kubwa ya kutuondolea mashaka haya.
Kuna wakati najiuliza, hivi wale binadamu wenye nia na imani ya dhati kabisa kwa Mungu, kimbilio lao liko wapi? Maana viongozi wa dini mambo yao hata hayafai kusema. Yanatisha yaani. Pengine sasa ni ule wakati wa kila mtu kusimama kivyake na Mungu wake akisubiria hukumu yake bila kutegemea mafundisho kutoka kwa mtu yeyote. Makanisa yatabaki kama social gatherings tu ambako watu wanaenda kusalimiana na kusikiliza kwaya, kama huku Ulaya. Kanisa ninalohudhuria hapa kuna zamu za kuandaa kahawa kwa ajili ya wanaohudhuria misa jumapili. Na wakati wa kutoka, mlangoni tunagawiwa vipeperushi vinavyotangaza jinsi ya kuwapata "singles" wanaosali hapo. Huyo aliyebuni mradi huo naona amefanikiwa, maana ni miongoni mwa makanisa machache yenye misa 3 zinazojaa watu!
Sijui bwana!