Na Said Mwishehe
MCHUNGAJI Dkt. Getrude Rwakatare, ameteuliwa kuwa Mbunge wa Viti Maalumu kupitia CCM kuziba pengo la aliyekuwa Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Bibi Salome Mbatia, aliyekufa kwenye ajali ya gari.
Taarifa zilizopatikana jana jioni Dar es Salaam kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC) zilithibitisha kuteuliwa kwa Mchungaji Rwakatare.
Akizungumza na Majira, mmoja wa maofisa wa NEC, ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini, alisema Mchungaji Rwakatare aliteuliwa kushika wadhifa huo na tayari chama chake kimefahamishwa kuhusiana na uteuzi huo.
"Tumeshaandika barua kwa CCM kuwafahamisha uteuzi wa Mchungaji huyo kushika wadhifa huo. Hivyo kisheria NEC haina ulazima wa kutangaza jina lake kwa wananchi, bali chama chake ndicho kinaweza kufanya hivyo, baada ya kuwapa barua," alisema ofisa huyo.
Naye Ofisa Habari wa NEC, Bw. Bathlomew Wandi, alipoulizwa kuhusiana na uteuzi huo, alisema ni kweli Mchungaji Rwakatare, ameteuliwa na tayari barua ya kukitaarifu chama chake imeshakwenda.
"Taarifa nilizonazo ni kwamba tayari CCM wameandikiwa barua ya uteuzi huo, lakini ni vema mkapata maelezo zaidi kutoka kwa viongozi wa CCM kwani ndio wenye jukumu la kumtangaza mtu wao, kutokana na kuchaguliwa kwake," alisema Bw. Wandi.
Mwaka 2005, Dkt. Rwakatare aliingia katika kinyang'anyiro cha kupata nafasi hiyo kupitia mkoa wa Morogoro, lakini alishindwa; na sasa ameingia kwa utaratibu wa mlolongo wa nafasi walizopata mwaka huo.
Kuingia kwa Mchungaji huyo bungeni kwa tiketi ya CCM kunafanana na jinsi alivyoingia Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Dkt. Christine Ishengoma, ambaye naye aliteuliwa kushika nafasi hiyo, baada ya kifo cha aliyekuwa mbunge wa viti maalumu kupitia Jumuiya ya Vijana wa CCM, marehemu Amina Chifupa.
Kutokana na uteuzi huo, Dkt. Rwakatare anatarajiwa kuapishwa katika Mkutano wa 10 wa Bunge unaotarajiwa kufanyika Dodoma kuanzia Januari 29 mwakani.
Dkt. Rwakatare ambaye ni Mchungaji wa Kanisa na Assemblies of God Mikocheni, anamiliki shule na vyuo vya St. Mary's na kituo cha redio cha Praise Power Radio.
Source: Majira.
Kumbe akifa mtu anateuliwa aliyefuata kwa kura uchaguzi uliopita? Hivi wadau sheria ndivyo inavyosema au huu ni utaratibu wa CCM? Kwa mtaji huu wale katika viti maalumu wanaoamini "vipapai" watavisaka kwa udi na uvumba!