Mchungaji Faustine Munishi: Yanayofanyika Chato, Butiama inasikitika...

Kuna mbunge mmoja enzi za Nyerere aliomba Barbara ya lami kujengwa toka Musoma hadi Butiama, Mwalimu akusubiri alimtimua mazima. Baada ya Mwita kutimuliwa ubunge alirudi kijijini kulima na hadi Mwalimu anatoka madarakani hakuwahi kumfikiria nafasi yoyote
Nyerere nafikiri kuna kitu watu wa Butiama walimchafua akaona maendeleo ayaelekeze K'jaro. Nakumbuka pia hakupenda maendeleo Bukoba tuseme ukanda wote wa ziwa. Lakini ya Kasikazini aliyapa kipa umbele. Hivyo mnapo mlinganisha na wa sasa jaribu kujichunga msije mkafukua makaburi. Kuna watu wakikumbuka wanaumia.
 
Kama hujui geografia ya Nchi yako heri usiandike maana hapa unajidhalilisha. Hujui Chato na Ziwa victoria kuna umbali gani? Kwa taarifa Pwani ya Ziwa Victoria ndipo ulipo mji wa Chato.
Only great thinkers will read between the lines na kuelewa. You are not one of them
 
Hapa umenichokoza !! Katika makabila 120 ya Tanzania wajaluo hawamo ?!. Kama huwakubali wape na wilaya zao mbili (Tarime & Rorya) waende nazo
Usihangaike hawa hawajui nchi yao! Hawajui kuwa hata wakikuyu Tanzania wapo japo ni wachache! Mfano ni Joseph Mungai aliye kuwa waziri wa Tanzania kwa awamu nne. Ni kabila lililokuja Tanzania kutumika katika mashamba ya Chai. Wajaruo ambao huyu jamaa hawajui walioshika nyadhifa kubwa ni mzee Apio aliyekuwa katibu wa Nyerere kwa miaka mingi. Mwingine ni Professor Sarungi aliye kuwa hata waziri wa ulinzi wakati fulani (baba yake Maria Sarungi wa upinzani). Kuna hata mmoja hakujua kuwa Chato iko mwaroni mwa Lake Victoria!
 
Naona unavyojitahidi kutoa porojo, ok ukishamaliza nenda pale Ufipa ukachukue kadi ya ugombea jimbo la Singida Mashariki, wahi mapema maake nafasi ni chache.
I have never ever seen a warthog that can read and write till today!!! Too sad.
 
Hela kuongeza mishahara hatuna ila mradi ya chato airport, burigi chato, uwanja wa mpira ,bandari ,meli ya MV chato zipo .
 
Kama kila kitu kimepelekwa chato na huyo chunga nguruwe si ahamie hukohuko chato akafaidi,,kama wachaga hawakupendelea kwao,kwanini Kilimanjaro imeendelea kuliko mikoa mingi ya Tanzania?aache wivu,kwani chato siyo Tanzania?
 
hahahaha kumbe hoja imetolewa na mchaga
 
Mleta mada ni Munisi? Yule mpiga kinanda mikutano ya injili ya Mzee Moses Kulola Mzee wa kisukuma? Ambaye Ndie aliyemnyanyua Hadi kufikia kujulikana kitaifa na kimataifa ? Munisi Munisi Munisi laana ya Mzee Moses Kulola na iwe juu yako kwa roho mbaya kwa ndugu wa Moses Kulola wasukuma aliyekutendea mema bila kukubagua kuwa wewe mchaga.Mene mene Tekeli na peresi kwako na ukoo wako Munisi.
huyu ni Munishi wa Kibosho Not Munisi.
 
Munishi naye kaanza kuingia kwenye siasa?

Any way, labda keshaagana na nyonga kabla ya kuruka.
Munishi muda mrefu amejikita kuandika magazeti na tangu muda mrefu anaikosoa serikali ya ccm hata ana wimbo wake mmoja mwanzo mwisho anaikosoa ccm na kudai ni chama chakavu hivyo siyo Leo kaanza kukosoa na yeye ni mtumishi Wa Mungu anapaswa kusema ukweli siyo kumumunya maneno na haipaswi kuwa mnafiki mtumishi Wa Mungu
 
Nyambaf..!
Another poyoyo...!!Jikite kwenye hoja siyo kuzungumzia mtu..!! Hatutaki kujua huyu ni Munishi yupi...haituhusu!!!
Hoja hapa ni Magufuli kwanini anatumia KODI ZA WATZ KUNEEMESHA CHATO..??This is the thing!
hivi chato ipo msumbiji au morroco???
 
Mwalimu Nyerere ambaye pia ni Baba wa Taifa hili na Kiongozi aliyeliongoza Taifa hili kwa takribani miaka 26 anapoinua macho yake na kuitazama CHATO ya Magufuli anasikitika na kushindwa kupumzika kwa amani ndani ya kaburi lake.

Licha ya Mwalimu Nyerere kuwa Rais wa Tanganyika na baadae Tanzania kwa miaka hiyo yote aliitazama Tanzania kama nchi na kuleta juhudi kuijenga Tanzania nzima bila upendeleo wa aina yoyote. Hakuiweka Butiama mbele zaidi kuliko Nachingwea, Namtumbo au Kishumundu.

Mwalimu Nyerere angetaka Butiama iwe paradiso ya Tanzania angeweza kufanya hivyo. Mwalimu Nyerere angetaka makao makuu ya Tanzania, Bunge, Ikulu vikae Butiama angeweza.
Angetaka Butiama kuwe na uwanja wa Kimataifa wa kutua Concord na Antonov angeweza.

Mwalimu Nyerere angetaka makao makuu ya Shirika la Posta na ATLC yawe Butiama angeweza kufanya hivyo.

Hata angetaka mitaa, vijiji na vitongoji vya Butiama viwe na barabara za lami na taa za kuongozea magari hadi Mwitongo angeweza kufanya hivyo.
Lakini Mwalimu Nyerere alifahamu kuwa yeye sio Rais wa Butiama bali ni Rais wa Tanzania. Hakuipendelea Butiama aliweka mgawanyo sawa wa shughuli za maendeleo hata kama haikuwa 100% lakini walau aliweza hilo kwa zaidi ya 90%.

Daniel Yona alipokuwa Waziri wa Fedha na Mbunge wa Same mkoani Kilimanjaro wananchi wa same waliwahi kumuambia kuwa kwa nini hawaletei maji, umeme na barabara za lami hadi Vijijini ilihali yeye ni Waziri wa Fedha? Daniel aliwajibu kuwa yeye ni Waziri wa Fedha wa Tanzania nzima na wala sio Waziri wa Fedha wa Same hivyo hawezi kudhulumu maeneo mengine ili kuinufaisha Same.

Daniel Yona angetaka kutumia nafasi yake kama Waziri wa Fedha kuipendelea Same kwa gharama za kudhulumu maeneo mengine angeweza. Daniel pamoja na mapungufu yake mengine alitambua kuwa yeye ni Waziri wa Fedha wa Tanzania nzima na siyo Same.

Mwalimu Nyerere alitambua kuwa yeye ni Rais wa Tanzania nzima na sio Rais wa Butiama.

Benjamin Mkapa alitambua kuwa yeye ni Rais wa Tanzania na siyo Rais wa Masasi Mtwara.

Jakaya Kikwete alitambua kuwa yeye ni Rais wa Tanzania na sio Rais wa Bagamoyo pekee.

Cleopa David Msuya alitambua kuwa yeye ni Waziri wa Fedha, Waziri wa Viwanda na Waziri Mkuu wa Tanzania nzima na wala sio wa Mwanga Kilimanjaro pekee. Alilifahamu hilo na alilisimamia.

Edward Moringe Sokoine alitambua kuwa yeye ni Waziri Mkuu wa Tanzania nzima na wala sio Monduli pekee.

Alilisimamia hilo na alikuwa mkali kweli kweli kuhakikisha hakuna upendeleo.
Fredrick Sumaye alitambua kuwa yeye ni Waziri Mkuu wa Tanzania nzima na wala sio Hanang' pekee.

Sasa leo najiuliza kunani CHATO?CHATO kuna nini?

Hadi sasa Magufuli amekuwa Rais wa Tanzania kwa takribani miaka 4 pekee lakini ndani ya miaka hiyo 4 kijiji chake cha CHATO sasa hivi kinazidi mikoa mingi sana. Miradi mingi, mikubwa inakimbiziwa huko CHATO.

Machi 9, 2018 Rais Magufuli alifungua tawi la CRDB, CHATO Kijiji cha Kilimani alipozaliwa.

June 2016 Serikali ilianza rasmi kujenga uwanja wa ndege ambao leo hii Kigwangala amesema Rais Magufuli amesema uwe uwanja wa Kimataifa, hivyo utaitwa uwanja wa kimataifa wa CHATO kwa kimombo CHATO International Airport.

June 2, 2019 Serikali ilipandisha hadhi Pori la akiba la Burigi lililopo huko kijijini CHATO kuwa hifadhi ya taifa ya Burugi na kwa kuwa hakukuwa na hadhi ya kuwa hifadhi ya Taifa wanyama mbali mbali wakiwemo Twiga wakasafirishwa kwa magari kupelekwa CHATO.

Mwaka jana 2018 uwekaji wa taa za kuongoza magari ulikamilika huko kijiji cha CHATO. Na siku hii ya leo Serikali imesema itajenga uwanja mkubwa wa mpira huko CHATO. Uwanja huo unatajwa kuwa utakuwa wa Pili kwa ukubwa nchini baada ya ule wa Benjamin Mkapa Dar es Salaam lakini utakuwa wa kwanza wa kisasa zaidi nchini.

Dikteta uchwara Mobutu wa Zaire aliponyakua madaraka kwa mabavu alijenga uwanja wa Kimataifa kijijini kwako. Uwanja huo ulikuwa una uwezo wa kutua ndege kubwa aina ya Concord. Kijiji chake alikijenga na kuwa paradiso ya Congo.

Mobutu aliamrisha kuwekwe Hifadhi ya wanyamapori kijijini kwake. Akajenga jumba la kifahari kijijini kwake msituni.
Ndege za kifahari zikatua kijijini kwake kutoka Ulaya na Marekani na kupora mali za Zaire kimya kimya.

Dikteta uchwara Mobutu alipokufa vitu vyote hivyo vilizikwa katika kaburi la sahau na kijiji chake kimesalia mahame. Hata ile Meli yake ya kifahari aliyozunguka nayo mto Congo haipo tena.

Kesho ni nzuri kuliko jana. Mwalimu Nyerere aliupinga ubaguzi na upendeleo si kwa maneno tu bali kwa vitendo. Aliuhubiri na kuuishi uzalendo. Hakuishia kuuimba uzalendo.

Mimi nimewahi kuishi Musoma kwa zaidi ya miaka 4.Niligundua kuwa kumbe mkoa wa Mara ndiyo mbuga ya Serengeti ilipo.Lakini wanaofaidi ni watu wa Arusha.Nyerere hakuwa na upendeleo wa kwao.Lakini alilkuwa na udhaifu wa kutelekeza kwao.
 
Imeandikwa kwenye biblia ",Wafu hawajui neno lolote wala hawana ijara tena, maana kumbukumbu lao limesahauliwa "Mhubiri 9:5
Nyerere Huko alipo hajui lolote linalojiri ndio maana yake.
sio kila unachokiamini wewe ndio sahihi ,duniani watu wana imani tofauti tofauti,ni nani toka dunia iumbwe aliwahi kukaa huko kaburini akaona kuwa wafu hawajui neno lolote?
 
Mwalimu Nyerere ambaye pia ni Baba wa Taifa hili na Kiongozi aliyeliongoza Taifa hili kwa takribani miaka 26 anapoinua macho yake na kuitazama CHATO ya Magufuli anasikitika na kushindwa kupumzika kwa amani ndani ya kaburi lake.

Licha ya Mwalimu Nyerere kuwa Rais wa Tanganyika na baadae Tanzania kwa miaka hiyo yote aliitazama Tanzania kama nchi na kuleta juhudi kuijenga Tanzania nzima bila upendeleo wa aina yoyote. Hakuiweka Butiama mbele zaidi kuliko Nachingwea, Namtumbo au Kishumundu.

Mwalimu Nyerere angetaka Butiama iwe paradiso ya Tanzania angeweza kufanya hivyo. Mwalimu Nyerere angetaka makao makuu ya Tanzania, Bunge, Ikulu vikae Butiama angeweza.
Angetaka Butiama kuwe na uwanja wa Kimataifa wa kutua Concord na Antonov angeweza.

Mwalimu Nyerere angetaka makao makuu ya Shirika la Posta na ATLC yawe Butiama angeweza kufanya hivyo.

Hata angetaka mitaa, vijiji na vitongoji vya Butiama viwe na barabara za lami na taa za kuongozea magari hadi Mwitongo angeweza kufanya hivyo.
Lakini Mwalimu Nyerere alifahamu kuwa yeye sio Rais wa Butiama bali ni Rais wa Tanzania. Hakuipendelea Butiama aliweka mgawanyo sawa wa shughuli za maendeleo hata kama haikuwa 100% lakini walau aliweza hilo kwa zaidi ya 90%.

Daniel Yona alipokuwa Waziri wa Fedha na Mbunge wa Same mkoani Kilimanjaro wananchi wa same waliwahi kumuambia kuwa kwa nini hawaletei maji, umeme na barabara za lami hadi Vijijini ilihali yeye ni Waziri wa Fedha? Daniel aliwajibu kuwa yeye ni Waziri wa Fedha wa Tanzania nzima na wala sio Waziri wa Fedha wa Same hivyo hawezi kudhulumu maeneo mengine ili kuinufaisha Same.

Daniel Yona angetaka kutumia nafasi yake kama Waziri wa Fedha kuipendelea Same kwa gharama za kudhulumu maeneo mengine angeweza. Daniel pamoja na mapungufu yake mengine alitambua kuwa yeye ni Waziri wa Fedha wa Tanzania nzima na siyo Same.

Mwalimu Nyerere alitambua kuwa yeye ni Rais wa Tanzania nzima na sio Rais wa Butiama.

Benjamin Mkapa alitambua kuwa yeye ni Rais wa Tanzania na siyo Rais wa Masasi Mtwara.

Jakaya Kikwete alitambua kuwa yeye ni Rais wa Tanzania na sio Rais wa Bagamoyo pekee.

Cleopa David Msuya alitambua kuwa yeye ni Waziri wa Fedha, Waziri wa Viwanda na Waziri Mkuu wa Tanzania nzima na wala sio wa Mwanga Kilimanjaro pekee. Alilifahamu hilo na alilisimamia.

Edward Moringe Sokoine alitambua kuwa yeye ni Waziri Mkuu wa Tanzania nzima na wala sio Monduli pekee.

Alilisimamia hilo na alikuwa mkali kweli kweli kuhakikisha hakuna upendeleo.
Fredrick Sumaye alitambua kuwa yeye ni Waziri Mkuu wa Tanzania nzima na wala sio Hanang' pekee.

Sasa leo najiuliza kunani CHATO?CHATO kuna nini?

Hadi sasa Magufuli amekuwa Rais wa Tanzania kwa takribani miaka 4 pekee lakini ndani ya miaka hiyo 4 kijiji chake cha CHATO sasa hivi kinazidi mikoa mingi sana. Miradi mingi, mikubwa inakimbiziwa huko CHATO.

Machi 9, 2018 Rais Magufuli alifungua tawi la CRDB, CHATO Kijiji cha Kilimani alipozaliwa.

June 2016 Serikali ilianza rasmi kujenga uwanja wa ndege ambao leo hii Kigwangala amesema Rais Magufuli amesema uwe uwanja wa Kimataifa, hivyo utaitwa uwanja wa kimataifa wa CHATO kwa kimombo CHATO International Airport.

June 2, 2019 Serikali ilipandisha hadhi Pori la akiba la Burigi lililopo huko kijijini CHATO kuwa hifadhi ya taifa ya Burugi na kwa kuwa hakukuwa na hadhi ya kuwa hifadhi ya Taifa wanyama mbali mbali wakiwemo Twiga wakasafirishwa kwa magari kupelekwa CHATO.

Mwaka jana 2018 uwekaji wa taa za kuongoza magari ulikamilika huko kijiji cha CHATO. Na siku hii ya leo Serikali imesema itajenga uwanja mkubwa wa mpira huko CHATO. Uwanja huo unatajwa kuwa utakuwa wa Pili kwa ukubwa nchini baada ya ule wa Benjamin Mkapa Dar es Salaam lakini utakuwa wa kwanza wa kisasa zaidi nchini.

Dikteta uchwara Mobutu wa Zaire aliponyakua madaraka kwa mabavu alijenga uwanja wa Kimataifa kijijini kwako. Uwanja huo ulikuwa una uwezo wa kutua ndege kubwa aina ya Concord. Kijiji chake alikijenga na kuwa paradiso ya Congo.

Mobutu aliamrisha kuwekwe Hifadhi ya wanyamapori kijijini kwake. Akajenga jumba la kifahari kijijini kwake msituni.
Ndege za kifahari zikatua kijijini kwake kutoka Ulaya na Marekani na kupora mali za Zaire kimya kimya.

Dikteta uchwara Mobutu alipokufa vitu vyote hivyo vilizikwa katika kaburi la sahau na kijiji chake kimesalia mahame. Hata ile Meli yake ya kifahari aliyozunguka nayo mto Congo haipo tena.

Kesho ni nzuri kuliko jana. Mwalimu Nyerere aliupinga ubaguzi na upendeleo si kwa maneno tu bali kwa vitendo. Aliuhubiri na kuuishi uzalendo. Hakuishia kuuimba uzalendo.
Mmmm,kuna tatizo kweli,kuna haja ya kujitafakari upya.Institution ya Urais ni kwa ajili ya Tanzania nzima.You have a point.
 
Back
Top Bottom