Mchungaji Faustine Munishi: Yanayofanyika Chato, Butiama inasikitika...

Mwalimu Nyerere ambaye pia ni Baba wa Taifa hili na Kiongozi aliyeliongoza Taifa hili kwa takribani miaka 26 anapoinua macho yake na kuitazama CHATO ya Magufuli anasikitika na kushindwa kupumzika kwa amani ndani ya kaburi lake.

Licha ya Mwalimu Nyerere kuwa Rais wa Tanganyika na baadae Tanzania kwa miaka hiyo yote aliitazama Tanzania kama nchi na kuleta juhudi kuijenga Tanzania nzima bila upendeleo wa aina yoyote. Hakuiweka Butiama mbele zaidi kuliko Nachingwea, Namtumbo au Kishumundu.

Mwalimu Nyerere angetaka Butiama iwe paradiso ya Tanzania angeweza kufanya hivyo. Mwalimu Nyerere angetaka makao makuu ya Tanzania, Bunge, Ikulu vikae Butiama angeweza.
Angetaka Butiama kuwe na uwanja wa Kimataifa wa kutua Concord na Antonov angeweza.

Mwalimu Nyerere angetaka makao makuu ya Shirika la Posta na ATLC yawe Butiama angeweza kufanya hivyo.

Hata angetaka mitaa, vijiji na vitongoji vya Butiama viwe na barabara za lami na taa za kuongozea magari hadi Mwitongo angeweza kufanya hivyo.
Lakini Mwalimu Nyerere alifahamu kuwa yeye sio Rais wa Butiama bali ni Rais wa Tanzania. Hakuipendelea Butiama aliweka mgawanyo sawa wa shughuli za maendeleo hata kama haikuwa 100% lakini walau aliweza hilo kwa zaidi ya 90%.

Daniel Yona alipokuwa Waziri wa Fedha na Mbunge wa Same mkoani Kilimanjaro wananchi wa same waliwahi kumuambia kuwa kwa nini hawaletei maji, umeme na barabara za lami hadi Vijijini ilihali yeye ni Waziri wa Fedha? Daniel aliwajibu kuwa yeye ni Waziri wa Fedha wa Tanzania nzima na wala sio Waziri wa Fedha wa Same hivyo hawezi kudhulumu maeneo mengine ili kuinufaisha Same.

Daniel Yona angetaka kutumia nafasi yake kama Waziri wa Fedha kuipendelea Same kwa gharama za kudhulumu maeneo mengine angeweza. Daniel pamoja na mapungufu yake mengine alitambua kuwa yeye ni Waziri wa Fedha wa Tanzania nzima na siyo Same.

Mwalimu Nyerere alitambua kuwa yeye ni Rais wa Tanzania nzima na sio Rais wa Butiama.

Benjamin Mkapa alitambua kuwa yeye ni Rais wa Tanzania na siyo Rais wa Masasi Mtwara.

Jakaya Kikwete alitambua kuwa yeye ni Rais wa Tanzania na sio Rais wa Bagamoyo pekee.

Cleopa David Msuya alitambua kuwa yeye ni Waziri wa Fedha, Waziri wa Viwanda na Waziri Mkuu wa Tanzania nzima na wala sio wa Mwanga Kilimanjaro pekee. Alilifahamu hilo na alilisimamia.

Edward Moringe Sokoine alitambua kuwa yeye ni Waziri Mkuu wa Tanzania nzima na wala sio Monduli pekee.

Alilisimamia hilo na alikuwa mkali kweli kweli kuhakikisha hakuna upendeleo.
Fredrick Sumaye alitambua kuwa yeye ni Waziri Mkuu wa Tanzania nzima na wala sio Hanang' pekee.

Sasa leo najiuliza kunani CHATO?CHATO kuna nini?

Hadi sasa Magufuli amekuwa Rais wa Tanzania kwa takribani miaka 4 pekee lakini ndani ya miaka hiyo 4 kijiji chake cha CHATO sasa hivi kinazidi mikoa mingi sana. Miradi mingi, mikubwa inakimbiziwa huko CHATO.

Machi 9, 2018 Rais Magufuli alifungua tawi la CRDB, CHATO Kijiji cha Kilimani alipozaliwa.

June 2016 Serikali ilianza rasmi kujenga uwanja wa ndege ambao leo hii Kigwangala amesema Rais Magufuli amesema uwe uwanja wa Kimataifa, hivyo utaitwa uwanja wa kimataifa wa CHATO kwa kimombo CHATO International Airport.

June 2, 2019 Serikali ilipandisha hadhi Pori la akiba la Burigi lililopo huko kijijini CHATO kuwa hifadhi ya taifa ya Burugi na kwa kuwa hakukuwa na hadhi ya kuwa hifadhi ya Taifa wanyama mbali mbali wakiwemo Twiga wakasafirishwa kwa magari kupelekwa CHATO.

Mwaka jana 2018 uwekaji wa taa za kuongoza magari ulikamilika huko kijiji cha CHATO. Na siku hii ya leo Serikali imesema itajenga uwanja mkubwa wa mpira huko CHATO. Uwanja huo unatajwa kuwa utakuwa wa Pili kwa ukubwa nchini baada ya ule wa Benjamin Mkapa Dar es Salaam lakini utakuwa wa kwanza wa kisasa zaidi nchini.

Dikteta uchwara Mobutu wa Zaire aliponyakua madaraka kwa mabavu alijenga uwanja wa Kimataifa kijijini kwako. Uwanja huo ulikuwa una uwezo wa kutua ndege kubwa aina ya Concord. Kijiji chake alikijenga na kuwa paradiso ya Congo.

Mobutu aliamrisha kuwekwe Hifadhi ya wanyamapori kijijini kwake. Akajenga jumba la kifahari kijijini kwake msituni.
Ndege za kifahari zikatua kijijini kwake kutoka Ulaya na Marekani na kupora mali za Zaire kimya kimya.

Dikteta uchwara Mobutu alipokufa vitu vyote hivyo vilizikwa katika kaburi la sahau na kijiji chake kimesalia mahame. Hata ile Meli yake ya kifahari aliyozunguka nayo mto Congo haipo tena.

Kesho ni nzuri kuliko jana. Mwalimu Nyerere aliupinga ubaguzi na upendeleo si kwa maneno tu bali kwa vitendo. Aliuhubiri na kuuishi uzalendo. Hakuishia kuuimba uzalendo.
Sijakuelewa. CRDB siyo mali ya Serikali. Ilijengwa na Kimei.

Wakati wa Mwl uchumi ulikuwa chini sana kiasi cha kushindwa hata kupanga Manzese na mitaa mingine ya Dar.

Wakati wa Mwl hatukuwa na rasilimali watu na fedha za kutosha kuweza kufanya unayolalamikia.

Acha ubaguzi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom