Mchungaji Antony Lusekelo 'Mzee wa Upako' afunguka baada ya kashfa

Namjua Happy Ngasala...sikujua kama Lusekelo ndio mume wake...
N'lisikiaga tu kaolewa na mchungaji...choka mbaya (maana kwao kidogo walikuwa mambo safi)...kumbe wameshatosoa
Alisoma na dadangu enzi za mwalimu...


Mke wa mchungaji huyo, Happiness Ngasala aliiambia Mwananchi kuwa mchungaji huyo alikuwa nyumbani kwake.

“Mume wangu yupo nyumbani hapa. Hizo taarifa hazina ukweli wowote,” alisema.

Kuhusu madai ya kutoa maneno nayo, Ngasala alisema: “Hata huo waraka si wa kweli. Mchungaji hawezi kutoa maneno kama hayo.”

Ngasala, ambaye alithibitisha kwamba mume wake yupo nyumbani alipoombwa ampe Mzee wa Upako simu ili mwandishi azungume naye, alisema apigiwe kwenye simu yake.

Mwandishi alipomwambia kwamba mchungaji huyo amepigiwa simu yake lakini hajapokea, alisema mume wake hajakamatwa na kwamba kuna kinyozi alifika kwa ajili ya kumnyoa nywele, hivyo apigiwe baadaye.
 
Kwanini hampendi jirani yake kama nafsi yk wakati biblia inaagiza tupendane ni tatizo
 
Back
Top Bottom