Mchungaji aliyedai kuvunjiwa Kanisa Zanzibar afunguka. Serikali yatangaza kumsaka, yasema ni nyumba siyo Kanisa

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,460
Siku chache tangu kuripotiwa kwa taarifa za kuvunjwa kwa Kanisa la T.A.G lililopo Sebleni, Unguja ripoti kamili ya kilichotokea imetolewa kutoka upande wa kanisa pamoja na upande wa Serikali ya Zanzibar.

Mchungaji wa kanisa hilo linaloelezwa kuwa limevunjwa, David Victor Suna amefunguka kilichotokea kwa kusema:

MCHUNGAJI AFUNGUKA
“Ni kweli wamevunja nyumba yetu ya ibada licha ya kutambua kuwa tuna uhalali wa kila kitu, na suala hilo kwa sasa lipo kwa wanasheria wetu wanalishughulikia.

“Eneo hilo nilinunua kihalali kabisa kwa Sh milioni 16 na wakati nanunua nilikuta kuna banda ambalo lilikuwa shemu ya mauzo ya kiwanja, nilichofanya nikaboresha kwa kujenga ukuta.

“Lakini baada ya kuanza kuwa tunasali, nikapata malalamiko kuwa wakazi wa hapo hawataki kanisa, wakawa wanakuja viongozi kadhaa wa Serikali kukagua wakiniambia malalamiko ya uwepo wa kanisa letu mahali hapo.

“Kwanza waliniambia nimejenga ukuta kimakosa, kwa kuwa sina kibali cha kujenga ukuta, nikawaambia sawa hilo nakiri kwa kuwa sikuwa najua kama ukta unahitaji kibali, nikawaambia nitafuata mchakato wa kupata kibali kwa mamlaka husika.

“Baada ya mvutano wa muda mrefu nilienda hadi kwa Mkuu wa Wilaya akaniambia kama kama ninataka kibali cha nyumba ya makazi ya kawaida nitapata lakini kama ni kuhusu kanisa hapo siyo sehemu sahihi na hawatanipa kibali kwa kuwa wakazi wa eneo hilo hawataki kanisa.

“Siku hiyo ndiyo nikashangaa wamekuja wakavunja kwa kutumia mgongo wa Manispaa. Viongozi wetu wakuu akiwemo Askofu Mkuu amesema niwe kimya, nisifanye chochote kwa sasa, wao ndiyo watakaotoa tamko kwa kuwa suala letu limefika ngazi ya kitafa.

“Mimi ni mkazi wa Unguja miaka mingi, najua wanachofanya ni kitu ambacho wanakifanya muda mrefu, kuna upande ambao unakuwa una nguvu kubwa kiimani kuliko mwingine.

“Mimi kwa sasa nipo kimya, hata kule walipofunja siendi kwa kuwa sitaki matatizo, sijafanyiwa fujo zaidi ya siku ile ambayo walivunja, lakini mpaka sasa (Machi 11, 2022) sijapata tatizo lolote.”

TAMKO LA SERIKALI, LAMSAKA MCHUNGAJI
Mkuu wa Wilaya wa Mjini Magharibi kisiwani Unguja, Rashid Msaraka amezungumza na waandishi wa habari leo Machi 11, 2022 baada ya kufika eneo la tukio.

“Mamlaka zinazohusiana na utabiri wa hali ya hewa, zimetoa tathmini yao kuhusu mvua zinazotarajiwa kunyesha hivi karibuni, nikatoa maelekezo kwa Mkurugenzi wa Manispaa kuwa na tahadhari ya maeneo hatarishi, moja kati ya maeneo hayo ni hiyo iliyobomolewa.

“Nyumba mojawapo iliyobomolewa ni nyumba ya kawaida lakini taarifa inayosambaa ni kanisa, hapana mimi sina kibali cha kujengwa kwa kanisa.

“Hivyo, imevunjwa kwa kuwa ni sehemu ya nyumba zilizokuwa hatarishi, tunaweka mazingira sawa, siyo hapa tu bali ni maeneo yote.

“Yote yanayoendelea mitandaoni kuwa kuna maandalizi ya vita ya Waislamu dhidi ya Wakristo siyo kweli.

“Katika taarifa zinazosambaa kuna mtu anaitwa David Suna, sijui kama ni kiongozi wa kawaida au kiongozi wa dini, hatumfahamu, nimempa maelekezo Kamanda OCD kumtafuta huyo Daudi Suna ili kutoa maelezo ya kinachoendelea mitandaoni.

“Sisi tumemwambia ODC hiyo clip inayosambaza ni mbaya na ni ya uchochezi.

“Kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kila mtu ana haki ya kuambudu lakini lazima kuwe na utaratibu.

“Nasisitiza kuwa hapakuwa na kanisa, kulikuwa na nyumba za kuishi. Tunatoa taarifa kuwa hakuna rabsha yoyote.

“Tumewaambia wale ambao wanaona hawajatendewa haki basi waje watuambie lakini hakuna mtu hata mmoja aliyejitokeza.

“Tutahakikisha tunawalinda raia wote bila kuwa na ubaguzi, usalama wa raia wa kila mtu ni muhimu. Zanzibar ni sehemu ambayo ina historia ya kuw ana makanisa tangu enzi na enzi, hatutamvumilia mtu au watu ambao watakuwa wanania ya kuharibu taswira ya Serikali ya Zanzibar.”

Pia Soma~~ Zanzibar: Kanisa la T.A.G pamoja na makazi ya Mchungaji wake Daudi Suna, yamebomolewa na wanaodaiwa ni wakazi wa eneo hilo
 
Ukweli tuuseme tu, hata kama unatuuma.
Suala la uvumilivu wa kiimani kwa Zanzibar uko chini sana. Kujenga kanisa huwa kunawakera na kuwaudhi mnoo watu waliopo Zanzibar. Makanisa yanayoheshimiwa ni yale ya kihistoria ambayo yanafanya watalii waje, tofauti na hapo yangekuwa yameshavunjwa siku nyingi.

Kwa Zanzibar malaya, mashoga na mateja wana thamani kubwa kuliko muumini wa Kikristo mwenye msimamo.
 
Nyumba ya mtu ni ruksa kuivunja?
 
Kwa hyo mabwabwa Wana thaman kubwa huko zenji?

Ila tambueni dini tumeletewa na mkoloni

Watu hawajiulizi mbona hakuna nabii mwenye rangi nyeusi yaan mwafrika ina maana SS weusi tulitengwa hatukuhtaji dini

Watakatifu wote watu weupe weus n wakuhesabu Sana Tena had tuwalazmishe

Msikitini lugha n kiarabu TU Kwan MUUMBA hasikii kiswahili kwann tusiswali kiswahili ili kila mtu aelewe?

TUJIOKOE KIFIKRA

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Ukweli tuuseme tu, hata kama unatuuma.
Suala la uvumilivu wa kiimani kwa Zanzibar uko chini sana. Kujenga kanisa huwa kunawakera na kuwaudhi mnoo watu waliopo Zanzibar. Makanisa yanayoheshimiwa ni yale ya kihistoria ambayo yanafanya watalii waje, tofauti na hapo yangekuwa yameshavunjwa siku nyingi.

Kwa Zanzibar malaya, mashoga na mateja wana thamani kubwa kuliko muumini wa Kikristo mwenye msimamo.

Mkuu Zanzibar ni nchi ya kiislamu, 99% ya watu wake ni waislamu, kwahiyo hakuna cha ajabu kuwa na mifumo ya kiislamu kwenye maisha yao, ni tofauti na Bara ambapo uwiano wa dini hizi mbili ni mkubwa nearly 50 - 50, So cha muhimu ni kufahmu kuwa haiwezekani mazingira ya Zanzibar yakawa sawa na Bara. Tujaribu kulitathmini kwa uandani na sio kuishabiki. Tatizo kuu la Zanzibar ni suala la Makanisa kuwa yanaengezeka kwa kasi kila siku zinavyokwenda, Na hilo linawafanya wananchi wao wengi kuwa insecure. Nchi nyingi ambazo ziko dominated na dini moja kwa zaidi ya 90% ni lazima watu wa dini nyengine wata experience mambo kama hayo, na hasa wakiwa Wageni.
 
Mbona wanasemaje uislam unashamiri sana Europe?
 
Huyo mkuu wa Wilaya mbona ana akili za kipumbavu namna hii,tangu lini mamlaka zinabomoa nyumba kisa mamlaka ya hali ya hewa imesema kwamba kutakuwa na mvua?

Halafu nyumba iliyobomolewa ni moja tu?kuna jambo limejificha hapo.
 
Mbona wanasemaje uislam unashamiri sana Europe?

licha ya kuwa Europe kuna nchi ambazo zinakua na haki nyingi za kibinaadamu mpaka nyengine za aibu lakini bado hawapo huru kama wanavyokua katika maeneo yao, na zaidi ni kuwa Uislamu Europe unashamiri kutokana na Wazawa wengi kuingia katika waislamu, na sio kwa kutegemea wageni.
 
Ukweli tuuseme tu, hata kama unatuuma.
Suala la uvumilivu wa kiimani kwa Zanzibar uko chini sana. Kujenga kanisa huwa kunawakera na kuwaudhi mnoo watu waliopo Zanzibar. Makanisa yanayoheshimiwa ni yale ya kihistoria ambayo yanafanya watalii waje, tofauti na hapo yangekuwa yameshavunjwa siku nyingi.

Kwa Zanzibar malaya, mashoga na mateja wana thamani kubwa kuliko muumini wa Kikristo mwenye msimamo.
Pamoja na hayo hawa jamaa wanamakelele sana.
 
Back
Top Bottom