Mchumba wangu ana karama ya unabii, ananitisha!

kuna mambo mawili, ni mchumba wako maana yake ni girlfriend huwa mnafanya uasherati pamoja au ni mchumba yule aliyeokoka ambaye mnasubiri hadi ndoa ndio mshirikiane tendo? kama hajaokoka na huwa mnafanay dhambi ya uasherati, pole sana, upo na muonaji ambaye ni sawa tu na mganga wa kienyeji, kwasababu Roho wa Mungu huwa hakai mahali pachafu penye uzinzi na uasherati. wapo waonaji wengi tu wenye mapepo ya kuona na kutabiri, wengine ni wajukuu wa waganga wa kienyeji hivyo wanarithishwa mikoba tangu utotoni, wengine mashetani ya ukoo yamewavamia, watu wa aina hiyo nawajua wengi sana na wanaweza kukuambia kitu ambacho ni cha kweli kitatokea. kwahiyo kama hamjaokoka, ni kwamba unashirikiana na mtu mwenye mapepo na yatakuingia na wewe kwasababu wewe na yeye ni mwili mmoja kutokana na mnavyoingiliana. ila kama ameokoka, na wewe umeokoka, mshikilie huyo awe mkeo. ni lulu hao.
We nadhani haujasoma huo uzi vizuri, kuna sehemu kasema mchumba wake ni bikra.
 
Wakuu habarini za wakati huu...

Niliwahi kuleta Uzi humu kuhusu mchumba wangu ambaye ni Mcha Mungu, bikira, mpole, mkarimu, mzuri n.k.

Nimegundua kwamba huyu mwanamke ana karama ya unabii pia (muonaji). Zamani manabii waliitwa waonaji.

Kwanini nimefikia hii conclusion? Mjomba wangu alikuwa anaumwa, yaani kaka yake mama yangu. Siku Moja kabla ya kifo cha mjomba wangu, mchumba wangu akanipigia simu kunimbia anaona huzuni KUBWA Kwa mama yangu, kesho yake mjomba akafariki, kweli mama aliumia sana!

Mimi ni Wakili, nilikuwa na kesi Tanga Jana, kabla sijaondoka akanipigia simu kuniambia anaona vita KUBWA kwenye hiyo kesi, na ananiona Niko hospitalini! Baada ya kesi, ule upande wa pili wakaniomba tuonane nje ya Mahakama nikiwa na mteja wangu ili tufute kesi tuyazungumze, kweli tukaenda kuonana nao, nikawekewa sumu kwenye kinywaji changu, nikapelekwa hospitalini kweli na nikalazwa, Sasa hivi ndio wameni-discharge.

Hayo ni machache tu kati ya mengi. Ama kweli, ukimtanguliza MUNGU mbele HUWEZI kuikataa taasisi ya NDOA. NDOA ni baraka.

Huyu nikimuoa inabidi niwe makini sana

Muwe na jioni njema.
Sasa uwe makini kwa nini wakati yupo?Wewe kabla ya jambo,ni kumwambia akuangalizie.
 
anaeza pia akawa na pepo la utambuzi cc Mshanajr
nina baba yangu mdogo yeye ni mganga,anaonyeshwaga mikasa akiwa amelala. kama kuna jambo baya linatokea hasa kwa watu anaowafahamu anaonyeshwa
Nafahamu kuhusu roho ya utambuzi.

That is not the case kwa huyu binti. Hii ni karama ya unabii kabisa.

Siwezi kusema kila kitu hapa ila naamini umenielewa.
 
Aisee huyo ni GUARDIAN ANGEL, hutakiwi kumuogopa kabisa maana once mkianza kuishi pamoja kama familia, utawajua mpaka marafiki wanafiki ambao kwasasa wewe unahisi ni watu wako wa karibu sana kumbe sio.

Nasema hivi kwasababu mimi wife wangu ni wa aina hii, baada ya kuanza kuishi nae rasmi nimegundua vitu vingi ambavyo binafsi nisingevijua kabisa.

Na amekuwa msaada sana maana kuna muda unaweza ukajikuta life linakuwa tight sana na mishe zote zinakwama kumbe wanaokwamisha ni washikaji zako wa karibu sana na huwezi hata kuwafikiria.

Hivyo wife wa aina hii ni rahisi sana kukuambia nini kinaendelea na hatua gani ufanye au watu gani unatakiwa uachane nao kabisa.

Maana kama adui yako ni rafiki yako wa karibu na wewe hujui lolote lile. Kutoboa kwenye maisha ni ngumu sana kwasababu unamuamini na unamshirikisha mambo yako mengi sana kumbe mwenzio anaenda kukuharibia bila hata huruma wala sababu ya msingi.

Kuoa mke wa aina hiyo kuna Advantages zake, lakini pia haimaanishi kwamba ukioa mke ambaye sio muonaji maisha hayawezi kwenda, yataenda tu kama wote mtamtegema MUNGU kwa kila jambo.

MAONI YANGU NI HAYO TU.
Asante sana mkuu wa mafunuo haya. Umeniongezea kitu kikubwa sana.

Ubarikiwe!
 
unasema kesi sio vita wakati walitaka kukuua....kesi ni vita ndo maana kila mtu anapambana kivyake ili ashinde
Msiwe vichwa maji.

Nikisema kesi sio vita namaanisha mapambano hayawezi kufikia hatua ya kufanyiana ubaya. That is what I mean. Anayefanya ubaya anakuwa ametafsiri vibaya maana ya kesi ni vita/mapambano.

Sisi huku tunashindana kwa Sheria na Mantiki, sio mtutu wa bunduki.

Na kama ulikuwa hujui, Wanasheria tunahimizwa sana kumaliza kesi nje ya Mahakama, kuendelea na kesi iwe ni last resort. Ndio maana walipotuita hatukusita kwenda kuwaona. Ingawa wao walikuwa na nia ovu.
 
Wakuu habarini za wakati huu...

Niliwahi kuleta Uzi humu kuhusu mchumba wangu ambaye ni Mcha Mungu, bikira, mpole, mkarimu, mzuri n.k.

Nimegundua kwamba huyu mwanamke ana karama ya unabii pia (muonaji). Zamani manabii waliitwa waonaji.

Kwanini nimefikia hii conclusion? Mjomba wangu alikuwa anaumwa, yaani kaka yake mama yangu. Siku Moja kabla ya kifo cha mjomba wangu, mchumba wangu akanipigia simu kunimbia anaona huzuni KUBWA Kwa mama yangu, kesho yake mjomba akafariki, kweli mama aliumia sana!

Mimi ni Wakili, nilikuwa na kesi Tanga Jana, kabla sijaondoka akanipigia simu kuniambia anaona vita KUBWA kwenye hiyo kesi, na ananiona Niko hospitalini! Baada ya kesi, ule upande wa pili wakaniomba tuonane nje ya Mahakama nikiwa na mteja wangu ili tufute kesi tuyazungumze, kweli tukaenda kuonana nao, nikawekewa sumu kwenye kinywaji changu, nikapelekwa hospitalini kweli na nikalazwa, Sasa hivi ndio wameni-discharge.

Hayo ni machache tu kati ya mengi. Ama kweli, ukimtanguliza MUNGU mbele HUWEZI kuikataa taasisi ya NDOA. NDOA ni baraka.

Huyu nikimuoa inabidi niwe makini sana

Muwe na jioni njema.

Umesema ni BIKIRA eeeee?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom