Mchoro huu umenifikirisha sana

Uzito wa mizigo (magari mkubwa) huchangia barabara kuharibika mapema.., miaka hiyo ya zamani farasi, punda, na ngamia ndio walikuwa wabebaji wa mizigo so barabara lazima zidumu kwa muda mrefu.
 
Wanayotwambia siyo sawa na tunayoyaona
 
uzito wa mizigo (magari mkubwa) huchangia barabara kuharibika mapema.., miaka hiyo ya zamani farasi, punda, na ngamia ndio walikuwa wabebaji wa mizigo so barabara lazima zidumu kwa muda mrefu.
Yaani wanajenga hawajui nani anakuja kupita hapo- halafu wanasema wana elimu?
 
Unaongelea barabara zipi?
 
Hiyo picha ya kwanza imechorwa, picha ya pili ni real, still tunacompare kitu real na cha kufikirika, engineering imefika watu wanajenga madaraja kwenye bahari huko, sector ya ujenzi imefika level ya juu sana na hizo barabara utazikuta mostly africa kutokana na corruption, ila kufananisha sector ya ujenzi ya sasa na kipindi cha kale ni kutotumia akili.
 
Barabara ya Mawe, zege (rigid) ni tofauti na barabara ya lami (flexible). Kwa hiyo fananisha barabara ya lami ya zamani vs lami ya sasa au ya Mawe ya zamani vs ya Mawe ya sasa. Daima barabara za mawe au zege hudumu zaidi kuliko za lami.

Ukiuliza kwa nini hatujengi za mawe sasa? Hilo sasa suala sio la engineer maana linahusu bajeti na barabara za mawe, zege ni gharama zaidi kuliko za lami.
 
Sikatai kuwa mbishi nitakuwa mnafki kwa hilo, ila atleast nabisha kwa hoja

Sina ubishi kwamba hakuna mainjinia wasio walaghai wenye kufanya njama na watu waserikali. Ila nitakuwa mtu wa mwisho kukubaliana na wewe kua kwa uwepo wa aina hiyo ya mainjinia ndio kigezo cha kuishusha hadhi moderm technlogy na civil engineering kiujumla

Hapo utakuwa unafanya kitu kinachoitwa "Hasty Generalization" kufanya makosa ya kufananisha hoja kwa mifano michache ku prove point yako

Hiyo ni sawa na kusema, benadi alifeli kiswahili, ashura naye akafeli kiswahili, christian alifeli pia hivyo nahitimisha kua yeyote atayefanya mtihani wa kiswahili atafeli pia

Hiyo haiwezi kuwa sababu ya kujustify kwa watu wote, vipi kama benadi, ashura na christiani walikuwa hawazingatii masomo? Au kipindi mwalimu anafundisha wao walikuwa wanaumwa hawakuweza kuhudhuria?


Hizo barabara za kikoloni ziliweza ku handle circumstances kama hizi

Au hatahivi




Wote tutakubaliana kwamba zilijengwa mahususi kwa ajili ya hivi


Wakoloni walijenga barabara kwa ajili ya kupitisha majeshi na watumwa ambapo wanajeshi walivaa sendos na watumwa walikuwa peku, ulitegemea uone damage gani tena kwa matumizi hayo ya barabara?
 
Engineer Kama engineer 😂
 
mbona mpaka sasa hivi hao punda hawapo yanapita magari na still road iko tough
 
mbona mpaka sasa hivi hao punda hawapo yanapita magari na still road iko tough
Mfano nimekuta lami iliwekwa soko la majani mapana tanga, ile lami nimeanza kuiona miaka ya 80 still bado ipo
 
Ni Barabara ngapi za mkoloni bado ziko hai mpaka Leo hii?
 
Kama punda hawakuharibu barabara za enxi hizo ni kitu gani kituaminishe kwanini tujitetee wa enzi hizi kwakuwa excavator zinaharibu barabara zetu. Wao hawakuenda vyuo kujua punda asiweze kuharibu barabara... sisi tumeenda shule nini kimetufanya tushindwe kujua hii barabara iko siku itapita excavator kwahiyo tutumie digrii zetu kuhakikisha barabara hazitaharibika?

Jibu najua unalo. Zamani hakukuwa na Siasa kazini. Ila hivi sasa Hussein Mwinyi ambaye hakuwahi kuwa kuruta JWTZ anakuwa waziri wa Ulinzi, na baadae Rais wa Zenji.... Ummy Mwalimu ni waziri wa afya lakini hajui ABC za Panadol

Dr. Mwele (RIP) akitoa angalizo mwanasiasa aliesomea korosho zinapataje mimba anamtimua kazi

Pathetic
 
Hizi barabara unazoziona sio za kiwango tukiamua tuzitumie kupitishia punda na wanajeshi waliovaa sendo na wananchi ambao wako peku, basi life span yake itakuwa ndefu zaidi

Ishu sio siasa, ishu ni kwamba tupo kwenye ulimwengu ambao una watu ambao wanapenda vya bei ndogo katika mazingira ambayo ni magumu kwa upatikanaji wa material.

Inawezekana kutengenezewa barabara nzuri yenye ubora utaodumu kwa kipindi kirefu zaidi lakini je bajeti hiyo mnaweza kuimudu?

Halafu unavyoliongelea hili ni kama unalenga africa na Tanzania kiujumla lakini hata huko kwa mabeberu zipo barabara za kirumi na bado barabara za mainjinia wa kisasa bado zina potholes je nao hao utasema wazungu wana siasa za kuweka watu ambao hawa fit kwenye idara husika?

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…