Mchina aliyepata "A" tisa NECTA

Inaweza kuwa huu mtihani pia ulitungwa China.
 
Mie pia nasoma kitu na kukielewa lakini kukielezea kwa kuongea dah! Kiukweli huwa nashindwa, hata huyo mchina simshangai
 
Kama Rushwa inarukakuta na kuingia Ikulu, BOT,TRA,TPA na TAMISEMI sipendi kuamini kuwa NECTA ina Fence ngumu kufikika!
 
Uko sahihi. Kitu ambacho baadhi ya GTs hawakijui ni kwamba lugha yo yote ni taaluma, yaani wanaoizamia wanajifunza sayansi yake - kinachoifanya kuwa njia ya kuwasiliana. Kwa hivyo Kiswahili na Kiinglish au Kiarabu ni taaluma (somo katika shule za msingi na sekondari, na uwanja maalumu katika vyuo vikuu). Si kila mzungumzaji (native speaker) wa Kiswahii au Kiingereza anaweza kushinda mtihani wa Kiswahili au Kiingereza ngazi yo yote ile ya shule bila kujifunza au kusomea sayansi yake (isimu na fasihi). Kama ingekuwa ni rahisi namna hiyo basi vijana wa Kitanzania ambao Kiswahili ni lugha mama, wangekuwa wanapata A katika somo la Kiswahili. Kiswahili ni somo kama masomo mengine - ulijifunza sanyasai yake na ukaimudu hata kama wewe ni mchina, utapata A. Tunampongeza sana huyo binti wa Kichina. Huyu binti anatakiwa awe kielelezo kwa watoto wa Kitanzania kwamba ukifanya masomo yako kwa bidii, the limit is the sky!
 
Alipataje phD wakati yeye anajua saddam alikuwa rais wa kuwait
 
Umewahi kukutana na mtu anaandika essay iliyonyooka ila kuongea english ni broken? Kuna kitu kinaitwa craming unameza 4 exams kuelewa baadae.....
Wapo wengi wanajua Kingereza cha kuandika tu lakini cha kuongea ni shida, hata yule mchina anajua Kiswahili cha maandishi lakini cha kuongea ni shiiiiiiiiiida.
 
Unaweza kujua lugha ukashindwa kutamka maneno bali ukajua kuyaandika.
Hhizo halina Ubishi mkuu, wengi hawajui Kiswahili cha kuongea lakini cha maandishi darasani wanajua hata kwa English ndiyo hivyo hivyo wengi hawajui Kingereza cha kuongea lakini cha maandishi ni wakali sana.
 
Umeishajiuliza shule nzima wanafunzi wanaongea kiswahili inakuaje wengine wanapata F.
 
Mbona wabongo wanafumua A za kingereza, kifaransa na kiarabi hamshangai
Watanzania wengi ni malimbukeni wanaamini kujua English ni ujanja hawathamini lugha ya Taifa matokeo yake mchina kawapa Somo zuri angalau sasa wataanza kujitambua na kuithamini Lugha ya Taifa.
 
Umeishajiuliza shule nzima wanafunzi wanaongea kiswahili inakuaje wengine wanapata F.
Ni kutokana na kutoithamini Lugha yetu na kuamini kuwa English ni bora kuliko Kiswahili
 
Ki
kiswahili cha darasani kile cha mitaala kina utofauti kidogo na Kiswahili cha Mtaani hivyo ni rahisi kwa mwanafunzi kufaulu pasipo kujua kutamka vyema Maneno pindi akiwa anaongea, wengi hawajuia Kiswahili cha kuongea lakini cha kuandika ni hodari wakubwa.
 
Kuongea sio sawa na kuandika,japo unayoyaandika ndio unayoyatamka
 
Usedcountrynewpipo umesema Wachina wanatengeneza iphone sawa kabisa na zinazotengenezwa na Wamarekani Aaaah hii siyo kweli,ukweli ni kuwa Wachina wamekuwa wakitengeneza vitu vingi kwa kuiga hasa kutoka North Amerika,Europe na Japan Iphone wanazotengeneza zinafanana sana na iphone zinazotengezwa na Wamarekani,ila ubora wake na ufanisi wake ni wachini ukilinganisha na original iphone na hii ni kwa sababu wameshindwa kujua siri ya software ya iphone Ukitaka kulijua hili jaribu kulinganisha iphone zote mbili...utaona tofauti kubwa sana Iphone za Wachina zinapatikana sana ktk nchi zinazoendelea kama Tz kwani nchi hizi hazina uwezo mkubwa wa kudhibiti bidhaa zinazoingia nchini mwao Mfano mwingine hai ni wa bidhaa za kichina zilizoingizwa Tz,kama vile pikipiki na mabasi,ufanisi wa vitu hivi sio mzuri ukilinganisha na pikipiki zilizotengenezwa Japan,ila tunavipenda vitu hivi na kujaa kwenye masoko yetu kwa sababu vinauzwa kwa bei nafuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…