Mchikichini: Mtaa wa mateja uliotoa vipanga wengi kielimu Dar na mikoani

Requal

JF-Expert Member
Jun 5, 2020
1,025
1,905
Achana na elimu ya sasa inayoruhusu mwanafunzi mwenye CCF kwenye combination kupangiwa shule na serikali, na DDD kupangiwa chuo cha kati kwa ufadhili wa serikali yenye madaraja ambayo hayaeleweki mara GPA n.k

Naizungumzia Elimu ile angalau ya 2012 kushuka chini, kipindi ambacho matokeo yakitoka nchi nzima inazizima na internet cafe zote zinajaa. Kipindi kile kuwa top ten kitaifa habari ilikuwa gumzo tofauti na sasa, kipindi ambacho mtu akipata Div. 1 ya point 17 anahuzunika, Kipindi ambacho "A" ilianzia 81, Ambacho Ukifaulu kijiji kizima kinajua, Kipindi ambacho ukifaulu vizuri NECTA wanakuwekea nyota kwenye matokeo yako.

Mchikichini na Mapambano ni kati ya sehemu za tuition hapa jijini ambazo zilitoa vichwa wengi sana kwa shule za hapa mjini na mikoani, binafsi ilikuwa ni bora nikose pindi la darasani kuliko la Mchikichini, pindi zake zilikuwa na madini adimu sana kuliko vipindi vya shule kwa tuliosoma shule za serikali na hata huko private kama feza walimu walitumia notice za hawa miamba kufundishia, notice zao zilisambaa karibia kwa shule nyingi na mikoa yote hapa nchini.

Kwa O'level na Advance, nani hamjui moody (Physics), Hidden (Mathematics), na Mbuga (Chemistry na Bios) Kwa advance nani hamjui Mtiga (Advance Physics) - Mapambano na Mwalamy (A. Mathematics) - mchikichini na Ubungo, kwa masomo mengine sikuwa na interest nayo na sikujua hata waliyokuwa wanayafundisha, mchikichini ilikuwa ni zaidi ya shule isiyokuwa na usajili rasmi iliyozungukwa na mateja kila kona ya mtaa.

Notice za hawa miamba zilikuwa ni zaidi ya Abolt au chand, zilifanya physics, maths na chemistry zionekana kama chai ya mlenda kwa O'level na Advance, nakumbuka tukiwa O'level watu tulikuwawa hatushindani tena kupata "A", 81 kwa kipindi hicho bali tukawa tunashindana kutengeneza making scheme kwenye vyumba vya mitihani. Kiukweli waliifanya elimu kuwa kitu chepesi sana japo pia ufaulu ulikua mgumu sana nyakati zile

Hii sehemu ni chafu kwelikweli hasa kipindi cha mvua, lakini ni sehemu pekee iliyokuwa inakutanisha vichwa kutoka shule mbalimbali karibia kona zote za jiji la Dar es Salaam na mikoani kama Feza, Marian, Baobaob, Mzumbe, Kibaha, Tabora Boys, Minaki, Pugu, Ilboru, na zinginezo

Mnakumbuka ile mitihani ya kujipima pale shule ya msingi mchikichikini na kule mapambano, jangwani sekondari na kwa manyirizu kila weekend? Watoto wa feza na St. Marian tulikuwa tunawaburuza sana kule, lakini ndio hivyo NECTA wanaingia top ten

Enzi hizo mtu anapata alama 83 anachana chana karatasi kwa hasira, anaona hakustahili.

Uishi miaka mingi Mapambano na mchikichini mtaa wa mateja, Iko siku mitaa hii itapata hadhi inayostahili.
 
Zamani matokeo ya darasa la saba na Form four yalikua ni kama matukio ya kitaifa. Yali create attention sana. Ila introduction ya BRN ndio ikaanza kupunguza ari ya vijana kujituma.maana kufauru kulikuja kuwa ni kitu rahisi.

The real and serious education iliishia 2010.
 
Huyu mtu wa kuitwq Mr. Mtiga Mungu amuweke sana! huyu jamaa ni fundi.
Juzi nmekutana na Madesa ya Chalange wa EKU, jamaa amecopy na kupaste ngoma za Mr. Mtiga.
Huwezi kusoma mtiga na moody halafu physics ikusumbue hasa ile O'level unaona ni utoporo kabisa, jamaa walicover kila sehemu

ulikuwa unasolve past paper unaona watunzi wote hawana akili
 
Zamani matokeo ya darasa la saba na Form four yalikua ni kama matukio ya kitaifa. Yali create attention sana. Ila introduction ya BRN ndio ikaanza kupunguza ari ya vijana kujituma.maana kufauru kulikuja kuwa ni kitu rahisi.
The real and serious education iliishia 2010.
Kabisa chief, kwa sasa hiki tunachozalisha sio elimu tena.
 
Hidden alinipa A ya hesabu.
Kipindi hicho tulikuwa hatushindani kutafuta "A" YA HESABU hasa kwenye mitihani ya shule, mock na NECTA maana lilikuwa jambo rahisi sana, tulikuwa tunashindana kutengeneza making scheme kwenye chumba cha mtihani.

Ishu ilikuwa inakuja kwenye ile mitihani ya mitaani, ilikuwa inasukwa balaaa
 
Moody Physics, Mtata De Mtatuz Adv Maths. Jumane & Jumamosi tunapiga zoezi la Pure kwa Manyilizu Jangwani.

Shule zilikuwa ni examination center tu. 😁 😁 😁 😁
Na watu tulikuwa tunatoboa kwelikweli...siku hizi haina mzuka kabisa
 
Afu hata mimi nilikuwa nawasikia sana hao jamaa wa Mchikichini,ila nilikuwa sipendagi masuala ya tuition kabisa.Kwanza huyo wa kukupeleka na kulipia uweze kusoma hiyo twiiti ni nani?

So inakulazimu tu kuignore habari za tuition na kuacha natural selection of its own.
 
Back
Top Bottom