Tujikumbushe tuliokimbia ugumu wa Dar es Salaam na kuja kupata nafuu mikoani

Eli Cohen

JF-Expert Member
Jun 19, 2023
1,309
4,017
Mr Blu mtoto wa mjini daslam aliwahi kusema "Bongo nyoso, Bongo balaa" huku Becka akiimalizia balaa kwa kusema "aaa aaah" kwa kumaanisha bongo ni balaa sana.

Kipindi hicho unaiona Dar es Salaam kama sehemu muhimu kwa ajili ya maendeleo yako lakini daslam yenyewe inakuona kama boya lingine la kulikaanga na hili joto kali.

Unapambana kugombania dala dala za gomz, unamwambia mchoma chips aku balansie za buku, bahasha ya vyeti hadi imekakamaa kutokana na kuishikilia sana unapotembea kutafuta hata ku-volunteer, mpenzi ulienae anakuomba hela ya pedi wakati hata wewe umeshindwa kuongeza boxer nyingine, baba ukimwomba pesa anakuambia wewe upo dar huko pesa hauwezi kosa, hapo hapo vishoka wameshakula pesa zako kwa kudanganya watakutafutia mishe, huku geto majirani wanakusema eti unajifanya msomi sana hauwachangamkii bila ya kujua una pitia depression ya hatari.

Hakika dsm ni connection, dsm ni kujipanga. Wanaenjoy dsm ni wale walio kuja wakiwa katika "control mode".

Simaanishi dsm sio sehemu sahihi, ila sio sahihi kwa kila mtu, haikuwa sahihi kwangu, nilisepa mapema, nikarudi mikoani na namshukuru Mungu nilijitafuta huku na nikajipata, Maisha yanaendelea.

TUSICHOKE KUPAMBANA, ILA TUSIONE HAYA KUBADIRISHA MAZINGIRA.

Screenshot_20230825_103236_Firefox.jpg
 
Semeni yote lkn hapa mjini sitoki kitakachonipeleka nyumbani ni vitu kama;
Kwenda kusalimia wazazi
Kwenda kuwania Jimbo japo kimakazi takua daslam
Mwili wangu kurudishwa home mwenyezi atakapoamua ugomvi wangu na kutuliza bahari
 
Mikoani shamba unapata mpaka kwa milioni, shule za kusomesha watoto za serikali zipo, wanawake wenye maadili wapo sema ndo hivyo hutaona magorofa na starehe za mijini sahau.
Hakika
 
Yani nikimbie kijijini kwetu daslam niende wapi?. Mzaramo nawaza kujitosa unyamwezini huko mambele mana daresalaam pamoja na kuwa jiji kubwa mm ndo kijijini kwangu. Naendra wapiiiiiiir?
Hapo ni kwenu pambana
 
Dar es salaam ni Jiji gumu sana kwa mtu asiye na gari lenye AC, nyumba kando ya bahari, biashara/kazi ya maana, nk.

Binafsi bora niishi Jiji lolote lile,! Ila siyo Dar na Arusha.
Kuna sisi wengine ambao hatuwezi kuishi popote isipokua dar na arusha😃😃 kama haupo kwenye hiyo miji unapitwa sana kumbuka "success is hidden in what you fear" ukiona sehemu hakuna ugumu na hela pia ni changamoto ila kukaa dar au arusha inabidi ukaze kwelikweli
 
Back
Top Bottom