Mchezo wa Ng'ombe huko Pemba

Mpasuajipu

JF-Expert Member
Oct 22, 2010
836
49


Mchezo wa ng'ombe Pemba kisiwani

Pemba ndipo mahali pa pekee katika Afrika penye desturi hii ya mchezo wa ng'ombe. Hii ni kutokana na athira ya Ureno kwenye mwambao wa Afrika ya Mashariki miaka 400 iliyopita. Mara Wareno walikuwa na kituo huko Chake Chake, mara walikuwa na mapatano ya usaidizi na Pemba, mara waliuachia utawala Sultani wa Mombasa. Haijulikani jinsi walivyoacha desturi hii Pemba.

Kuhusu mchezo huu amesema Abdullah Amur Suleiman:
“Mchezo wa ng’ombe ni mchezo wa taifa huko Pemba, hapana mtoto wa kiume hata mmoja wa Kipemba, akiwa mwenye asili ya Kiafrika au Kiarabu ambaye hajuwi kumcheza Ng’ombe. Mchezo huu jinsi unavyopendwa na vijana wa kiume wa Pemba ni kama vile wavulana wanavyoupenda mchezo wa mpira yaani ‘football’, huko Zanzibar, Tanzania bara na kwingineko ulimwenguni.
Aghlabu mchezo wa ng’ombe huchezwa wakati wa watu ambao wamerejea mavunoni na karafuu zimekwisha tena na hapo hutazamiya kustarehe. Watu wengi hujumuika kwenye sherehe hizo za mchezo wa ng’ombe na hawaji tu kuona mchezo huo lakini hulipa ada maalum kwa ajili ya kuuona namna mchezo huo ufanywavyo na mastadi wake hodari.

Je mchezo huu bado upo au umetoweka?
 
heh mi ndo kwanza nasikia huu mchezo !!!!!!!!tujuzeni km bado upo tukautizame!!!!!!!!!!!
 
Bull fight ipo sana, nchi za Ureno na Spain (Basiq na Catalani), niliwahi ishi mwaka fulani kaskazini mwa Spain, kuna viwanja kabisa vya maonyesho na mara nyingi huwa yanaanza miezi ya August. kwa kweli ni mchezo hatari sana na wa kusisimua. Nakubaliana na mwenye thread hii inawezekana ni Wareno walileta huu mchezo huko kwa wenzetu wapemba. Kama mtu anajua huwa unaanza kuchezwa miezi gani, naomba msaada nataka nikaushuhudie
 
Inabidi uje na hapa Bongo huo mchez wa ng'ombe labda unawez kutufaa maana football wanatuzingua tu.
 
heh mi ndo kwanza nasikia huu mchezo !!!!!!!!tujuzeni km bado upo tukautizame!!!!!!!!!!!

Huu ni mchezo maarufu sana huko Catalan, na nguli wa mchezo huu huitwa Matador, neno ambalo kipindi hiki limetumiwa kuelezea wacheza mpira wazuri huko Hispania. Kuhusu Pemba hata mimi ndo nasikia leo... Nitajaribu kufuatilia nifahamu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom