Gazeti la Jamhuri: Waziri Mkuu atapeliwa

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,034
Waziri Mkuu wa Tanzania na Meya wa Jiji la Dar es Salaam Omary Kumbilamoto wanatajwa wanatajwa kuwa miongoni mwa viongozi waliojikuta wakitapeliwa bila kufahamu; JAMHURI linarpoti.

Utapeli huo ulifanyika wakati wa maandalizi ya Sikukuu ya Eid al-Adha inavosherehekewa na Waislamu kote duniani kwa kuchinja wanyama na kutoa au kugawa nyama kama sadaka.

Akizungumzia suala la utapeli kwa wazir mkuu, ofisa mmoja wa Rehema Foundation, taasisi inayomilikiwa na raia wa Uturuki (jina linahifadhiwa), amesema taasisi hiyo iliahidi kupeleka ng'ombe 300 Ruangwa, jimboni kwa waziri mkuu kama sadaka ya siku hiyo muhimu kwa Waislamu.

"Lakini cha ajabu, hakuna hata ng'ombe mmoja aliyefikishwa Ruangwa na kuchinjwa kwa ajili ya sadaka. Suala hili ni la ajabu na aibu sana kwa sababu mamia ya watu walishinda kutwa nzima wakisubiri sadaka hivo lakini hawakuipata, anasema ofisa huyo.

Rehema Foundation ni taasisi isiyokuwa ya kiserikali inayomilikiwa au kuongozwa na raia wa Uturuki, ikijishughulisha na utoaji wa misaada ya kimaendeleo kwa jamii chini ya ubalozi wa taifa hilo la Ulaya.

Nini hasa kilichotokea?

Taarifa kutoka ndani ya Rehema Foundation zinadai kwamba maofisa waliopewa jukumu la kupeleka sadaka ya kuchinja jimboni Ruangwa walichukua Sh milioni 147 wakielekezwa kwenda kununua ng'ombe 300 wa sadaka mkoani Mtwara, kisha wawapeleke Ruangwa kuwachinja na kugawa nyama kwenye misikiti ya kata zote.

"Sasa badala ya kufanya hivyo, mtu mmoja (jina tunalo) akatoroka na fedha hizo. Matokeo vake kuna watu hawakula nyama Sikukuu ya Eid al-Adha," anasema mtoa taarifa wetu.

Anasema wananchi wa Ruangwa walikuwa wameshapewa taarifa ya kuwapo kwa sadaka ya nyama, matokeo vake wakashinda misikitini wakisubiri kitoweo bila mafanikio.

Akithibitisha kutokea kwa utapeli huo Sheikh wa Wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi, Mussa Lyambamba, anasema: "Rehema Foundation walituletea taarifa hiyo na sisi tukaisambaza kwenye misikiti ya Ruangwa. "Tukawaambia waumini wetu kwamba siku ya Sikukuu ya Eid al-Adha, Waturuki watatuletea nyama. Miskiti ya wilaya nzima iliiandaa kupokea sadaka hiyo, lakini katika hali ambayo hata mimi sijaielewa, haikuletwa!"

Sheikh Lyambamba anasema hadi sasa waumini bado wanamuuliza kutaka kujua nini kilikwamisha kutolewa kwa sadaka hiyo huku wakilalamikia usumbufu walioupata pasipo kuelezwa sababu. Wilaya ya Ruangwa ina kata 22 na Sheikh wa Wilaya anaitaja Nkowe kuwa ndivo kata pekee iliyofanya sherehe za mwaka huu kwa kuchinja ng'ombe watatu tu.

"Mwaka jana haikuwa hivi, kwani taasisi va Rehema iliahidi kutoa kitoweo na wakatekeleza. Walileta nyama ya kutosha na hakukuwapo malalamiko yoyote. Mwaka huu kilichotokea, mimi sifahamu hata Ofisi ya Bakwata Wilaya hawajui," anasema

Atokomea na Sh milioni 147

Kwa upande mwingine JAMHURI limeelezwa kwamba kilichotokea Ruangwa kilisababishwa na mtandao wa kitapeli na wizi ndani ya Rehema Foundation.

"Ofisa mmoja alitoroka na fedha, Sh milioni 147, zilizotengwa kwa ajli ya sadaka. Baada va sikukuu alikamatwa na kufikishwa Kituo cha Polisi cha Urafiki kilichopo Ubungo, Dares Salaam," taarifa kutoka Rehema oaundation zinaeleza.

Mtoa taarifa wetu anadai kwamba alipofikishwa Kituo cha Polisi, mtuhumiwa huyo alikiri kuingia mitini na fedha zilizotengwa kwa ajli ya jimbo la waziri mkuu na kuahidi kuwa angezirejesha Julai 7 (Ijumaa iliyopita) mwaka huu.

Hata hivvo, kabla hajarejesha fedha hizo, Ubalozi wa Uturuki nchini uliwatuma wanasheria wake kuingilia kati shauri hilo na kulihamishia Kituo cha Polisi Oysterbay, Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni.

Siku aliyopaswa kurejesha fedha, mtuhumiwa huyo na viongozi wa Rehema Foundation walifanya kikao ofisini kwa RCO Kinondoni, makubaliano yakafanyika na shauri likaondolewa polisi, kisha mtuhumiwa akaahidi kurejesha fedha hizo leo (Jumanne, Julai 11, 2023).

JAMHURI limezungumza na uongozi wa Rehema Foundation kutaka kujua ni hatua gani watachukua dhidi ya aibu waliyosababishiwa Ruangwa.

Mwakilishi wa Rehema Foundation aliyepewa jukumu la kununua ng'ombe wa sadaka, Mohamed Assah, hakuwa tayari kuzungumza na mwandishi wetu akielekeza maswali na ufafanuzi upelekwe kwa ofisa wa juu yake aliyemtaja kwa jina la Hamza Msuya.

Msuya amekiri kufahamu kuwapo kwa suala hilo, lakini akadai kuwa yeye hawezi kulitolea ufafanuzi bila kibali kutoka kwa viongozi wa juu zaidi.

"Mkurugenzi wetu kwa sasa yuko Uturuki. Mimi ndani ya taasisi hii siwezi kuamua kitu au kutoa taarifa unazohitaji mpaka nipewe ruhusa na vongozi," anasema Msuya.

Mtoa taarifa wetu ambaye naye ni mfanyakazi wa taasisi hivo anaonyesha shaka akisema: "Huu ni mchezo wa ndani ya taasisi na ubalozi unafahamu, kwa hiyo usitarajie kwamba mtuhumiwa alivesababisha usumbufu kwa wapiga kura wa wazir mkuu atachukuliwa hatua yoyote."

Dar es Salaam nao watapeliwa

Mbali na utapeli unaodaiwa kufanywa na Rehema Foundation, JAMHURI limeelezwa kuwa taasisi nyigine inayoendeshwa na raia wa Uturuki; Eastern Coral Education Development, nayo ilifanya tukio la aina hivo hivo siku ya Sikukuu ya Eid al-Adha, lakini si Ruangwa, bali Bungoni jijini Dares Salaam.

Ni utapeli wa taasisi hii ndio unaomgusa Meya wa Jiji, Kumbilamoto, na taarifa zinadai kwamba yeye, masheikh na maimamu wa misikiti kadhaa ya Bungoni walishinda kwenye machinjio ya Vingunguti wakisubiri nyama ya sadaka lakini hawakuipata.

Taarifa ya kuwapo kwa sadaka hiyo ilitolewa na Sheikh wa Kati wa Bungoni kwa wakazi wa eneo hilo, ikisema kwamba siku ya sikukuu ya kuchinia Waturuki wangetoa ng'ombe wa sadaka kwa ajili yao. Kwamba, katika machinjio ya Vingunguti kungechinjwa ng'ombe 600 siku hiyo; hatua iliyowafanya wakazi wa Bungoni na maeneo jirani wakiongozwa na Kumbilamoto kuelekea huko tavari kupokea sadaka.

Watu wengine waliokwenda Vingunguti ni madiwani wa kata, lakini tukio hilo liliota mbawa na kuwaacha wakishangaa.

"Hadi jioni ya siku va sikukuu hakukuwa na taarifa ilivotolewa na Eastern Coral kuhusu kuahirishwa au kushindikana kutimizwa kwa ahadi yao," anasema mtoa taarifa wetu

Akizungumza na JAMHURI kuhusu suala hilo, Meya Kumbilmoto amesema tukio la Vingunguti halimhusu moja kwa moja kwa kuwa yeye aliombwa na rafiki yake, Sheikh wa Kati wa Msikiti wa Bungoni kumsindikiza kupokea nyama.

"Kwa hivo hata taasisi ilivoahidi kugawa nyama ya sadaka sijui," anasema Meya.

Sheikh wa Kati wa Bungoni, Abdul Abdul, maarufu Mussa Bad, anakiri kutokea kwa suala hilo akisema yeye alipewa kazi ya kuwataarifu wakazi wa Bungoni na misikiti jirani kwamba taassi ya Eastern Coral Education Development italeta kitoweo.

"Kilichotokea hadi taasisi hiyo ikashindwa kutimiza ahadi yake sikijui. Kazi yangu ilikuwa kuwataarifu tu watu na nilifanya kwa kuandika barua kwenda misikiti jirani.' anasema Sheikh Mussa Bad.

Sheikh huyo anasema hana uhusiano au mawasiliano ya moja kwa moja na taasisi husika zaidi ya kupewa kipeperushi chenye anwani yao bila namba yoyote ya simu.

Mchezo mchafu

JAMHURI limeelezwa kuwa siku hivo katika machinjio ya Vingunguti walikuwapo watu kadhaa wanaodhaniwa kutumwa na taasisi ya Eastern Coral, waliokuwa wakipiga picha makundi ya ng'ombe wa wafanyabiashara waliopelekwa kuchinjwa.

"Kwa kuwa hawa watu mchezo wao huwa ni kukusanya watu, kuorodhesha majina yao na kisha kuwapiga picha wanazopeleka kwa wahisani kuhalalisha matumizi ya fedha walizotoa, bila shaka hata hao waliokuwa wanapiga picha makundi ya ng'ombe Vingunguti ni walewale,” anasema.

Mbali na sakata la Ruangwa na Vingunguti, zipo taarifa kwamba taasisi nyingine ya raia wa Uturuki, Daynat, nayo ilijipa jukumu la kusambaza nyama Zanzibar, Morogoro na Mbeya,

"Zanzibar na Mbeya kuna uhitaji mkubwa wa ng’ombe lakini badala yake Daynat walipeleka Ng’ombe Morogoro pekee

"Zanzibar hawakupeleka hata ng'ombe mmoja wakati Mbeya walipeleka ng ombe 15 kwa ajili ya sadaka ya kitoweo kwa kata 36 za Jii la Mbeya,' anasema mtoa taarifa

wetu.

Üchunguzi wa JAMHURI umebaini kuwa baadhi ya taasisi za raia wa Uturuki zimekuwa zikichota fedha kutoka katika mfuko wa shirika la misaada la nchi yao kwa lengo la kuwasaidia Watanzania, lakini aghalabu huishia mifukoni mwao.

JAMHURI lilimpata Ofisa wa Kitengo cha Mawasiliano kwa Umma wa Ubalozi wa Uturuki nchini, Hashim Abdallah, kutaka kujua nini ambacho ubalozi unakifahamu kuhusu tuhuma za utapeli zinazoelekezwa kwa raia wa Uturuki na taasisi wanazoziongoza.

Hata hivyo Abdallah hakutaka kutoa ushirikiano pamoja na kuelezwa masuala yote yaliyotokea.


Jamhuri.jpeg

IMG_5674.jpg
 
Balile ni mtu wa hovyo sana.

Eti waziri mkuu atapeliwa mil 147 za Eid.. to hell with that.

Kuhusu Bandari;
Kinachogombaniwa na nani? Serikali ipo kinachoshindikana ni kitu gani.

Hoja hapa ni maslah ya Tz kwenye mkataba na sio ufanisi wa bandari.

Tunachoka kuelekeza vichwa safari.
 
Balile ni mtu wa hovyo sana.

Eti waziri mkuu atapeliwa mil 147 za Eid.. to hell with that.

Kuhusu Bandari;
Kinachogombaniwa na nani? Serikali ipo kinachoshindikana ni kitu gani.

Hoja hapa ni maslah ya Tz kwenye mkataba na sio ufanisi wa bandari.

Tunachoka kuelekeza vichwa safari.
Nikimuangaliaga na ule mtumbo wake nasikiaga kichefu chefu... kuna siku nilipanda nae ndege nilitamani kumtia makonzi
 
Back
Top Bottom