Mchezo unaotaka kufanyika NSSF huu hapa

Mchezo unaotaka kufanyika NSSF huu hapa

Hapa ndo huwa nashindwa kuwaelewa hawa madogo wasaka kaazi wa siku hizi wasiojiamini.... Mkiishi kwa kuamini kila kitu kwamba atapata mtoto wa kigogo NI UJINGA MTUPU. Na sijui shule inawasaidia nini...

Ngoja nikuulize maswali mawili tu, halafu jijibu.

1. Naamini kwenye interview walikuwepo vijana wengi, na naamini sio wote ulisoma nao au unawajua, sasa umejuaje kwamba watoto wa vigogo waliangukia pua na nyinyi watoto wa magogo au miti kamili mlifaulu??

2. Umejuaje kwamba fulani ni mtoto wa hicho kigogo na mwingine ni mtoto wa mti?? Uliwauliza wote??

Acheni habari zenu za kulalama majukwaaani.... Jiamini katika usaili.. Hata mimi baba na mama yangu ni wafanyakazi wa kada ya mwisho serikalini hawana hela na hawamjui yeyote, lakini nimefanya interview na kufaulu zaidi ya sehemu tatu sensitive hapa nchini (makampuni yanayolipa zaidi hapa nchini) bila kuhonga hata shilingi.. Na interview moja unakuta wameomba watu hadi elfu moja.. Lakini tunafanya saili za kutosha na tunashinda..

Yaani ulichoandika hapa ni sawa na vile ulivyokimbia panya road na kujificha uvunguni mwa bajaji... Vijana wa kiume wa Dar bana..

Kweli kabisa inabid tujiamin,tuondoe haya mashaka mashaka,watu wanapga pepa wanasonga mbele,tukiwa hatujiamin hata hyo interview hatuwez fika mbali
 
Mi hata kama wakiniita mara mia moja nakuja hivyo hivyo tu hadi kieleweke
 
Mi nina shaka labda mtihani wa mwanzo watu walifeli sana wameamua kurudia
 
Acha kupotosha umma hao watoto wa vigogo (kama wapo) wakitakiwa wataitwa tu wanaweza hata wasifanye hiyo interview yenyewe

siamini watoto wa vigogo watasoma ifm huko tunapeleka watoto wetu sie kajamba nani wao vigogo watoto wao wako reading na houston sasa hivi

c.t.u
 
Kiufupi kila mtu alieudhuria interview ya kwanza ameitwa kwenye usahili wa pili swali la kujiuliza hata kama hii ni system yao ya kufanya written mbili ila inavyokua idadi inatakiwa ipungue katika ya pili lakini cha ajabu idadi ni ile ile ina maana mara ya kwanza ilikua kazi bure kufanya pepa na wanaotoka mikoani je si ni gharama hizi zisizo na maana

wanafanya watu mazuzu kweli...yani hawajachuja?
 
Mtoto wa mkulima mwenyewe. Acha mambo ya kizamani wewe ,
 
Ebu acheni kutetea hao wapumbavu nssf! Hio sio akili kuita watu wote kwenye interview mara 2!hizi ni inshu za kubebana!siku moja itaeleweka kama uhamiaji ilivyotokea!
 
Kwa hiyo unataka kutuaminisha kuwa hao waliofeli nao wameitwa tena? Tuwekee evidence, maneno matupu tutayaamini vipi?
 
Humu kuna watu wanavijikaz vyao mchwara kwa hyo wanataka kuzingua wenzao tu we cha msingi hudhuria hata zikiwa 4 nenda zote

Hivyo hivyo Mkuu,wanataka kutukatisha tamaa wakati wengine hatukati tamaa kirahisi,Aluta Continua Mkuu,Mbele Daima, Nyuma Mwiko,Tukutane DUCEEEEEEEEEEEEEE,#Team DUCE#Mukuje hapaaaaa
 
Ni Kweli hapana kuchoka mtu hapa, hadi kieleweke kwa kweli, hata waite mara ishirini
 
Hakuna mtu anayeweza kutoa sababu kwanini wameita tena cha msingi kwa wale wasikata tamaa kama mimi tukutane DUCE
 
Assumptions
1. Au inatafutwa average kutoka kwa hii ya pili
2. Au kipepa cha kushade kilizingua kusahihishwa
3. Au applicants wamefaulu wengi kwa kufungana kupita malengo ya oral
4. Au malalamiko ya watu, maswali 100 n.k

Cha msingi ni kuhudhuria tu, we are job seekers so we have to seek indeed
 
Hakuna mtu anayeweza kutoa sababu kwanini wameita tena cha msingi kwa wale wasikata tamaa kama mimi tukutane DUCE

I will be there mkuu kesho saa kumi na mbili tu mapema mm mtoto wa mkulima face to face na watoto wa vigogo hapa mjini
 
Back
Top Bottom