SI KWELI Mchezaji wa Simba Babacar Sarr ana historia ya ubakaji, udanganyifu na kukimbia mamlaka

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Here it is, kwanza
1. Kadanganya Miaka yake kwa wikipedia today changed his age 32 To 26
2. Anatafutwa as an international fugitive.
3. Out of all players, wameenda kwa mtu ana history ya ubakaji. Why?

tano-1024x683.jpg
 
Tunachokijua
Januari 6, 2023, Klabu ya Simba ilimtambulisha mchezaji wake mpya kutoka Senegal anayeitwa Babacar Sarr. Sehemu ya taarifa rasmi iliyochapishwa na klabu hiyo kwenye tovuti yake inasema;

"Tumemsajili kiungo mkabaji, Babacar Sarr raia wa Senegal mwenye umri wa miaka 26 kutoka US Monastir kwa mkataba wa miaka miwili.

Sarr ni kiungo mwenye uzoefu wa kucheza soka la Afrika ambapo mbali na Monastir amewahi kuzichezea Olympique Beja ya Tunisia, Teungueth FC, AS Pikine na Mbour P.C.

Sarr ana uwezo mkubwa wa kucheza kama kiungo mkabaji na wakati mwingine anaweza kucheza kama kiungo mshambuliaji kwahiyo ni jambo ambalo limetuvutia.

Sarr anakuja kuungana na viungo wakati kama Fabrice Ngoma, Sadio Kanoute, Mzamiru Yassin na Abdallah Khamis"


Baaada ya kutolewa kwa taarifa hii, madai ya mchezaji huyu kuhusishwa na ubakaji, kudanganya umri pamoja na kuwa anatafutwa na polisi yalianza kusambaa.

Mathalani, mtumiaji wa Mtandao wa JamiiForums.com anayefahamika kwa jina la Danielmwasi alianzisha mjadala huu akiainisha tuhuma tatu zinazomkabili Sarr. Aidha, utafutaji wa JamiiCheck umebaini pia baadhi ya watumiaji wa Mtandao wa X waliungumzia tuhuma za Sarr.

Mtumiaji mmoja wa Mtandao huo anayetumia jina la MKUDA alimnasibisha Babacar Sarr na tuhuma za ubakaji.

Ukweli wa madai haya upoje?
JamiiCheck imefuatilia tuhuma hizi na kubaini kuwa hazina ukweli.

Aidha, utafutaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck umebaini kuwa Danielmwasi alitumia Wikipedia kama chanzo mama cha taarifa yake kama inavyothibitishwa hapa.

Kwa mujibu wa Wikipedia, Babacar Sarr anayezungumziwa hapa amezaliwa mwaka 1991 na alifanya ubakaji huo nchini Norway.

Pia, miongoni mwa timu alizowahi kuchezea ni Selfoss, CA Bastia, Start, Molde na Damac.

Tovuti hii inabainisha zaidi kuwa hati ya kimataifa ya kukamatwa kwake inafanya kazi hadi mwaka 2025 hivyo Askari wa Kimataifa (Interpol) bado wanamtafuta.

Utofauti wa Taarifa za Sarr
Babacar Sarr aliyesajiliwa na Simba amezaliwa mwaka 1997, hivyo kwa sasa ana umri wa miaka 26 na sio miaka 32 kama madai yanayosema. Aidha, timu ya mwisho aliyochezea kabla ya kujiunga na Simba ni US Monastir na sio Damac FC ya Saudia kama iliyoandikwa na Wikipedia.

Mwaka 2020, BBC ilichapisha makala yanayofafanua tuhuma za Sarr pamoja na kuambatanisha picha yake. Sura ya mtu anayeonekana kwenye picha hiyo haifanani na sura halisi ya Sarr aliyesajiliwa na Simba.
_110983639_babacar-sarr-composite.png.webp

Babacar Sarr (Picha na BBC)

tano-1024x683-jpg.2866056

Babacar Sarr (Mchezaji wa Simba SC)
Umri wa Wikipedia haujabadilishwa
Madai mengine ya Danielmwasi ni kuwa baada tu ya kusajiliwa na Simba, taarifa zinazohusisha umri wa Sarr zilihaririwa kwenye tovuti ya wikipedia kutoka miaka 32 hadi 26.

JamiiCheck imefuatilia madai haya na kubaini pia hayana ukweli. Kwa mujibu wa taarifa zilizopo kwenye tovuti hiyo hadi kufikia Januari 9, 2023, siku 3 baada ya kuwepo kwa madai haya zinaonesha kuwa Babacar Sarr ana umri wa miaka 32 ileile, yaani amezaliwa Februari 15, 1991. Unaweza kufanya rejea hapa.

Kwa mujibu wa tovuti ya Transfer Markt, Babacar Sarr ana urefu wa Mita 1.83 na thamani yake kwenye soko ni Tsh. Bilioni 1.37 (Zaidi ya Euro 500,000)
Here it is , kwanza

1. kadanganya Miaka yake kwa Wikipedia today amechange his age 32 To 26

2 . Ni anatafutwa as international fugitive .
3 . Out of all players wameenda kwa mtu Ana history ya ubakaji . Why ?

4.
Kwahiyo Tanzania amekuja kujificha kwa tuhuma alizonazo na kwa ulimbukeni wamakolo wameempa mkataba na mshara mnono fugitive
 
Hii nchi wenye akili tumo wachache sana. Mtu ana google vitu vyovyote anatuletea hapa. Ushaambiwa Babacar Sarr mbakaji ni ex player bado hujui maana yake. Kina Babacar Sarr ni wengi sana West Africa na specifally Senegal. Wengine wana miaka zaidi ya 60. SI lazima kupost kama hujui unachopost
 
Wikipedia ina freely editable information. Usichojua ni kuwa hata wewe unaweza kwenda ku edit info za profile ya mtu wikipedia.

Pia mchezaji hawezi kusajiliwa bila kuwa cleared na bila kuwa na work permit kutoka wizara ya mambo ya ndani.

Je kama angekuwa wanted unafikiri wizara imelemaa kiasi hicho?
 
Hii nchi wenye akili tumo wachache sana. Mtu ana google vitu vyovyote anatuletea hapa. Ushaambiwa Babacar Sarr mbakaji ni ex player bado hujui maana yake. Kina Babacar Sarr ni wengi sana West Africa na specifally Senegal. Wengine wana miaka zaidi ya 60. SI lazima kupost kama hujui unachopost
Halina akili hili mkuu achana nalo
 
Here it is , kwanza

1. kadanganya Miaka yake kwa Wikipedia today amechange his age 32 To 26

2 . Ni anatafutwa as international fugitive .
3 . Out of all players wameenda kwa mtu Ana history ya ubakaji . Why ?

4.
Akuna timu ya waarabu wanaoweza kumuacha mchezaji ambaye ni mzuri labda awe na shida, na ndicho kilichopo kwa uyo mchezaji aliachwa na U.s monasteries mwezi wa kumi na moja na wamemsajili akiwa free agent!
Mwarabu awezi kumuacha mchezaji ambae ni Bora ata siku moja ukiona ivyo ujue ni wale wale wakina sawadogo!
 
8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom