Kwa miaka ya karibuni huyu bwana amepanda sana chati na kuwa mmoja wa mamastermind wa uendeshaji wa nchi hii. Ukiacha nasaba na kuwa mkwe wa mama lakini pia ni waziri mwandamizi anayefoka kwenye maongezi yake kwamba yeye ndiye boss wa wakuu wa mikoa so hamna atakayefanya lolote anapoagiza. Ukitazama kwa undani kidogo utagundua mama kamuachia pia maamuzi yote ya ofisi kuu. Kaibuka ghafla sana, je ni merits kwamba ni smart sana, elimu nzuri anayo au tu kwa kuwa mkwe wa mama? Hatumjui vema katoka wapi
Anapojinadi anakua kavaa kofia ya kikomunisti (nafikiri anamuiga Che Guevara) ambayo bahati mbaya sana vijana wa kisasa hawajui hata maana yake, nikifikiri ndio message anayotaka kuwapa.
Kwa mustakabali wa nchi yetu, na kuwajua viongozi wetu vizuri, na kwa nguvu aliyonayo sasa sio ajabu kabisa kuja mbele ya safari kuona anapewa uongozi wa nchi, ukizingatia trend ya sasa na uongozi kwenda kwa ndugu na jamaa wa familia zilezile, sisi kenge wa mama naamini tuna haki ya kumfahamu vyema.
Wanabodi wa nyumba hii wanafahamu mengi na hebu sasa tufunguke kumfahamu vyema mkomunisti huyu wakati tukiendelea kuona itikadi hiyo ikifa taratibu!