Mchengerwa: Hatutaki dawa feki Tanzania

Mchengerwa: Hatutaki dawa feki Tanzania

Atukuzwaye

Senior Member
Joined
Oct 5, 2026
Posts
116
Reaction score
117
Waziri wa Afya, Mohamed Mchengerwa ameitaka Bodi ya Ushauri ya Wizara kwa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba Tanzania (TMDA) kuhakikisha inasimamia kwa uadilifu ubora na usalama wa dawa Nchini, huku akisisitiza kuwa Serikali imeweka kipaumbele katika kuhakikisha Tanzania inakuwa na uwezo wa kuzalisha dawa zake yenyewe.

Akizungumza leo, Oktoba 20, 2026, wakati wa uzinduzi wa Bodi hiyo, Mchengerwa amesema moja ya majukumu ya kwanza aliyokabidhiwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan baada ya kuingia Wizara ya Afya ni kuhakikisha Taifa linaongeza uwezo wa uzalishaji wa dawa, akieleza kuwa hilo ni jukumu la dharura na la kudumu kwa maendeleo ya Sekta ya Afya nchini.

Mchengerwa amesema mafanikio ya TMDA katika kufikia viwango vya kimataifa ni muhimu kwa Tanzania kupata nafasi katika Soko la Dawa barani Afrika na duniani, huku akisisitiza kuwa hakuna Nchi itakayonunua dawa kutoka Tanzania iwapo vyeti vya mamlaka hiyo havitaheshimiwa Kimataifa.

Aidha, ameitaka Bodi hiyo kuhakikisha mifumo ya TMDA inaunganishwa na mifumo ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), ili kuzuia dawa ambazo hazijasajiliwa na TMDA kulipiwa kupitia bima ya afya, hatua ambayo amesema itasaidia kuimarisha udhibiti wa dawa Nchini
MILAAAADD.jpg
 
Waziri wa Afya, Mohamed Mchengerwa ameitaka Bodi ya Ushauri ya Wizara kwa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba Tanzania (TMDA) kuhakikisha inasimamia kwa uadilifu ubora na usalama wa dawa Nchini, huku akisisitiza kuwa Serikali imeweka kipaumbele katika kuhakikisha Tanzania inakuwa na uwezo wa kuzalisha dawa zake yenyewe.

Akizungumza leo, Oktoba 20, 2026, wakati wa uzinduzi wa Bodi hiyo, Mchengerwa amesema moja ya majukumu ya kwanza aliyokabidhiwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan baada ya kuingia Wizara ya Afya ni kuhakikisha Taifa linaongeza uwezo wa uzalishaji wa dawa, akieleza kuwa hilo ni jukumu la dharura na la kudumu kwa maendeleo ya Sekta ya Afya nchini.

Mchengerwa amesema mafanikio ya TMDA katika kufikia viwango vya kimataifa ni muhimu kwa Tanzania kupata nafasi katika Soko la Dawa barani Afrika na duniani, huku akisisitiza kuwa hakuna Nchi itakayonunua dawa kutoka Tanzania iwapo vyeti vya mamlaka hiyo havitaheshimiwa Kimataifa.

Aidha, ameitaka Bodi hiyo kuhakikisha mifumo ya TMDA inaunganishwa na mifumo ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), ili kuzuia dawa ambazo hazijasajiliwa na TMDA kulipiwa kupitia bima ya afya, hatua ambayo amesema itasaidia kuimarisha udhibiti wa dawa NchiniView attachment 3694157
Maneno na vitendo vifanane
 
Back
Top Bottom