Hatujui tuendako kwa sababu tupo gizani, tumekuwa gizani kwa miaka karibu mitatu na upo uwezekano tutaendelea kuwa gizani kwa karibu miaka mingine miwili. Katika muda huo tumeshuhudia juhudi za kila wanaojaribu kututoa gizani zikibezwa na wale ambao kubaki kwetu gizani ndio salama yao. Mabaunsa wenye sura za kutisha na wenye misuli iliyojengeka wamekaa milangoni kuhakikisha hatoki mtu. Mwanga, utakaomulika hata yale yanayowezekana tu gizani kama rushwa, hujuma, ufisadi na maovu yote yanayofanyika kwa kificho, hauna nafasi humo.
Leo tunashtuka umeme kukatika nchi nzima utafikiri sio sisi hao hao ambao kila tukipata nafasi ya kuchagua kati ya mwanga na giza, hukimbilia giza. CCM na jemadari wake ukiwawashia taa ghafla watapofuka macho kwa athari za giza zilizowaathiri mpaka watoto na wajukuu zao. Uzuri moja ni kuwa giza haliwezi kushamiri kwenye mwanga na tumaini lililobaki ni kuwa hofu ya mwanga ulioanza kutokea kwa mbali inawatia kiwewe - shuhudia walivyoanza kugongana wenyewe kwa wenyewe humo gizani na si ajabu hawautaki mwanga hata kwa miaka mia ijayo !!