Mchele Shilingi Elfu kumi kilo tatu!! Kikwete uko wapi?

Inauma sana kuona kuna watu wanaweza kumudu magari yanayowafanya watumie laki kwa siku kununua mafuta, wengine tunafikiria bei ya mchele kufika 2700!
Haya matabaka ni ishara mbaya sana ya kutuparaganyisha. Yes tunataka mabadiliko, lakini nani wa kumuamini? Kila mtu kigeugeu... Leo hapa mimi na wewe tunaandika waraka huu, tukifika makazini kwetu tunategea majukumu na pengine hata kunyanyasa wateja na wahitaji huduma zetu, wengine tunakula rushwa na mali za uma hivi hivi kwa kisingizio nikiacha mungine atakula tu... Hili taifa lina matatizo mengi mno, siasa is just a tip of an iceberg.
 
Wakulima nao wameamua.
Jibu analo waziri wa kilimo, atuambie kazi yake nini na yuko wapi ndo maana Kikwete alimweka kuhakikisha watanzania wanakula na kushiba.
Ukijaribu kufikiria waziri a kilimo hana cha kufanya...hapa gharama za uzalishaji wa chakula kutokanana sera mbovu hasa ktk mambo ya mafuta. utakuta mkulima anatumia pembejeo zenye bei kubwa na vilevile husafirisha mazao yake kwa bei kubwa....hapo unategemea nn? kwa taarifa yako mkulima kule shambani bado ana hali ngumu kama hujui! pamoja na kuwa beo sokoni ni kuba lkn hali siyo nzuri kwa wakulima...
 
Hili swala kwamba washauri wake hawamwambii ukweli JK wa hali halisi ya ugumu wa maisha nchini si kweli na inakera. JK anaona na anajua kila kitu . kama anaweza kuhudhuria misiba uswahilini ndani ndani huku mbagala kwa mtongore na sijui wapi huko asijue bei za vyakula zimepaa? Ukweli ni kwamba hatuna raisi.
 
Inauma sana kuona kuna watu wanaweza kumudu magari yanayowafanya watumie laki kwa siku kununua mafuta, wengine tunafikiria bei ya mchele kufika 2700!
Haya matabaka ni iLeo hapa mimi na wewe tunaandika waraka huu, tukifika makazini kwetu tunategea majukumu na pengine hata kunyanyasa wateja na wahitaji huduma zetu, wengine tunakula rushwa na mali za uma hivi hivi kwa kisingizio nikiacha mungine atakula tu... Hili taifa lina matatizo mengi mno, siasa is just a tip of an iceberg.shara mbaya sana ya kutuparaganyisha. Yes tunataka mabadiliko, lakini nani wa kumuamini? Kila mtu kigeugeu...

Ndugu yangu haiwezekani Raisi akawa mla rushwa wafanya kazi wengine wakawa sio wala rushwa...kama huamini hilo

linganisha mataifa yote yaliyofanikiwa kupunguza vitendo vya rushwa!

Tusikwepe tatizo, tuna kiongozi ambaye hashughilishi kichwa ndiyo maana unaona tuna matatizo mengi.!

Haiwezekani watanzania hawahawa waliokuwa wachapakazi na wasiondekeza rushwa wakati fulani......

waamue tu kuwa wazembe na walarushwa wakubwa!....hapana think, Uongozi legelege hasahasa wa raisi na mfumo

anaoutegemea...lkn hasahasa raisi(maana anauwezo wa kubadili hata mfumo ili kuliletea maendeleo taifa).
 
Kikwete c yupo magogoni
Jamani mwenzenu, nimepatikana wiki hii.
Mchele jamani, ukitoa shilingi elfu kumi unapata kilo tatu tuu!!!!
Sasa hivi kilo moja sh 2700 hadi 3000!!!!!! .....nchii imefikaje mahali hapa tutawalishaje watoto wetu? ilhali vipato vyetu vifinyu?

Hivi tuna raisi kweli? anajua mambo haya?.....au anadanganywa? taarifa sahihi za maisha haambiwi na wasaidizi wake?
Hivi matatizo yetu watanzania inamaana hayamhusu raisi wetu??.............
..............ndiyo maana anaitwa kichwa cha nanihii, kwa kufumbia macho matatizo ya wananchi!
 
Juz nilikua kwao BWAGAHEART,MCHELE 2400,unga kilo buku
Jamani mwenzenu, nimepatikana wiki hii.
Mchele jamani, ukitoa shilingi elfu kumi unapata kilo tatu tuu!!!!
Sasa hivi kilo moja sh 2700 hadi 3000!!!!!! .....nchii imefikaje mahali hapa tutawalishaje watoto wetu? ilhali vipato vyetu vifinyu?

Hivi tuna raisi kweli? anajua mambo haya?.....au anadanganywa? taarifa sahihi za maisha haambiwi na wasaidizi wake?
Hivi matatizo yetu watanzania inamaana hayamhusu raisi wetu??.............
..............ndiyo maana anaitwa kichwa cha nanihii, kwa kufumbia macho matatizo ya wananchi!
 
Ukekuwa mkulima wa mpunga hiyo bei ingekunufaisha na ungeifurahia.Je ungempongeza raisi(Kikwete) au ungewahurumia walaji wanaonunua?

Kumbuka hata mkulima huyo wa mpunga naye hazalishi bure naye kunagharama zilizoongekezeka km vile wasaidizi, mbegu na ukoboaji nk. nk.
 
Yaani jana niikuwa Sinza Makaburini karibu na maduka ya nafaka dada mmoja akashuka kwenye gari akaulizia bei ya mchele akaambiwa kilo 2800 alirudi nyuma huku akisema hiyo siwezi ku-afford. Yaani maisha yamekuwa magumu hadi dagaa na maharage nayo yamekuwa anasa.
 
Kaka, dagaa wa kigoma kariakoo kilo moja shilingi 20,000/=!!!!
 
Sasa wajameni, haka kabwana brazemen kenyewe bei ya mchele hata ikipanda, au ikishuka inakasaidia nini...??? Kila kitu kanapata bule kwa kodi tunazolipa SISI kwanza hata sijui kama kwenye salary yake na kenyewe kanakatwa kodi...!!
NSSF yake sijui katachukua kakistaafu au hakana mpango nayo kama Uncle Benja alivyogoma kwenda kuchukua NSSF yake...????

Kama mchele umepanda bei, usilalamike sana nunua unga kula ugali kila siku,au nenda pale fell kuna mama ntilie wali nyama na maharage mwingi kichzi 1000 sijui wao wanautoa wapi...????
 
Ukekuwa mkulima wa mpunga hiyo bei ingekunufaisha na ungeifurahia.Je ungempongeza raisi(Kikwete) au ungewahurumia walaji wanaonunua?

Si kila 'higher price' inamnufaisha muuzaji pia tofautisha baina ya individual higher price na 'inflation'. Maisha yanaendeshwa kwa 'factor movement' Sasa jiulize hali inakuwaje ikiwa mkulima huyo anayeuza mchele bei ya juu then anapambana na pembejeo,na mahitaji mengine pia bei juu?
 
Back
Top Bottom