Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 25,860
- 50,644
Anatakiwa mchawi aliyebobea ama awe wa makafara au mchawi wa matunguli ambaye atakuwa na uwezo wa kubadili hali ya mambo kwa muda mfupi sana. Mchawi huyo awe na nguvu ya kupindua mazindiko ya mizimu ama ya "Kisomo" yaliyowekwa kwenye eneo lolote lile hata kama eneo hilo linalindwa kwa hali ya juu kiasi gani.
Malipo yake yatategemea kumaliza kazi yake kwa wakati na kwa lengo lilokusudiwa. Nafasi hii ipo wazi hata kwa wale wenye uwezo wa kuvuta majini bahari yafanye "Shughuli" na kama wewe una mizukule ama vibwengo na vinyamkela pia unakaribishwa.
Mtu anayetakiwa kulogwa anatakiwa arudi kwenye utimamu wa akili yake kwani hali aliyo nayo sasa inamfanya apende sifa hadi jina lake mwenyewe amelisahau badala yake anajitambulisha kwa jina la marehemu babu yake!! Anayelogwa anaonekana kama vile amekuwa kichaa na mlogaji anatakiwa amloge ili arudi kwenye utimamu wake!!