SoC01 Mchango wangu kuhusu Tanzania

Stories of Change - 2021 Competition

mussaamos

New Member
Jul 15, 2021
4
3
Mchango wangu in kama ifuatavyo:-

Uchumi na biashara- Serikali itoe elimu kwa wananchi kuhusu biashara na kodi, pia iweke kodi rafiki kwa wafanyabiashara ili watu wengi zaidi kutoka ndani na nje ya nchi washawishike kuwekeza katika biashara na uchumi wa watu na taifa utakua. Pia serikali ijikite katika vyanzo vingine vya mapato kama vile uchukuzi, maliasil, madini na hata bahari na maziwa kujiongezea mapato, na iwashirikishe wananchi juu ya fulsa zilizopo kwenye sekta hizo.

Uchujmi wa nchi hutegemea zaidi viwanda ambavyo vitazalisha bidhaa na kuuza nchini na nje ya nchi na lazima, serikali ihamasishe wananchi na wawekezaji wa nje ya nchi na kuwaonesha fursa za viwanda vilivyopo nchini ili wenye uwezo wawekeze pia iweke mazingira rafiki kwa wawekezaji wa viwanda na kupunguza mlolongo wa kodi.

Utawala bora na uwajibikaji, demokrasia na haki za binadamu:- kila kiongozi ni vyema kuongoza watu wa kufuata misingi ya utawara bora wenye kuheshimu haki za binadamu. Viongozi waongoze kwa kuzingatia sheria na kanuni zilizopo pia kuwe na sheria itakayowawajibisha pindi wanapoenda kinyume na sheria.

Viongozi wahubiri amani, upendo na mshikamano kwa watu. Chaguzi ziwe za huru na haki na viongozi Wakubali kushindwa au matokeo ya chaguzi, pia Serikali isimamie usawa wa kijinsia katika jamii, ikomeshe masuala ya unyanyasaji wa kijinsia, iweke mfumo mzuri utakaowawezesha watoto waliojifungulia majumbani kuendelea na masomo. Kwasasa kuna suala la ulawiti kwa watoto wadogo, wanabakwa na kuingiliwa kinyume na maumbile na Mara nyingine na ndugu zao, hali hii inasababisha watuhumiwa kutojulikana kwa swala kumalizwa kifamilia, naiomba serikali ijikite katika kutoa elimu kwa wazazi ili waache kuwafumbia macho watuhumiwa pia serikali iweke adhabu Kali juu ya wanaopatikana na ukatili huo ili iwe fundisho na onyo kwenye jamii.

Sayansi na teknolojia:- Naishauri serikari ipitie upya mitaala ya elimu hasa katika masomo ya sayansi yawe ya vitendo zaidi ili kuzalisha wasomi wanaoendana na ukuaji wa sayansi na teknolojia kwenye nchi zilizoendelea, pia serkali iwawezeshe vijana na vikundi vyote vinavyobuni vitu mbalimbali ili kuviendeleza.

Serikali iwaamini na kuwapa fulsa wataalamu mbalimbali wa sayansi na teknolojia ili kuwajengea moyo wa kujiamini na ubunifu. Serikali ilete wataalamu wa sayansi na teknolojia ambayo haipo nchini ili waweze kuja kuifundisha hapa hapa nchini kwa watu wengi badala ya kupeleka mtu mmoja mmoja kwenda kusomea huko nje ya nchi matokea yake anaajiriwa hukohuko badala ya kuja kuwafundisha wengine hapa nchini.

Kilimo:-
bado wananchi wengi nchini wanategemea kilimo, serikali itoe elimu kwa wananchi ili waanze kilimo cha kisasa na namna ya kupata mazao yaliyo bora yanayoweza kushindana katika soko la kimataifa, serikali kwa kutumia wataalamu wa kilimo waratibu na kuhakikisha mbegu bora za mazao zinamfikia mkulima pia itoe elimu na ihimize matumizi ya mbolea na aina ya udongo kwani wakulima hupata mavuno kidogo ilihali wametumia mbolea, na suala la bei ya mbolea pia liangaliwe upya sio kilo hamsini za mbolea ziuzwe 80000 halafu gunia la mahindi liuzwe 35000, serikali iandae soko la mazao mapema kuepusha wananchi kukopwa mazao yao.

Serikali iwape wakulima mikopo nafuu. Wananchi walio karibu na maziwa, bahari na mito wapewe elimu ya kilimo cha umwagiliaji. pia wananchi wapewe elimu juu ya kilimo cha samaki kwani kina faida nyingi sana, na pia wawekezaji wahamasishwe katika kuwekeza kwenye kilimo hasa cha umwagiliaji.

Afya:-
serikali kwa kushirikiana na sekta binafsi iboreshe miundombinu ya afya na kuhakikisha dawa zinapatikana hospitalini kwa gharama nafuu. Itoe elimu juu ya umuhimu wa bima za afya, na ihamasishe watu kupima afya zao Mara kwa Mara.

#NchiYanguTanzania.AmaniYangu.
 
Back
Top Bottom