Mchango wa vijana katika kuleta Uhuru wa nchi hii, kwanini vijana tusiandae mdahalo wetu sisi wenyewe?

PAZIA 3

JF-Expert Member
Jan 30, 2018
1,074
1,856
Kabla ya Tanganyika kujipatia Uhuru, vijana ndiyo walipigania kufa na kupona ili nchi yetu iachiwe na wakoloni, hatimae wakoloni walituachia nchi yetu, ndiyo maana leo hii tuna siku ya mashujaa( Hawa Ni vijana) waliopigania nchi yetu. Kwakuwa Sasa hivi tupo katika kipindi Cha uchaguzi mkuu, Kuna milengo miwili imetugawa sisi vijana.

Lipo kundi linathamini mapokeo ya mababu zetu/wazee wetu, yaan wanaamini misingi iliyowekwa kipindi tumejitawala Kama nchi huru, tuendelee kuitumia hapa namaanisha katiba iliyopo. Kuna kundi jingine linakuja kwa kasi, lenyewe linataka tuifumue misingi ya wazee wetu kwani katiba hiyo inampa Raisi mamlaka ya Ki mungu,, Alfa na Omega/ Hawa wanahoja zao nene, na kubwa wakiamini sera hiyo inaamika zaidi na wananchi.

Mi nimewaza, Hakuna haja ya sisi vijana kujificha nyuma ya keyboards, tuitishe mdahalo kitaifa, kila mwenye uwezo wa KUFIKA kwenye mdahalo, ajiandikishe. Tunaitaji kusikia sera za Hawa vijana wakitetea ilani za vyama vyao. Inawezekana, Kama inawezekana, tushare thread hii iwafikie ITV Tanzania alhamisi siku ambapo huwa Kuna nidahalo ya wazi
 
Kama hata hapa wameshindwa kufika basi hiyo siku ungefika peke yako mkuu.

Mimi natamani wafumue mfumo wa elimu ila ndo hivyo sauti ni ndogo na vijana wengi hawajitambui hivyo hakuna ushirikiano wapo kule MMU.
 
Vijana tugawanywa sana kupunguza nguvu zetu pia vijana tunadanganywa kwa ni wa kesho wakat kesho huandaliwa leo
 
Kabla ya Tanganyika kujipatia Uhuru, vijana ndiyo walipigania kufa na kupona ili nchi yetu iachiwe na wakoloni, hatimae wakoloni walituachia nchi yetu, ndiyo maana leo hii tuna siku ya mashujaa( Hawa Ni vijana) waliopigania nchi yetu. Kwakuwa Sasa hivi tupo katika kipindi Cha uchaguzi mkuu, Kuna milengo miwili imetugawa sisi vijana.

Lipo kundi linathamini mapokeo ya mababu zetu/wazee wetu, yaan wanaamini misingi iliyowekwa kipindi tumejitawala Kama nchi huru, tuendelee kuitumia hapa namaanisha katiba iliyopo. Kuna kundi jingine linakuja kwa kasi, lenyewe linataka tuifumue misingi ya wazee wetu kwani katiba hiyo inampa Raisi mamlaka ya Ki mungu,, Alfa na Omega/ Hawa wanahoja zao nene, na kubwa wakiamini sera hiyo inaamika zaidi na wananchi.

Mi nimewaza, Hakuna haja ya sisi vijana kujificha nyuma ya keyboards, tuitishe mdahalo kitaifa, kila mwenye uwezo wa KUFIKA kwenye mdahalo, ajiandikishe. Tunaitaji kusikia sera za Hawa vijana wakitetea ilani za vyama vyao. Inawezekana, Kama inawezekana, tushare thread hii iwafikie ITV Tanzania alhamisi siku ambapo huwa Kuna nidahalo ya wazi
Wazo zuri
 
Back
Top Bottom