SoC02 Mchango chanya wa mitandao ya kijamii kwa vijana wa karne ya 21

Stories of Change - 2022 Competition

YESSE BRANSTONE

New Member
Aug 3, 2022
1
1
MCHANGO WA MITANDAO YA KIJAMII KWA VIJANA

Karne ya 21 ni karne ambayo kumekuwa na mabadiriko makubwa katika maisha ya binadamu katika nyanja mbalimbali kama vile kiuchumi, kijamii, kisiasa na kiutamaduni. Mabadiriko haya yamewafanya watu wengi kuweza kufikiria namna mbalimbali za kuweza kujikwamua au kuondokana na changamoto ambazo zinajitokeza katika maisha yao. Katika jamii kuna watu mbalimbali wenye rika tofautitofauti kama vile watoto, vijana, watu wazima na wazee. Lakini, kati ya makundi haya yote vijana wanaonekana kuwa na idadi kubwa sana kuliko kundi lolote lile katika jamii, kundi ambalo licha ya uwapo wao kwa wingi limekuwa likikumbwa na changamoto mbalimbali hasa katika suala zima la kutafuta kazi au ajira kwa ajili ya kujikimu kimaisha na kutimiza mahitaji yao. Kutokana na wingi wao imefanya hata kazi zinazopatikana katika jamii kutoweza kuwafikia vijana wote.

Ni kweli kuwa vijana wengi katika jamii wamepata fursa ya kupata elimu rasmi lakini ajira imekuwa changamoto sana, jambo ambalo baadhi yao limewafanya kuwa katika hali ambazo hazipendezi na kuwasababisha kufanya mambo ambayo yako kinyume na maadili kama vile ukabaji, wizi, ubakaji, uvutaji wa madawa ya kulenya, uchangudoa na ushoga.

Endapo kijana wa leo angeweza kuamka na kutazama ulimwengu upo kwenye zama gani basi baadhi ya changamoto zingeisha kabisa na kumfanya kijana huyu kuweza kumudu maisha kwa njia mbalimbali ambazo ni za haki na kweli. Ni wazi kuwa, mitandao ya kijamii endapo ikitumiwa katika hali chanya basi inaweza kuleta mabadiriko makubwa kwa vijana na kuwafanya waweze kupunguza au kuondoakna na changamoto ambazo zinawakumba katika maisha yao. Hii ni kutokana na kwamba ulimwengu upo katika ngazi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ambayo kimsingi inaweza kusaidia kwa kiwango kikubwa kumtoa kijana wa leo katika ngazi ya chini na kumpandisha ngazi ya juu.

Vijana wengi sana wamejiunga katika mitandao mbalimbali ya kijamii kama vile Twitter, Instagram, Facebook, WhatsApp, Youtube, Google na nyinginezo lakini wengi wamekuwa walifanya mambo mbalimbali yanayozidi kuwaporomosha kimaadili, kimtazamo, kiuchumi na kisaikolojia. Hii ni kutokana na kwamba wengi wao hupoteza muda na fedha nyingi kwa ajili ya kufatilia mambo ambayo hayana msaada katika maisha yao ya leo na kesho kwa mfano kuangalia picha na video za uchi, kufatilia habari za umbea na udaku na kutupia picha ambazo zinaihaibisha jamii na kukiuka utamaduni wa jamii husika. Nilimsikia kijana mmoja anasema nikikosa bando kwenye simu yangu nakosa raha kabisa na ni bora nikose chakula kuliko kukosa bando lakini nilipomuuliza huwa unatumia bando lako kufanya nini akasema huwa napenda kufatilia habari za umbe na udaku na kuangalia hasa wasanii wameposti nini katika akaunti zao (Chanzo cha mfano huu ni Uwandani). Kutokana na mfano huu inaonesha wazi kuwa wengi wa vijana katika jamii wamekuwa wakitumia mitandao ya kijamii kwa ajili ya kufanya au kuangalia mambo ambayo si sahihi.

Ajira zimekuwa ngumu sana kupatikana, fursa nazo zimekuwa changamoto kwani wengi wa vijana wanakosa jicho la kuona fursa zinazowazunguka kutoakana na upofu ambao umesababishwa na uraibu unaotokana na mitandaoya kijamii. Ajira ni chache lakini kazi za kufanya zipo nyingi sana katika jamii na fursa pia zipo nyingi zinazojitokeza lakini wengi wanazikosa kutokana na kwamba mitandao ya kijamii wameipatia maana nyingine ambayo ni hasi.

Kazi kubwa ya mitandao ya kijamii ni kujenga mahusiano, ushirikiano na kuwezesha mawasiliano ya mtu na mtu, jamii na jamii au hata taifa. Na ndio maana kuna msemo unaosema “haijalishi unachokijua bali unamjua nani” msemo huu umeibuka hivi karibuni kutokana na kwamba wahitaji wa ajira, fursa mbalimbali au kazi wamekuwa wengi. Jambo ambalo kuja kufanikisha jambo hilo muda mwingine itakuhitaji uwe na mtu au watu unaowafahamu na jambo hilo linaweza kuwezeshwa zaidi na mitandao ya kijamii. Kwani ina uwezo wa kuunganisha mtu na mtu, jamii na jamii au taifa na taifa.

Mitandao ya kijamii kwa karne hii imekuwa na watumiaji wengi sana na kwa maana hiyo fursa nyingi zipo katika mitandao ya kijamii. Lakini, changamoto ya vijana wengi ni kuona fursa hizo zilizopo katika mitandao hio. Vijana wachache ambao wamegundua hili wameweza kupiga hatua mbele kila siku katika maisha yao. Kwa mfano, kwa wafanyabiashara na wajasiriamali wanaouza vitu mbalimbali au hata kutoa huduma mbalimbali katika jamii kwa sasa ni rahisi sana kukutana na wateja wengi au wahitaji wa huduma husika katika mitandao ya kijamii kutokana na kwamba wengi sasa hivi wamejiunga katika mitandao ya kijamii kutokana na ujio wa simu janja na kompyuta.

Pia, kila siku katika mitandao mbalimbali ya kijamii kuna biashara zinaendelea kufanyika dunia nzima zenye mabilioni ya fedha ambayo huitaji mtu mwenye ujuzi ambaye anaweza kuifanya biashara hizo kwa mfano biashara ya ubadilishanaji pesa (Forex Trading) biashara inayoongoza kuwa na mzunguko mkubwa wa pesa duniani kila siku, utafutaji wa masoko ya bidhaa mbalimbali, biashara za karne ya 21 wengi wakizijua kama Network Marketing of 21 century) zinaendelea kila siku na zinazidi kudunguliwa kadri muda unavyosonga. Fursa zote hizi haziwezi kufanyika au kufanywa bila kuwa na ujuzi na maarifa ya kuwezesha utekelezaji wake.

Lakini, cha kufurahisha ni kwamba hata maarifa ya namna fursa hizo zinavyofanyika zinapatikana katika mitandao ya kijamii kama vile Google na Youtube ambapo unaweza kuingia kutafuta kile ambacho unakihitaji katika utekelezwaji wa fursa hizo na zaidi. Endapo, wengi wa vijana wataacha uvivu wa kutopenda kusoma na kutafuta maarifa pamoja na kuacha kufatilia mambo ambayo kimsingi hayawezi kuwanufaisha katika maisha yao.
 

Attachments

  • story change.docx
    14 KB · Views: 6
Back
Top Bottom