Ndugu wana jf salam! naomba nielweshwe hapa. kuna uhusiano gan kati ya Habibu Mchange na Said Arfi? hebu someni hapa:-
Subject: TANZANIA HAIHITAJI VIONGOZI WAROPOKAJI : ARFI
From: Said Amour Arfi (said_arfi@yahoo.com)
To:
mchangehabibu@yahoo.com;
Date: Sunday, August 10, 2014 11:59 AM
TANZANIA HAIHITAJI VIONGOZI WAROPOKAJI : ARFI
Najua unayo mamlaka ya kuhariri lakini nitapenda isomeke kama nilivyoandika hapo juu.
Katika gazeti lako la leo Mwananchi August 09 ukarasa wa pili "wajiandae kuwa Wabunge wa Mahakama
imeandikwa na Julias Mathias " katika habari hio nami nimetajwa kwa jina napenda kumkumbusha Lissu
kama anapenda kusema akili yake isiwe ya kusahau ni hatari kwa Kiongozi na wala hataepuka kuitwa
mropokaji naomba arejee kauli yake iliyoandikwa pia na gazeti lako la 27.06.2014 Nanukuu
"......kutoruhusiwa kushiriki shughuli za kambi hio......"" Lissu anapata wapi uhalali wa kuhoji matendo na
maamuzi yangu wakati wamenitenga kinyume na kanuni za kambi rasmi hivi Lissu ni nani anapoka
mamlaka na kuachiwa katika suala hili angewaachia wenye akili na busara kushughulikia na kulisemea na
si Lissu.
Aidha kukaa kimya si ujinga ni busara tu lakini si kwa kila jambo utaacha kusema huyu Lissu
anapolazimisha kwamba hatushiriki mpaka uongozi wa BMK watoe ufafanuzi wa kifungu cha 25 cha
sheria ya mchakato wa Katiba sura ya 83 anajidanganya na kuwadanganya Watanzania Bunge kazi yake
kutunga Sheria na chombo cha Kikatiba cha kutafsiri sheria ni Mahakama ningemuelewa vyema kama
Lissu Mwanasheria angetushauri kwenda Mahakamani kusimamisha Bunge hili kupata tafsiri ya sheria na
sio kushawishi kutoka.
Mwisho hivi huyu Lissu haoni hata chembe ya aibu na kuheshimu maoni ya watu na viongozi wa dini
kututaka kurudi Bungeni lakini ameweza kusema hadharani kuwajibu viongozi wa BAKWATA mbona
hakufungua mdomo wake kuwajibu viongozi wa Makanisa au la Maaskofu Katoliki Tanzania Mimi
nawaheshimu sana viongozi hawa nimewasikia na kuwatii
Lissu weka akiba ya maneno usiwe mropokaji Tanzania inahitaji viongozi makini waliotulia
Said A Arfi (MB)
Sent from my iPad
naomba kuwakisha jamani!