ACT Wazalendo
JF-Expert Member
- May 5, 2014
- 610
- 1,540
MCHAKATO WA KUPATA TUME HURU YA TAIFA YA UCHAGUZI (NEC) UANZE SASA
Chama cha ACT Wazalendo, kupitia kwa Makamu Mwenyekiti Tanzania Bara ndg Isihaka Rashid Mchinjita, kimewataka Wajumbe wote wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) wajiuzulu ili mchakato wa kuundwa kwa Tume mpya ya Uchaguzi uanze kwa mujibu wa Sheria ya Tume ya Uchaguzi iliyopitishwa na Bunge hivi karibuni.
Tume mpya itakayopatikana kwa ushindani wa Watanzania kuomba, kusailiwa na Jopo Maalumu, kuchujwa na kisha kuteuliwa;
1. Iratibu Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa mwishoni mwa mwaka huu 2024, na
2. Iendeshe Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025
Kwa heshima na taadhima, makamishna wa NEC waliopo wanapaswa kuwapa nafasi Watanzania kupata NEC mpya kwa mujibu wa Sheria mpya ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
Busara inataka WAJIUZULU KWA MPIGO (enmass)