Mchakato wa kumpata Mrithi wa Askofu Shoo kuanza hivi karibuni

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,379
8,124
Safari ya kumsaka mrithi wa Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofu Fredrick Shoo, inatarajia kuanza wakati wowote kuanzia sasa wakati kikao cha Halmashauri Kuu ya Kanisa hilo kikitarajiwa kukaa ili kupokea majina matatu ya maaskofu waliopendekezwa kugombea wadhifa huo wa juu.

Kikao hicho cha Halmashauri Kuu kitaketi chini ya Askofu Shoo ambaye ni Mkuu wa Kanisa wa KKKT anayemaliza muda wake wa uongozi wa miaka nane, kikao kinachofanyika katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Makumira (TUMA), kilichopo Makumira mkoani Arusha.

Waandishi wa Mwananchi Digital walifika mapema katika ukumbi huo, walielezwa kuwa kikao cha Halmashauri Kuu kinakutana muda wowote kuanzia sasa baada ya kukamilika kwa ibada iliyokuwa ikiendelea ukumbini.

"Tukimaliza hiki kinachoendelea sasa hivi ndio Halmashauri Kuu ya Kanisa itakaa kupokea majina matatu ya maaskofu yaliyopata kura nyingi na hao ndio watakuwa wagombea wetu. Kila kitu kinakwenda vizuri sana kuliko hayo yanayosemwa mitandaoni," amesema mmoja wa maofisa wanaoshughulika na uratibu wa mkutano huo.

Kulingana na Katiba ya KKKT, katika hatua ya kwanza, Mkuu wa Kanisa ataitisha faragha ya maaskofu waliopo kazini kwa makusudi ya kuimarishana, kuzungumza na kuombea agenda ya uchaguzi na itaitishwa kabla ya Halmashauri kuu.

Halmashauri Kuu katika kikao kitakachotangulia mkutano mkuu, itapendekeza majina yasiyozidi matatu na kuyapeleka mbele ya mkutano mkuu ili yapigiwe kura na mchakato wa kupata majina hayo matatu umeanishwa kikatiba.

Kila mjumbe wa Halmashauri Kuu ataandika majina matatu kutoka miongoni mwa maaskofu wanaoongoza Dayosisi za KKKT, majina yatakayoongoza ndiyo yatakayopendekezwa mbele ya mkutano mkuu wa uchaguzi mkuu wa Kanisa.

Mkutano mkuu utayapokea majina matatu kutoka Halmashauri kuu na mkutano mkuu unayo haki ya kuongeza jina moja ikibidi na utaratibu wa kupiga kura utakuwa wa kura ya kuandika na itakuwa ni utaratibu wa kura ya siri.

Mwenyekiti wa agenda ya uchaguzi wa mkuu wa Kanisa atachaguliwa na mkutano mkuu wa Kanisa miongoni mwa wajumbe wa mkutano mkuu na mkutano mkuu utawachagua watu watano ambao watahusika na kazi ya kuhesabu kura.

Katika zoezi la kupiga kura, kila mjumbe mwenye haki ya kupiga kura atachagua jina moja kutoka katika majina matatu yaliyowasilishwa mbele ya mkutano mkuu na mshindi lazima apate kura zisizopungua theluthi mbili ya kura zilizopigwa.

Iwapo mshindi hatapatikana katika duru ya kwanza, majina mawili yenye kura nyingi yataingia duru ya pili na iwapo kura ya theluthi mbili haitapatikana baada ya kupiga kura, kura ya uwingi wa uchache itatumika kwa duru ya tatu.

Miongoni mwa majina ya maaskofu yanayotajwa tajwa kuweza kumrithi Askofu Shoo ni pamoja na Mkuu wa Dayosisi ya Karagwe mkoani Kagera, Dk Benson Bagonza, Askofu Dk Abednego Keshomshahara wa Dayosisi ya Kaskazini Magharibi, Bukoba na Askofu Dk Blaston Gavile wa Dayosisi ya Iringa.

MWANANCHI
 
Bagonza na keshomshahara ni moto mkali mmoja anaweza kuwa mkuu wa kanisa na hasa bagoza. Huyo wa iringa hajulikani kama ni mhafidhina au mliberali.
 
Wasi wasi wangu . Je CCM Watakubali Bagonza awe askofu mkuu wa KKKT? Ni ngumu sana hii
 
Waumini tunataka mwenye hofu ya Mungu ambaye hawezi kunyamaza kukemea uovu unaofanyika nchini.mfano uuzwaji wa maliasili za nchi
 
Bagonza na keshomshahara ni moto mkali mmoja anaweza kuwa mkuu wa kanisa na hasa bagoza. Huyo wa iringa hajulikani kama ni mhafidhina au mliberali.
Begonia ni senior angeshskuwa askofu mkuu siku nyingi tatizo hakujiandaa kwa post kubwa Post kubwa mtu unatakiwa kujiandaa mapema kimaadili na utulivu

Yeye malaya kazaa nje na ushahidi upo na vyombo vya habari viliandika umalaya wake na kuzaa nje

Pili yeye mwanasiasa wa wazi wa Chadema

Askofu ni wa vyama vyote na wasio na vyama hatakiwi kuonyesha msimamo wake hadharani yeye chama gani hilo lilimshinda pia

Lakini angekuwa yuko vizuri angekuwa askofu mkuu hata kabla ya Malasusa au Shoo

Ila hajielewi yupo yupo tu anaishi kama hooligan wa barabarani. Cheo cha uaskofu ni kikubwa mno

Watapata wengine ila sio yeye

Elimu anayo nzuri tu ila tabia na self discipline na kuheshimu hadhi ya cheo cha uaskofu hana
 
Shoo ameisimamia vizuri show. Kanisa limekuwa tulivu na lenye muelekeo. Amefuata vizuri nyendo za Malasusa ambaye naye alilisimamia vizuri kanisa.
Ikiwapendeza maaskofu wamuongezee Shoo mwaka mmoja.
 
Shoo ameuza sana rasilimaliza kanisa na miradi mingi imefia mikononi mwake, analiacha kanisa na madeni mengi sana ya nje na ndani ya kanisa
 
Back
Top Bottom