Mchakamchaka/School morning jogging na Nyimbo zake

Mchakamchaka/School morning jogging na Nyimbo zake

Smallfish

JF-Expert Member
Joined
Feb 16, 2012
Posts
241
Reaction score
66
Nakumbuka jinsi nyimbo za mchakamchaka zilivyokua zinahamasisha wanafunzi kuwa wazalendo, amasa achilia kuwa fiti kimwili na kiakili. Mfano wimbo wa Iddi Amini, Banda, Mzee Jumbe .................... taja nyimbo zingine. Kwa nini waanzilishi na wabunifu wa nyimbo hizi wasijielekeze kutunga nyimbo za mafisadi, madawa ya kulevya nk.?
 
Unanikumbusha shule moja ilikuwa na eka 60 za mahindi na eneo kubwa la kufyeka...yaani unakuwa na mueneo mkuubawa wa kufyeka afu siku za kilimo unagawiwa miraba yako kama 15 hivi.

Sasa basi msimu huo kwenye mchaka "unalia nini kijana ..........(jina la shule) ulijaza mwenyeweeee..........
 
"Niko kilimani naranda nangojea pijo kupanda"

"Nani ajuae Nyerere ni mwenye! Aaaje-aajee simba mtu!"

"Kaburu matata hiyaaa-hiyaa"
 
"Niko kilimani naranda nangojea pijo kupanda"

"Nani ajuae Nyerere ni mwenye! Aaaje-aajee simba mtu!"

"Kaburu matata hiyaaa-hiyaa"

Hiyo ya Kaburu matata hiyaa ilikuwa bomba sana sisi tulikuwa tunasoma na mibaba mizima sasa yenyewe ndo inakuwa inatoa Bass kwenye kuitikia ile Hiyaaaa!

Mwingine ulikuwa unasema "KAMBONAAAA! AMEOLEWA, WAPI? HUKO ULAYA"

BANDA WA MALAWI, KATUVALIA NGOZI YA SIMBA KUTUTISHIA WATANZANIA, HATUJALI

Kipindi hicho shule ilikuwa na raha zake, sasa hawa wa sasa hivi masikini sijui hata kama wanakimbia mchakamchaka!!
 
Waukimbilie wapi! Job K ?
Now days watoto wako "English medium school"
 
Last edited by a moderator:
Nina nyimbo kibao hapa:
1. Mchaka mchaka chinja..... Aliselema Alija.....
2. Alisemaa, alisema. Alisema Nyerere, alisema, vijana wangu twende mchaka mchaka
3. Ntuji ondono adina na Sabo, alisobelwa na ganamhala .... Bayanda Ba lalucha Miso Guti Mbiti ilolile Gali ( Huu ni wa Kisukuma kwa wale wa Mikoa ya Kanda ya Ziwa)
 
Vijana wenu tumerejea,
Vita imemalizika,
Idi amin kakimbia,
Kachokoza tanzania,
Moto umemuwakia,
Cha ukweli amekipata,
Ingawa ameshajongo.........
Jamani wenzangu wa 1947 mnakumbuka kujongo? Kuwa selule? Kusogeza? Kuambiwa 'hi' unaitika 'moja'?
Hahahahaha Kambarage wa mwitongo alikuwa mwanaume ,alitunyooosha.
 
kuna hii...P***U la mzee likinasa kwenye ***A halitoki.......
 
1.Theresia twende Dodoma,tukalione gari la moshi..2.Harambeee oya oya,harambee wana twiga...Harambe harambe mchaka mchaka..

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Mbuga za wanyama Tanzania...ya kwanza ni serengeti Ngorongoro Manyara na mikumi ooh Tanzania oyeee!
 
Nina nyimbo kibao hapa:
1. Mchaka mchaka chinja..... Aliselema Alija.....
2. Alisemaa, alisema. Alisema Nyerere, alisema, vijana wangu twende mchaka mchaka
3. Ntuji ondono adina na Sabo, alisobelwa na ganamhala .... Bayanda Ba lalucha Miso Guti Mbiti ilolile Gali ( Huu ni wa Kisukuma kwa wale wa Mikoa ya Kanda ya Ziwa)
Mkuu wangu Bugota wewe ni mshenzi kichaa wangu!!

Yaani huo wimbo namba 3 nusura univunje mbavu eti "Vijana macho mekundu kama fisi anaangalia gari??!!" Bahati mbaya huu kwetu hatukuwahi kuuimba naamini utakuwa wa Mwanza ile ya mbali na barabara ya lami pamoja na Shinyanga yote! Ila kwa kweli enzi hizo kulikuwa na nyimbo nyingi za kutujengea uzalendo kwa nchi yetu. Eti alisema, alisema, alisema Nyerere alisema , vijana wangu wote mmelegea.......... Yale maneno mengine nimeyasahau mkuu!! Hii ilikuwa miaka ya 70's kuja mpaka 80's inagawa na wale wa 90's watakuwa waligusagusa kwenye haya mambo. Maskini juzi nikawauliza vijana wangu kama wanahabari na mchakamchaka! Wakasema hawajawahi kukimbia tangu wamejiunga na shule zetu hizi zilizotuzuzua (Eng. Medium)
 
Angola eeh las tayari sisi tunakuja
Tumesikia umejenga ngome ndicho kikwazo kwa muafrika
Watu wa mbele ongeza mwendo kdg kdg
Watu wa nyuma ongeza mwendo kdg kdg....
Na kibaridi cha alfajiri. Hakuna kuzubaa
 
... chama yupo chama yupo ukiona kundi la siasa chama yupo baba nyerere ongeza majela wafungwe wapinga ccm ongeza majela wafungwe........... sie tuliimba kama hivyo.
 
Last edited by a moderator:
Jumbe analia. iddi amini akifa mimi siwezi kulia, vumilia kidogo n.k
 
... chama yupo chama yupo ukiona kundi la siasa chama yupo baba nyerere ongeza majela wafungwe wapinga ccm ongeza majela wafungwe........... sie tuliimba kama hivyo.
Mamndenyi
haaaa haa unanikumbusha zama hizo vijana wakati wa wakati ule walikuwa wakakamavu hawa makamanda wako wapo laini kama mlenda ukichanganya na sembe wanalopiga ndio balaa nyanya ngumu!
 
Last edited by a moderator:
Wavulana wanapenda ku ku kumaliza shule

Wasichana wanapenda mbo mbo moga za majani

Ntakuto to tolea nje

Huu wimbo tuliimba 2001 tukiwa tunajiita LY aka wakubwa wa shule..Tulichapwa siku hiyo na adhabu kedekede ilikuwa shule ya jesh mwanzishaji mwimbo fimbo zake na waitikiaji za kwao.Kama kawaida watu wakaanza kujitetea"Mwalimu mie nilikuwa siitikii"Saut ya private inasikika hakunaaa njo hapa, haya chini paa paa paa fimbo kama kumi hiv. tuliacha usela tena.

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom