Kunta Kinte
JF-Expert Member
- May 18, 2009
- 3,690
- 1,293
Ni kweli kwani angekuwa mjane mjane tunaowajua hii isingetokea kwani inaonekana yeye ni Janet Kiwia's business profile as Chief Executive Officer at World Jet Travel Inc ambayo pia ina tawi Marekani. Hivyo huyu mama Rwaka (kama kweli ni yeye) alipima maji vibaya hapa.
Huyu mama ni al maarufu kama Lolita, amezaa na baba yake marehemu Nyaga watoto wawili Obre- wa La Liga Moshi na mdogo wake-Huyu mama ni mjanja wa siku nyingi mama Rwakatare hamuingii kwa lolote, kwa kweli hapa aliingia choo cha kiume!!
pale lazma azimie lile jengo ni hekalu la mafisadi sijui kama watadhubutu kubomoaTukitoka hapa tunahamia kwenye ile aliojenga kwenye Mkondo wa Bahari.
Umejuaje eneo ni la mjane wakati Mahakama ilikuwa imetoa stop order?Unawezaje kumtukana mwenzio mburura wa kwanza kwa mawazo yake ambayo hata wewe huwezi kujustify ukanushaji wako? Unaweza kuthibitisha kwamba huyo mama hataki kuuza ama kukaa mezani na kuongelea compensation? Matusi hayajengi sifa!. Kijana wa watu hata hakuonyesha tusi zaidi ya kupendekeza mawazo yake, na wewe una lipuka na matusi. Utamaduni gani huu katika mawasiliano?
Serikali,rwakatale na huyo mwenye viwanja wote mbuluraz,issue kama hiyo ni kukaa mezani tu!! Kama Mama mchungaji kavamia kiwanja serikali ingekaa kati kufanya win win situation kutafuta mtu wa kati ananue eneo mama mchungaji apate gharama alizotumia na aliedhulumiwa apate gharama ya kiwanja serikali ipate tozo ya kodi ya manunuzi....
Kondoo wanachungwa ili watumike kwa faida (waliwe, wauzwe, wakatwe sufi n.k).
Wachungaji hawafanyi kazi za hasara!
Mama hata mahakamani akiitwa alikuwa hataki kwenda hivyo uwezekano wa mashauriano yoyote kulikuwa hakuna!!!
Zote hizi ni sababu mkuu. Kwa mujibu wa sheria hata kama una umiliki halali wa eneo ni lazima upate BUILDING PERMIT toka mamlaka husika. Ukijenga bila kibali hata kama una hati ya kiwanja chako wakiamua kukubomolea wapo ndani ya matakwa ya sheria, kwasababu umekiuka sheria. Hivyo hata kama aliuziwa na kulikuwa na mgogoro wa umiliki, kisheria hakupaswa kujenga permanent structure yoyote mpaka michoro yake ya ramani ipitishwe na wahandisi wa manispaa na apewe kibali cha kuanza ujenzi.
Wewe umesoma wapi?udom? Au wapi? Maana nimejibu kam alivyotoa comment. Kwahio angalia kwanza hapo juu kwnaza aliandikaje.
The King.
Mbona hatukuelewi,andika vizuri basi
Mkuu hebu acha kubisha vitu vilivyo wazi bana. Hapa unatumia ubishi tu. Lakini kwa kukusaidia The Land Act of 1999, part XIV (Miscellaneous) kifungu 175, kinaongelea unlawful occupation of land. Ibara ya 2, inampa commissioner mamlaka ya kumsave mvamizi notice tu tena hata ya mdomo (ilimradi iwe kwa lugha atayoielewa) ya kuthibitisha umiliki na asipofanya hivyo anamwamuru atoke na mali zake iwe ni majengo, mazao nk. Tena imesisitiza "within anytime and subject to any conditions"! Zaidi hata kanuni zilizofuatia land Act zipo wazi kwenye hili. Commissioner hahitaji kufungua kesi eti kisa wewe umejenga bila permit.Kwa maana hii, kosa la kujenga bila permit hukumu yake ni moja, kubomolewa jengo bila haja ya mchakato kupitiwa na vyombo vya sheria? Nifashukuru ukinipa kifungu hicho cha sheria nikisome nipate mwanga zaidi.
Kuna watu wana hela zakupoteza sana yaani unajenga wakati umekatazwa
jamani pamoja na kwamba wote tunapenda pesa basi tutende haki. kama ni kweli mama rwakatare alimdhulumu huyu mjane arudi akamuombe msamaha
Kwa maelezo nyumba si ya Tibe John? Ya lwakatare kivipi?
Ha ha ha! Pesa za bure zipo, siku ya ibada. Mtoleeni Mungu