Kabla hujaamua kushangaa, ni vyema ukaelewa kwanza.
Madawa ya kulevya hayaongezi uchumi kwa sababu, japo wanajenga majumba, lakini athari za madawa ni kuua taifa. Kwamba wanaua afya za mili na akili kwa nguvu kazi na hiyvo kuathiri uzalishaji ambacho ndicho kiini cha maendeleo ya uchumi wa taifa. Na nyumba kama hazitumiki productively, si kitu kinachokuza uchumi wa taifa.
Pili usichanganye hoja. Hapa hatujadili chanzo cha mapato kwamba kavunjiwa nyumba kwa sababu amepata fedha kwa vyanzo haramu, kiasi cha kulinganisha na wanaojenga kwa mapato ya madawa ya kulevya.
Tatu, hao wahalifu wa madawa ya kulevya, hatuwezi kuwakomesha kwa kuwavunjia nyumba kama unavyoonekana kuelewa. KIla kosa liwe addressed kama lilivyo na ndivyvo sheria ilivyo.
Kosa la kumdhurum mjane, linasemwa leo, lakini siku za nyuma kulikuwa na taarifa amejenga katika eneo lisiloruhusiwa na hivyo kaharibu mazingira. ( Huyo mjane ndiye angerehusiwa kujenga asiharibu mazingira ama anamiliki eneo lile kwa matumizi gani? Mimi na wewe hatuna jibu kwa sasa). Ninachohitaji kionekane ni namna gani kunaweza kuwa na namna ya utafutwaji mtu hapa.
HOJA KUU, SIONGELEI UHALALI WA UMILIKI WA ENEO LILE. KILICHONISHANGAZA, NI KUONA WATU WANAVUNJA SHERIA NA SISI TUNASHANGILIA KWAMBA HAKI IMETENDEKA. HIYO HAKI KAIAMUA NANI?
NI DHAHIRI KWAMBA KULIKUWA NA MAAMUZI YA KISHERIA YALIYOASISI UVUNJWAJI WA NYUMBA ZILE. KINACHONIPA SHIDA NI ILE KUSEMA NYUMBA ZILE ZILIENDELEA KUVUNJWA HATA BAADA YA KUWASILISHA STOP ORDER KUTOKA MAHAKAMANI.
SHERIA MSUMEMONO, TUNAYOISHANGILIA INATAKA BAADA YA HIZO STOP ORDER KUWASILISHWA, ILITAKIWA KILA KITU KISIMAME, WAENDE MAHAKAMANI KUENDELEA NA MCHAKATO WA KUPATIKANA KWA HAKI. KUENDELEA NA EXECUTION WAKATI MAHAKAMA, IMEAGIZA WASIFANYE NI UVUNJAJI WA SHERIA!. SIJUI KAMA UMEELEWA.
ndg yangu sheria ni msumemo, unataka kuniambia wale wanaotakatisha fedha za dawa za kulevya kwa kujenga mahekalu waachiwe kwa sababu wanaongeza uchumi wa taifa.? Umenishangaza kweli kweli