Mch. Rwakatare avunjiwa nyumba

Mch. Rwakatare avunjiwa nyumba

Suala la dini lilmetoka wapi hapa? Usihukumu kabla hujapata undani wa jambo. Hujui huyu mama hilo eneo alilipataje. Watu wangapi wanauziwa maeneo ya hata kuwa na hatimiliki baadaye wanajikuta wengi wanahatimiliki za eneohilo na eneo ni open space? Ni vyema ungetafuta kwanza kufahamu, yeye alilipatje hilo eneo.Pili, inaonekana elimu yakok ya dini imekaa kisiasa zaidi na si kiroho. Vinginevyo nakushauri utafute tafsiri sahihi ya siasa na dini halafu utaelewa namna gani zinahusiana, pengine usingesema siasa ni sehemu ya dhambi hivyo watumishi wa Mungu hawatakiwi kuhusika.Amani.
Hakuna asiyejua km ndani ya dini kunakipengele cha siasa.ila kwa siasa za kiafrika ikiwemo na tz hazishabiani na dini,kwsbb viongozi wengi Wa siasa matendo yako ni tofauti na maelekezo ya dini .ninachozungumzia hapa simlengi mch.rwakatare peke yk ila ni kwa wote.
 
Kunta, hii habari kwamba alikuwa hataki kuitikia wito wa mahakama, umeipata wapi? Kwa hiyo amri ya kuvunjwa nyumba ni ruling halali ya mahakama? Na nini maoni yako kuhusu Stop Order ya mahakama waliyopelekewa wavunjaji waka i dis honor?

kipengele hiki umekisoma?

Nyumba hizo zilizokuwa katika Kitalu namba 314 chenye mgogoro wa umiliki, zilikuwa zinajengwa na John kwa kasi bila kujali kuwa kulikuwa na amri ya Baraza la Ardhi ya kuzuia ujenzi huo hadi mgogoro uliohusu eneo hilo utakapotatuliwa.

Kuna haja ya kuzungumzia amri iliyokuwa dis honoured wakati wao ndio wa kwanza ku dis honour amri za mahakama?
 
Kabla hujaamua kushangaa, ni vyema ukaelewa kwanza.

Madawa ya kulevya hayaongezi uchumi kwa sababu, japo wanajenga majumba, lakini athari za madawa ni kuua taifa. Kwamba wanaua afya za mili na akili kwa nguvu kazi na hiyvo kuathiri uzalishaji ambacho ndicho kiini cha maendeleo ya uchumi wa taifa. Na nyumba kama hazitumiki productively, si kitu kinachokuza uchumi wa taifa.

Pili usichanganye hoja. Hapa hatujadili chanzo cha mapato kwamba kavunjiwa nyumba kwa sababu amepata fedha kwa vyanzo haramu, kiasi cha kulinganisha na wanaojenga kwa mapato ya madawa ya kulevya.

Tatu, hao wahalifu wa madawa ya kulevya, hatuwezi kuwakomesha kwa kuwavunjia nyumba kama unavyoonekana kuelewa. KIla kosa liwe addressed kama lilivyo na ndivyvo sheria ilivyo.

Kosa la kumdhurum mjane, linasemwa leo, lakini siku za nyuma kulikuwa na taarifa amejenga katika eneo lisiloruhusiwa na hivyo kaharibu mazingira. ( Huyo mjane ndiye angerehusiwa kujenga asiharibu mazingira ama anamiliki eneo lile kwa matumizi gani? Mimi na wewe hatuna jibu kwa sasa). Ninachohitaji kionekane ni namna gani kunaweza kuwa na namna ya utafutwaji mtu hapa.

HOJA KUU, SIONGELEI UHALALI WA UMILIKI WA ENEO LILE. KILICHONISHANGAZA, NI KUONA WATU WANAVUNJA SHERIA NA SISI TUNASHANGILIA KWAMBA HAKI IMETENDEKA. HIYO HAKI KAIAMUA NANI?

NI DHAHIRI KWAMBA KULIKUWA NA MAAMUZI YA KISHERIA YALIYOASISI UVUNJWAJI WA NYUMBA ZILE. KINACHONIPA SHIDA NI ILE KUSEMA NYUMBA ZILE ZILIENDELEA KUVUNJWA HATA BAADA YA KUWASILISHA STOP ORDER KUTOKA MAHAKAMANI.

SHERIA MSUMEMONO, TUNAYOISHANGILIA INATAKA BAADA YA HIZO STOP ORDER KUWASILISHWA, ILITAKIWA KILA KITU KISIMAME, WAENDE MAHAKAMANI KUENDELEA NA MCHAKATO WA KUPATIKANA KWA HAKI. KUENDELEA NA EXECUTION WAKATI MAHAKAMA, IMEAGIZA WASIFANYE NI UVUNJAJI WA SHERIA!. SIJUI KAMA UMEELEWA.
Endelea kuchanganyikiwa tu, jengo lililokuwa limejengwa kinyume cha sheria na linaloharibu mazingira lipo na kesi bado inaendelea, na kesi hiyo yeye ndo kaenda kuishtaki jamhuri ya Tanzania. Suala la dawa za kulevya kwani mchungaji hakusemwa sana kuhusu kubeba mzigo kwa kutumia vitoto vyetu kwa kisingizio kuwa vimepewa trip ya kishule. Amkeni waTZ mmelela usingizi wa pono sana
 
Hapa ndipo ninapoipendea serikali yetu, haijali cheo, hadhi wa fedha za mtu linapokuja suala la kufuata sheria!
Upo dunia Gani Ndugu yangu huo ni uonevu tu!! Dar es salaam yote Squatter iweje Hizo tu ndio zivunjwe?
 
dah kwani ilikua impromptu? hata wangeokoa mabati jamani, hao mainjinia hata sio wachumi wangemwacha aokoe japo mali kidogo.
 
Subiri atakavyoilaani CCM kwenye kanisa lake la Mlima wa moto. Baadaye wazee aliowaandaa watawatapeli waamini ambao hawana hata vibanda wamchangie mama mchungaji kiongozi,kwa imani kuwa utakachotoa kitaongezeka 1000×. Kama Gwajima aliweza kuchangisha 9 mil kwa siku moja kwa ajili ya Mbasha(Mrs), sijui kwa mkurugenzi mwenyewe. Kweli hizi imani....
 
We ndio mbururula wa kwanza Tanganyika. Je kama hataki kuuza. Mali ni yake huyu mama mjane. Hakuna anayeweza kusemama lolote hata jamuhuri.


The King.

Unaelewa maana ya Win win situation kama nilivyosema?

win-win
| Definition | Thesaurus | Translations
Also found in: Acronyms, Wikipedia
win-win (w n w n )
adj.
Of or being a situation in which the outcome
benefits each of two often opposing groups.

~~~~~~
Hapa tupo katika lengo la kujenga,kutoa ushauri positive,mie najua gharama za ujenzi,najua uchungu wa ardhi,kumpoka mjane kiwanja sio vizuri pia kubomoa nyumba kisa uvamizi nayo haijakaa vizuri kama mama hataki kuuza basi alipe 800m ya nyumba alizotumia rwakatare kujenga kama hana basi wauze mama mjane apate chake,rwakatare apte 800m yake na serikali ilambe kodi hiyo ndio win win situation,usiwe mtu wa kubwabwaja toa michango ya kujenga!!!
 
Hats angeandika LA nani uchungaji gani huo unavamia viwanja vya watu he bibilia ndio inavyosema?
 
Ujuwe pia wachungaji wengine hawapo kwa ajili ya waamini wapo kimasilahi yao zaidi
 
Kongozi ukisema hivyo, hata hizi habari zote tunazozijadili hapa, tumezipata mtandani na ndiyo msingi wa majadilian.

Vinginevyo, nisingeweka neno kwa mjadala ambao facts zake ni za koubuni kutoka katika hisia za watu.

Kama unachanzo kingine kizuri kinachobainisha kwamba hapana court proceedings zinazoendelea juu ya suala hili na kwamba hakuna stop order iliyowasilishwa, unaweza kutuwekea hapa. Lasivyo siwezi kujadili hisia na thoughtful wishes.

Weka chanzo cha habari kwamba mama Rwak. alikataa kufika mahakamani na kesi ikaamuliwa upande mmoja.

Hata hivyo kwa ufahamu wako unamaanisha mahakama ikishatoa uamuzi hakuna review? Na kwamba haiwezi kutoa stop order ili ifanye review zaidi?

Kwa nini unasema siwezi kuhoji authority iliyotoa uamuzi wakati imeandikwa bayana kwamba ni uamuzi wa manispaa ya kinondoni na wizara ya ardhi. Ina maana wewe hujui mipaka kati ya wizara, manispaa na mahakama? Napata shida kuelewa unamaanisha nini kwamba authorities are unquestionable!. Lol,

Nikutakie shule njema.

Nimeshangaa kidogo unavyonitakia shule njema (sijui una maanisha nini?) pili, nadhani umeisoma juu juu post yangu maana ulichojibu sicho nilichokiandika kabisa. Hakuna sehemu nimesema huwezi kuhoji authority (iwe mahakama, wizara au manispaa) ila nimekwambia wewe kuwa kama huna details za court jugdement sidhani kama unaweza kusema kwa authority kuwa hili swala liliamuliwa in favour ya Lwakatare. It's fine umesema tuna argue on basis ya taarifa za gazeti. Lakini ni taarifa za gazeti hili hili ndo limeandika kuwa huyu mama yeye ndo alizuiwa kwa amri ya Baraza la Ardhi asiendelee na ujenzi wowote. Kilichoandikwa ni kuwa kesi ipo mahakamani na hiyo stop order sijui mwenzetu umeitoa wapi. Ndo maana tunakuuliza kama upo jirani na mgogoro huu na una hizo taarifa za ziada ziweke hapa. Unless, naona umeamua kumtetea mvunjaji wa sheria. Inawezekana una maslahi naye.
 
Usipokuwa na uwezo wa kuchambua hoja, utakufa kwa chuki. Madawa ya kulevya na uvunjaji wa nyumba vinahusianaje hapa?

Kwa heri bwana.

Endelea kuchanganyikiwa tu, jengo lililokuwa limejengwa kinyume cha sheria na linaloharibu mazingira lipo na kesi bado inaendelea, na kesi hiyo yeye ndo kaenda kuishtaki jamhuri ya Tanzania. Suala la dawa za kulevya kwani mchungaji hakusemwa sana kuhusu kubeba mzigo kwa kutumia vitoto vyetu kwa kisingizio kuwa vimepewa trip ya kishule. Amkeni waTZ mmelela usingizi wa pono sana
 
Kwa ufahamu huo kwamba siasa za Africa zimetawaliwa na giza na wanasiasa wameacha siasa sahihi na kufanya ushetani, unapenda waachiwe ili tuendelee kuwa na siasa zisizotija? Unaelewa umuhimu za siasa katika maisha yako ya kila siku?

Hakuna asiyejua km ndani ya dini kunakipengele cha siasa.ila kwa siasa za kiafrika ikiwemo na tz hazishabiani na dini,kwsbb viongozi wengi Wa siasa matendo yako ni tofauti na maelekezo ya dini .ninachozungumzia hapa simlengi mch.rwakatare peke yk ila ni kwa wote.
 
Ubishi wa kisheria utatufikisha mbali kwa sababu tafasiri yako, shria uliyonukuu na kilichofanyika havifanani. Hatujaaambiwa alipwewa notice ya kuondoka na vitu vyake. Kilichosemwa ni amri ya kuvunja. Usiwe mbishi kama hujaelewa. Unajua sheria siku zote haifuati utashi wako bali huangalia haki. Fahamu commissioner hayuko juu ya sheria, na anapaswa kuifuata siyo sheria imfuate.

Wengi hapa wanafurahia na kuchukua sehemu kwa ajili ya wivu wala si kwa hoja dhidi ya mama rakwatare.


Mkuu hebu acha kubisha vitu vilivyo wazi bana. Hapa unatumia ubishi tu. Lakini kwa kukusaidia The Land Act of 1999, part XIV (Miscellaneous) kifungu 175, kinaongelea unlawful occupation of land. Ibara ya 2, inampa commissioner mamlaka ya kumsave mvamizi notice tu tena hata ya mdomo (ilimradi iwe kwa lugha atayoielewa) ya kuthibitisha umiliki na asipofanya hivyo anamwamuru atoke na mali zake iwe ni majengo, mazao nk. Tena imesisitiza "within anytime and subject to any conditions"! Zaidi hata kanuni zilizofuatia land Act zipo wazi kwenye hili. Commissioner hahitaji kufungua kesi eti kisa wewe umejenga bila permit.
 
Haya ni mengine sasa! Kwanza si mjane. Sheria gani inazuia kumaliza mgogor mezani hata kama mali ni yake? Na wewe ni mburura vile vile.

We ndio mbururula wa kwanza Tanganyika. Je kama hataki kuuza. Mali ni yake huyu mama mjane. Hakuna anayeweza kusemama lolote hata jamuhuri.


The King.
 
Back
Top Bottom