Mch. Msigwa 'afyatuka' Bungeni... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mch. Msigwa 'afyatuka' Bungeni...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by VUTA-NKUVUTE, Jul 5, 2012.

 1. VUTA-NKUVUTE

  VUTA-NKUVUTE JF-Expert Member

  #1
  Jul 5, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 5,869
  Likes Received: 6,608
  Trophy Points: 280
  Ingawa ni maelezo marefu,si vibaya tukajikumbusha mambo haya kutoka kwenye Hansard za MKUTANO WA NANE

  Kikao cha Tano – Tarehe 19 Juni, 2012

  VIDEO:
  MHE. MCH. PETER S. MSIGWA:

  Mheshimiwa Mwenyekiti, nikushukuru sana kwa kunipa nafasi.Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kuanza kwa nukuuambayo naipenda sana inayosema:-


  "Insanity is keeping doing the same thing in the same way and expecting different result"

  ambazo zinalikabili taifa lakini kwa bahati mbaya nimeona yaani uwendawazimu nikufanya jambo lilelile kwa njia ileile huku ukitegemea matokeo tofauti.

  Mheshimiwa Mwenyekiti, mwanafalsafa Albert Einstein anasema:-"Problems can not be solved by the same level of thinking that creates them". Ndugu zangu, kabla sijawa Mbunge kama alivyosema kaka yangu Mheshimiwa Akunaay, nilikuwa nawa-admire sana Wabunge wanavyokuwa Bungeni, wakivaa suti, nilikuwa naona hapa ni mahali ambapo tuna reason, mahali ambapo tuna question na mahali ambapo tunatoka na solutions


  is the opposite, binafsi najisikia vibaya sana. Kama taifa tupohapa, we are dealing na future ya taifa hili, tunashughulika namamia ya maskini wa Tanzania, tunashughulika na barabarambovu za Watanzania, tunashughulika na hospitali mbovu zaWatanzania, halafu tunakuja hapa tunaongea mambo yakhanga!

  Mheshimiwa Mwenyekiti, ukisoma historia, nchi za Ulayakarne ya 14, Marekani na Ulaya na nchi zilizoendelea, zilikuwana fikra na mawazo kama tunavyofanya sasa hivi lakini ilipofikakarne ya 18, inaitwa age of enlightenment, reasoning age, walianza kufikiri, kuhoji na kudadisi. Tunapofika katika karne hiikatika Bunge la Jamhuri la Muungano wa Tanzania,tunapojadili bajeti maana yake tunazo changamotozinazotukabili kama taifa.

  Badala ya kukaa na kujiuliza kwa ninitupo hapa, tunatokaje hapa tulipo, tunaanza kuongeangonjera na maneno ya uswahiliuswahili yaani unafiki, woga,kujipendekeza na kutokujadili mambo ya msingi.


  (Makofi)


  Mheshimiwa Mwenyekiti, najisikia uchungu sana mamiaya wananchi wametuamini tuje tujadili vitu vya maana hapalakini tunakubaliana akili ndogo itawale akili kubwa. JamesMadison mwaka 1822 alisema, "
  knowledge forever will governignorance".

  Tumekubali Bunge hili knowledge ndogo i-governknowledge kubwa, tumekubali ignorance i-govern knowledge,tunalipeleka wapi taifa? Akichangia professor hapa hanatofauti na mtu wa darasa la pili. Huwezi kutofautisha mtumwenye masters na mtu wa darasa la pili, where are we takingthis nation? Watu wametupa kura, tunapoteza fedha zaWatanzania, tumekaa hapa tunaacha kujadili mambo yamsingi kwamba tunawezaje kutoka kwenye matope haya? Karne hiyo ya 18 ninayoisema walipoanza kuhoji, walipoanzakudadisi ndipo mapinduzi ya viwanda yalivyojitokeza, no wonder watu wanaosema ni wataalamu wa uchumi wametufikisha hapa tulipo, if that is the case, haya ndiyo masuala ambayo tunapaswa tuyajadili kama taifa.

  Mheshimiwa Mwenyekiti, bajeti inaonyesha hapa, kitabu cha uchumi cha Mheshimiwa Wassira kwamba deni limekuwa shilingi trilioni 20. Ukigawanya ni kama karibu kila Mtanzania anadaiwa shilingi laki nne na themanini na zaidi, hata mimba inadaiwa, ndiyo taifa tulipofika hapa sasa hivi.

  Pianinashangaa katika mpango wake wa bajeti taifa hili kamatunafuatilia na tunakwenda na takwimu, mdogo wangu amezungumza hapa kwamba tunatumia takwimu za nyuma, unawezaje kupanga mambo na takwimu za nyuma?

  Leo hii katika taifa hili 44.2% ni watoto walio chini ya miaka 15 maanayake hawa ni consumers, wanakula zaidi hawa-produce, wakoshuleni na wanao-produce katika nchi hii ni wachache sanakuliko wanaokula ukijumlisha na wazee tuna mzigo mkubwasana. (Makofi)  Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, kwa utaratibu wabajeti tulio nao hapa,
  there is no way kama tunaweza tukafanya maendeleo, it will take ages kubadilisha taifa hili kama tunaendelea na ngonjera za namna hii na kuruhusu akili ndogo itawale akili kubwa.

  Watu wenye akili kubwawanaweka akili zao mfukoni kwa sababu ya ushabiki wakivyama badala ya kukaa tuka-discuss namna ya kutatuamatatizo yetu.Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa kama wanao-consume niwengi na wanao-produce ni wachache maana yake nini?

  Tutaendelea kuomba fedha nje na kukopa fedha nje ilituwalishe kwa sababu ni wajibu wa Serikali kusomesha watoto,ni wajibu wa Taifa kuhakikisha watoto wanavaa na kusomashule nzuri lakini mpango mzima wa uchumi uko kimya,hauzungumzi.

  Hapa watu wasomi ambao tupo 350 taifalimetuamini tukae hapa tunatakiwa tujihoji, ndiyo maananimesema problems can not be solved by the same level ofthinking that created them, you guys you are tired!

  Kwasababu hamuwezi kutetea matatizo haya, mmetuwekakwenye mess ninyi wenyewe, ni lazima akili ya juu zaidi iwezekutatua, ni principle hii yaani huwezi kubadilisha that is theprinciple, iwe ni mwanamahesabu na nikiunganisha na insanityis keeping doing the same thing in the same way andexpecting different results and this is what we are doing.  Tunafanya hayohayo kila mwaka bajeti ya namna hiyohiyo.Ukienda kwenye elimu ni matatizo, ukienda kwenye kilimo nimatatizo, ukienda kwenye afya ni matatizo mwaka baada yamwaka ni matatizo yaleyale,
  why can't we think a little bitmore?

  We can't stretch our brain a little bit more kama taifa?(Makofi)  Mheshimiwa Mwenyekiti, nimeongea na watu wengineambao ni ma-professor wanasema mara nyingi wakitoaushauri wa kitaalamu, Serikali hamsikilizi na inawezekanawanakaa watu wachache, wanajifungia halafu wanatoamaamuzi kwa sababu wanajua mambo ni yaleyale, business asusual. Ndugu zangu, where are we going? Where are weheading?

  165

  Mheshimiwa Mwenyekiti, takwimu zinaonyesha tenakaribu 42% ya watoto wanaozaliwa wanadumaa,


  they can notthink properly, they can not question, they can not ask.

  Ubongo aliotupa Mungu ni lazima uwestretched ili uwezekuchambua kwani tumeumbwa ili tutatue matatizo hapaduniani na siyo tu-create matatizo. Tulipokuja hapa Bungenitunatakiwa tu-solve problems, Bunge hili naliomba liwe Bungela kimapinduzi, tu-change namna ya kufikiri na tu-change


  namna ya kufanya vitu na wengine wanapata taabu hapakwa sababu tumezoea Bunge la chama kimoja.

  Tuna mfumona traditional ya chama kimoja cha zamani, ulimwengu umechange
  halafu tumesimama mahali pamoja hatuendi naulimwengu unavyokwenda. Maendeleo duniani yamekuja kwakuwa na mawazo tofauti yanayopingana, badala yakutuzomea mtusikilize, huu ndiyo wajibu wetu. Mimi kama opposition

  siwezi kusifia bali nakukosoa ili ufanye kazi yako vizuriili na wewe utimize wajibu wako. (Makofi)  Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa deni kama hili kila mwakalinaongezeka halafu tunakaa hapa tunasema Serikali ya CCMitaendelea kutawala, so what? Ili iweje? Kwa sababu lengo laSerikali kuwepo ni kutatua matatizo ili tuhakikishe tuna-improve maisha ya watu lakini watu kwa sababu wanalinda vyeo, kunammoja amesema Mchungaji, lakini nitasema tu hata kamamtasema au kunitoa nje ya Bunge lakini kama ukweli unakosewa


  I will speak out kwa sababu hiyo ndiyo kazi ya Wachungaji vilevile. Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna Mbunge mmoja alishaurihapa tuombewe lakini sioni hata theory ya uchumi inayosemakama unataka kutatua matatizo ya uchumi eti ufanyemaombi, ninashangaa huyu amepata wapi hilo?

  As aTheologians hata Paul anasema asiyefanya kazi na asile siyo aombewe, unamnyima chakula lakini yeye anasema watu waombewe. Mimi kama Mchungaji naombea wazinzi, wanaofumaniwa na wake za watu, ndiyo tunawaombea, mimi kama Mchungaji tunawaombea wenye mapepo na hii ni
  principle tuna apply, una-consumers wengi lakini producers wachache maana yake you have to produce more tafuta njiaza ku-produce zaidi, we don't pray for this, we don't have topray for this. (Makofi)


  Mheshimiwa Mwenyekiti, halafu tumekaa hapatumezalisha taifa la watu waoga, wanafiki nawanajipendekezapendekeza, mimi sijaja hapa kwa kupewafedha bali wananchi wa Iringawamenichangua, wananiaminina ninajua wananiunga mkono, wananisikiliza. Sasa sihitajikujipendekeza nitaeleza ukweli as a nation tupo kwenyematatizo. Wehave to address this problems lakini siyo tunakujahapa tunaweka ngonjera maneno ya khanga halafu watumnawapigia makofi, tunalipeleka wapi taifa hili? (Makofi)


  Mheshimiwa Mwenyekiti, ninajisikia uchungu, naomba

  niachie hapo. Ahsante sana. (Makofi)
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 2. Ndekirhepva

  Ndekirhepva JF-Expert Member

  #2
  Jul 5, 2012
  Joined: May 18, 2012
  Messages: 377
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  jamani natamani ningepata ile video clip yake ndio ina msisimko zaidi, nisikie na zile" so what"?
  mwenye nayo atuwekee plz plz
   
 3. D

  DOMA JF-Expert Member

  #3
  Jul 5, 2012
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 946
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 45
  Ah imetulia sana hii. Viva msigwa
   
 4. m

  mob JF-Expert Member

  #4
  Jul 5, 2012
  Joined: Dec 4, 2009
  Messages: 2,027
  Likes Received: 510
  Trophy Points: 280
  Iko youtube mkuu
   
 5. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #5
  Jul 5, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,461
  Likes Received: 5,846
  Trophy Points: 280
 6. Tume ya Katiba

  Tume ya Katiba JF-Expert Member

  #6
  Jul 5, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,892
  Likes Received: 730
  Trophy Points: 280
  Mchungaji msigwa(aka mbunge muongozo), aache nidhamu mbovu bungeni, na nitamshitaki kwa wananchi wa jimbo la iringa -By Naibu spika Job Ndugai
   
 7. Lyimo

  Lyimo JF-Expert Member

  #7
  Jul 5, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,828
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
 8. L

  Luiz JF-Expert Member

  #8
  Jul 5, 2012
  Joined: May 23, 2011
  Messages: 342
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kweli huyu jamaa ananondo za kufa mtu.
   
 9. mtanzaniahai

  mtanzaniahai Member

  #9
  Jul 5, 2012
  Joined: Oct 3, 2010
  Messages: 21
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  I appreciate this extreemly good speech; Nadhani tukiwa na wabunge wenye mawazo kama haya tutaifikisha mbali nchi yetu.. Tujifunze yanayoendelea kwenye nchi ya UK ambapo wabunge walim-question CEO and others management staffs of Barclays Bank kwa benki yao ku-misuse LIBOR. Hivi hapa kwetu tukianza kuwahoji watendaji wa taasisi muhimu za umma wanapokosea au wasipowajika profesionally taasisi zao zikavurunda au nchi ikapata hasara; itakuwaje?? cha kuuliza Je Bunge letu halitaanza tena UCHAMA na mipasho??? Je wabunge wetu walio bungeni, bunge ambalo is one of the parliament with a lot of Professors, Doctors na wasomi wengine wengi in developing countries je are you focusing this?

  Maslahi ya nchi yapewe kipaumbele kwanza na siasa later..

  Nawakilisha wadau..
   
 10. Graph Theory

  Graph Theory JF-Expert Member

  #10
  Jul 5, 2012
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 3,804
  Likes Received: 1,118
  Trophy Points: 280
  Sikubahatika kumsikia ila kwa kusoma hapa nimemsikia tena mstari hadi mstari.
  Kila atajaye jina la Yesu, na auache uovu.
   
 11. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #11
  Jul 5, 2012
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  huyu baba ana akili sana..mweeee.sasa hawa ndo wanatakiwa kuwa mawaziri..sio akina wassira...
   
 12. Saharavoice

  Saharavoice JF-Expert Member

  #12
  Jul 5, 2012
  Joined: Aug 30, 2007
  Messages: 2,644
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Hizo ndizo ngonjera zenyewe mr. gamba.
  Msome tena Mh. Msigwa pengine itakusaidia kubadilika, maana elimu uliyonayo ni ya kujipendekeza pendekeza tu...
   
 13. S

  Starn JF-Expert Member

  #13
  Jul 5, 2012
  Joined: Oct 10, 2011
  Messages: 400
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Kazi aliyotumwa kuifanya hapa duniani imemshinda sasa kajikuta yupo sehemu ambayo hakutakiwa kuwepo. Anaanza kuongea utumbo. ni rahisi binadamu kumsikiliza kiongozi wa dini kuliko viongozi wa nchi, na yeye ameacha kuchunga kondoo kwa kutafuta uongozi wa nchi. Rudi kafanye kazi ya Mungu kaombee wazinzi ili wapate kumrudia Mungu.
   
 14. yutong

  yutong JF-Expert Member

  #14
  Jul 5, 2012
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 1,604
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  haya wekeni na ya mwigulu nchemba tuisome hapo
   
 15. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #15
  Jul 5, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Chakushangaza bado kuna wabunge na watu wengine humu jf wanambeza!
   
 16. yutong

  yutong JF-Expert Member

  #16
  Jul 5, 2012
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 1,604
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Ni baada ya kuona ktk kipindi zaidi ya miaka 40 watu wanasinzia na kulala bungeni na kupitisha bajeti hewa na huku maisha ya watz yakizidi kuporomoka unafikiri afanyaje sasa? Mbona rwakatare hamumsemi? wapeni nafasi kwanza hata hivyo hapa tulipofika ni kwa sababu ya upinzani
   
 17. yutong

  yutong JF-Expert Member

  #17
  Jul 5, 2012
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 1,604
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Sisi tuanendelea na maneno yaleyale tu tu ya mbayuwayu, mara waombewe sasa mtu kama huyu anainput gani kwa taifa?
   
 18. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #18
  Jul 5, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Msigwa = wabunge 200 wa magamba!
   
 19. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #19
  Jul 5, 2012
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Sad comment. Aliyemwita ndiye anajua amwemwita kwa kusudi lipi. Biblia inaniambia sote tu watumishi wa Mungu, hata hapo Bungeni kondoo ni wengi.
   
 20. Mimibaba

  Mimibaba JF-Expert Member

  #20
  Jul 5, 2012
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 4,566
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Ameitika wito wakuhudumia kondoo (Chama cha Mabwepande) waliopotea. Aliowatumikia katika nyumba za Mungu waqnaendelea vizuri. Imesemwa dawa hupewa mgojwa si mzima
   
Loading...