Mch. Msigwa 'afyatuka' Bungeni...

Mch. Msigwa 'afyatuka' Bungeni...

kazi aliyotumwa kuifanya hapa duniani imemshinda sasa kajikuta yupo sehemu ambayo hakutakiwa kuwepo. Anaanza kuongea utumbo. Ni rahisi binadamu kumsikiliza kiongozi wa dini kuliko viongozi wa nchi, na yeye ameacha kuchunga kondoo kwa kutafuta uongozi wa nchi. Rudi kafanye kazi ya mungu kaombee wazinzi ili wapate kumrudia mungu.

tunawafahamu wote wapinga ukweli ni wa ccm maana inawauma sana kuona mbunge wa upinzani akimwaga nondo za nguvu lakini ukweli unabaki palepale hivi maji marefu au komba au lusinde watasema nini mbele ya jamii zaidi ya mitusi na kejeli kwa watanzania? Jiulize hao viongozi wako wa ccm wanafanya kazi zao walizosomea? Jk mwanajeshi,huyo bilal ni mtaalamu wanyuklia, mizengo mwanasheria,komba muimba kwaya, maji marefu mganga wa kienyeji, huo ni mfano mdogo tu usikurupuke kuongea maneno mbofumbofu.
 
Kazi aliyotumwa kuifanya hapa duniani imemshinda sasa kajikuta yupo sehemu ambayo hakutakiwa kuwepo. Anaanza kuongea utumbo. ni rahisi binadamu kumsikiliza kiongozi wa dini kuliko viongozi wa nchi, na yeye ameacha kuchunga kondoo kwa kutafuta uongozi wa nchi. Rudi kafanye kazi ya Mungu kaombee wazinzi ili wapate kumrudia Mungu.

Huyo ndio Mchungaji wa kweli, aliyepambana na kuingia bungeni kwenda kuwaambia wanasiasa ukweli na kuwatetea wanyonge sio kama Mch Mama Lwakatare anayesubiri kusema ndioooooooo!! Acha ujinga!!
 
Kwa kweli inasisimua.sikubahatika kuisikiliza.inasikitisha ujumbe kama huu unapuuzwa na matokeo yake utumbo wa kina mwigulu unajadiliwa zaidi na kuacha mambo ya muhimu kama haya.Nchi hii tunaipeleka wapi?

Utashangaa wabunge wa CCM walivyowapumbavu wakamchangia na hela eti kuichambua bajeti ya upinzani kumbe wanamchangia hela za kwenda kuharibu ndoa za watu, shame on those ******!!!
 
Kazi aliyotumwa kuifanya hapa duniani imemshinda sasa kajikuta yupo sehemu ambayo hakutakiwa kuwepo. Anaanza kuongea utumbo. ni rahisi binadamu kumsikiliza kiongozi wa dini kuliko viongozi wa nchi, na yeye ameacha kuchunga kondoo kwa kutafuta uongozi wa nchi. Rudi kafanye kazi ya Mungu kaombee wazinzi ili wapate kumrudia Mungu.

Wewe Starn ni mpumbavu na huna akili kabisaaa. You dont understand what Msigwa is saying. Hata baba yako aliyekuzaa naye hana akili kama wewe. You a stupid pig and it seems you are living like a pig and you will die like donkey. watu wanatoa comment za maana wewe unaongea utumbo umeniudhi sana wewe **** **** nina zako weee.
 
Nimefurahia linkage ya kipindi hiki aliyotoa na age of reasoning and enlightment . Mabadiliko ya kifikra ya enzi hizo ndo yalipelekea mapinduzi ya Ufaransa. Fukuto lililokuwepo Ufaransa enzi hizo ndilo lililopo hapa nchini saa hizi, kweli naogopa. Serikali hii ijirekebishe naionea huruma. Aliyofanyiwa mfalme Louis xvi na mkewe Antonente nahofia viongozi wa nchi kufanyiwa tena na watoto wa walalahoi.
 
Ukiisoma hii hotuba na au kumsikiliza Msigwa, yaani unaweza TOA machozi .....!!!
Eeeee Mungu mwenye REHEMA, sisi wana wa TANZANIA tunahitaji watu kama hawa na si kama wale wengine.
 
shallom mtumishi wa MUNGU, Mch. P Msigwa.MUNGU AKUPE HEKIMA NA ROHO YA HURUMA ZAIDI KWA WATANZANIA WENZAKO.AMENI
 
Chakushangaza bado kuna wabunge na watu wengine humu jf wanambeza!

Kafulila alisema kuna baadhi ya viongozi wetu ambao uwezo wao wa kufikiria unaishia kwenye ngazi ya familia. Mkuu nadhani hao wanaombeza Msigwa, ndo type ya wale aliowasema Kafulila
 
Wewe Starn ni mpumbavu na huna akili kabisaaa. You dont understand what Msigwa is saying. Hata baba yako aliyekuzaa naye hana akili kama wewe. You a stupid pig and it seems you are living like a pig and you will die like donkey. watu wanatoa comment za maana wewe unaongea utumbo umeniudhi sana wewe **** **** nina zako weee.
HAhaha hahaha si unaoa jinsi ustaarabu ulivyowashinda walio pale bungeni na nyinyi wote akili zenu ni matope badala ya kutetea ili nipate kukuelewa kwanini unamtete mch, unaanza kuleta matusi. matusi hayato kusaidia kabisa kuwa mstaarabu.
 
Itashangaza sana mtu akiongea ukweli akaonekana hana akili. kuna watu wenye akili za kipumbavu ambao
bado wanalaumu Msigwa aliyo yaongea. huu ni wakati wa kutafakali sisi wananchi
 
Mchungaji msigwa(aka mbunge muongozo), aache nidhamu mbovu bungeni, na nitamshitaki kwa wananchi wa jimbo la iringa -By Naibu spika Job Ndugai

Kazi yake ni kuwaombea watu kama nyie, alisema Msigwa!
 
Kazi aliyotumwa kuifanya hapa duniani imemshinda sasa kajikuta yupo sehemu ambayo hakutakiwa kuwepo. Anaanza kuongea utumbo. ni rahisi binadamu kumsikiliza kiongozi wa dini kuliko viongozi wa nchi, na yeye ameacha kuchunga kondoo kwa kutafuta uongozi wa nchi. Rudi kafanye kazi ya Mungu kaombee wazinzi ili wapate kumrudia Mungu.

hvi ulishawah kuskia kuna chuo cha ubunge? Mle si kila mtu ana taaluma yake?tukisema kila mtu arud kwenye utaalamu wake bunge litabaki tupu, mbona Ayman al Zawahir ni daktar kitaaluma ila anaongoza Al Qaida kwa sasa? Kwa kifupi umeongea pumba ndugu, kama alivosema msigwa jaribu kufikiri a bit more
 
"if that the case" kamanda huwa ananikosha sana na hii misemo yake
 
haya wekeni na ya mwigulu nchemba tuisome hapo

Hii hapa Mkuu



MHE. MWIGULU L. M. MADELU: Mheshimiwa Mwenyekiti, nikushukuru sana kwa kunipa
nafasi hii ili nizungumze na Watanzania. Awali ya yote, Watanzania wanatakiwa wawe makini
sana na waigizaji. Ukimpata mwigizaji mzuri, unaweza ukalia, kumbe mwenzio anaigiza na hiki
ndicho ambacho kimetokea muda mfupi uliopita hapa. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, tatizo kubwa...
MWENYEKITI: Mheshimiwa, nakuomba ufute neno uigizaji.
WABUNGE FULANI: Aaah!
MHE. MWIGULU L. M. MADELU: Mheshimiwa Mwenyekiti, nafuta kama kuna waigizaji hapa.
MWENYEKITI: Naomba ufute neno uigizaji.
90
MHE. MWIGULU L. M. MADELU: Mheshimiwa Mwenyekiti, nafuta neno uigizaji kama kuna
waigizaji, lakini maana ya kusema hivi ilikuwa ni hii, tatizo linalojitokeza hapa ni kwamba, bajeti
imeandaliwa na wataalam, lakini watu badala ya kuuliza wajue undani wa bajeti, aliyesomea
Sheria za Mambo ya Kichawi na yeye anakuwa mchambuzi wa uchumi, mwenye uzoefu wa
kuendesha disko anakuwa mchambuzi wa uchumi, unawachanganya Watanzania. Sasa uhalisia
ndio huu, mimi ni Mchumi wa Daraja la Kwanza na Mwandamizi wa Benki Kuu ya Tanzania, ngojeni
niwaambie uhalisia wa bajeti. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kwenye Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano,
tunapoongelea 35%, tunajumuisha pamoja na uwekezaji kwenye sekta ya elimu lakini
tunapozungumzia bajeti hii ya leo, sekta ya elimu iko pembeni, fedha zake zimewekwa pembeni,
zile za maendeleo zimewekwa pembeni. Watanzania tuulizane, hivi kweli tunaposomesha
wanafunzi vyuo vikuu, hatuwekezi? Hivi kweli tunapojenga maabara, hatuwekezi? Hivi ni kweli
tunaposomesha vyuo, tunapoandaa Wataalam wa Ugani, tunapoandaa Madaktari, hatuwekezi?
Tulisoma wapi? Hiyo Sheria iliyokuwa inatenga investiment on human capital, ilikuwa ni ya miaka
ya 50 na 60 lakini ukisoma David Roma, ukasoma Waive, ukasoma Mankyu, miaka ya 90, Cop
Douglas Production Function, inatambua human capital kama investiment. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa Mpango wa Maendeleo huu tunaojadili, umejumuisha
investiment on human capital ndio ukapata 35%. Ukienda kwenye bajeti ya mwaka huu,
ukichukua investiment kwenye elimu, uwekezaji tuliouweka kwenye elimu, bajeti ya maendeleo
inaenda 39% kwenda 40%. Mmesoma wapi nyie? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini la pili, ukiingalia kiutaalamu tu bajeti yenyewe, kiutaalamu
tu, dependency ratio, utegemezi bajeti imepungua. Ukiweka na ile mikopo kwa sababu mikopo
nayo ni fedha yetu tutalipa, ukiondoa na ile ya mikopo, utegemezi kwenye bajeti imebaki 6.5%.
Sifa nyingine ya bajeti, ukienda zile fedha zinazoenda kwenye kulipa mishahara, hamna hata senti
moja inayoenda kwenye mishahara, mishahara inalipwa na fedha za ndani. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, hebu muone sasa hili nililolisema ambalo mmesema nilifute, hebu
oneni sasa Bajeti ya Kivuli, wameandika kwamba, kima cha chini kitakuwa 315,000/= hawajui
wanaolipwa kima cha chini ni wangapi, zidisheni mpate hesabu, mimi nitawaambia mwishoni.
Halafu chukueni Walimu muwapandishie mishahara mara 50, chukua Madaktari uwapandishie
mara 50, chukua Manesi uwapandishie mara 50, tafuta jumla yake. Halafu chukua walewale,
makundi matatu haya, uwapandishie mara moja na nusu, bajeti ya matumizi inaenda zaidi ya hii
shilingi bilioni tisa waliyoandika wao. Hii waliyoandika kwenye matumizi ya kawaida inazidi,
ukijumlisha na ile wanayosema kwamba watalipa pensheni kwa wazee, hawajui idadi ya wazee,
ukijumlisha inakuwa zaidi ya shilingi trilioni 15, mmnatumia bajeti ya wapi? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, halafu wanasema...
MBUNGE FULANI: Silly thinking.
MHE. MWIGULU L. M. MADELU: Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi hili nitalirudia tu, halafu
wanasema kujenga, wanasema kupunguza mzigo wa matumizi ya magari. Mwaka jana
Mwenyekiti wao, Mheshimiwa Mbowe, alirudisha gari akisema kwamba, kupunguza matumizi,
akawahadaa Watanzania. Baada ya muda fulani, kumbe alilikataa lile gari kwa sababu
limechakaa, lilikuwa linatumiwa na Kiongozi aliyepita, baada ya muda fulani kachukua
kimyakimya gari lingine analitumia. Amelirudisha kimyakimya hajawaambia Watanzania kama
ameshalichukua. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, hawa watu wanatakiwa kwa kweli Wachamungu wote, mimi
tangia nizaliwe sijawahi kuona Kambi ya Upinzani yenye pepo mtaka vyeo kama hawa hapa.
(Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, wanatakiwa waombewe, watalipeleka Taifa pabaya, mimi
nawaambia Watanzania mkiendelea kushabikia watu ambao haijulikani kama wako normal au
wanatakiwa wawe Mirembe mtapata kiongozi kama Iddi Amini hapa.
91
MBUNGE FULANI: Mwongozo wa Spika!
MBUNGE FULANI: Mwehu huyu!
MBUNGE FULANI: Mwongozo! Anatutukana huyu!
MHE. MWIGULU L. M. MADELU: Nimesema niseme na Watanzania, ngojeni niwaambie,
jambo lingine ambalo wanalolikataa hapa, ngojeni mjue unafiki uko wapi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine wanalolikataa wanaongelea OC kama vile ni
dhambi kubwa kwelikweli, angalieni OC kuna nini, OC Serikali imetenga shilingi bilioni 140 kupeleka
vijana JKT, hivi kweli hiyo ni dhambi kupeleka vijana JKT. (Makofi)
MBUNGE FULANI: Waambie!
MHE. MWIGULU L. M. MADELU: Serikali imetenga OC kwenda kwenye Tume ikakusanye
maoni ya Katiba Mpya, mnataka Katiba Mpya hamtaki tuweke bajeti, mnataka Katiba mpya kwa
kutumia fedha gani.
MBUNGE FULANI: Mwongozo wa Spika!
MHE. MWIGULU L. M. MADELU: Serikali imetenga fedha kwenye OC kwa ajili ya sensa,
mnataka sense, hamtaki tuweke bajeti. Serikali imetenga fedha kwenye OC kwa ajili ya fidia za
watu wanaondolewa kwenye maeneo kupisha miradi ya maendeleo, mnataka zisiwekwe, wale
watu mtawapatia hela gani mnapowaondoa pale? Serikali imetenga fedha kwenye OC kwa ajili
ya chakula, wanafunzi, wafungwa, wagonjwa mnataka ziondoke mtawapa nini? (Makofi)
MBUNGE FULANI: Mwongozo wa Spika!
MHE. MWIGULU L. M. MADELU: Mimi sijawahi kuona Bajeti Kivuli ya aina hii, this is concisely
and precisely rubbish. (Makofi)
MWENYEKITI: Samahani kaa chini, Mheshimiwa naomba ukae.
MHE. MWIGULU L. M. MADELU: Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja.
(Kicheko/Makofi/Vigelegele)
MWENYEKITI: Ngojea Mheshimiwa Mwigulu, order in the House, Mheshimiwa Mwigulu
naomba ufute neno pepo kwa sababu ni kinyume…
(Hapa baadhi ya Wabunge walizomea)
MWENYEKITI: Order in the House.
MBUNGE FULANI: Mbona walipotaja Mungu mpya hukusema?
MWENYEKITI: Order in the House.
MBUNGE FULANI: Afute.
MWENYEKITI: Order in the House, naomba ufute neno pepo halafu tuendelee.
MBUNGE FULANI: Mwongozo!
MWENYEKITI: Mheshimiwa Mwigulu futa neno pepo tuendelee.
MBUNGE FULANI: Mwongozo wa Spika!
92
MHE. MWIGULU L. M. MADELU: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa humu ndani nafuta lakini watu
wa aina hiyo wakaombewe, nafuta neno hilo. (Makofi)
MBUNGE FULANI: Mwongozo wa Spika.
MWENYEKITI: Naomba tuendelee.
MBUNGE FULANI: Kuhusu utaratibu!
MWENYEKITI: Naomba tuendelee, sasa namwita Mheshimiwa Ahmed Ally Salum na
Mheshimiwa Amina Clement ajiandae na atafuatia Mheshimiwa Komba. Yupo au hayupo?
 
Maneno haya aliyosema ni kweli kabisa yatupasa tujithathimini kama taifa, tuangalie tulipotoka, tulipo na tunapoelekea bila kuweka parties ideology mbele, siku zote Tanzania yapaswa kuwa ya kwanza ndo mambo mengine yafuate, viva Mh. Msigwa
 
Mhe. kwa sasa amebadilika na anajipanga kwenye hoja zake, hususan hoja yake ya leo kuhusu Wizara ya Ujenzi.
 
Yap yap ni kweli kabisa haiwezekani akili ndogo iongoze akili kubwa halafu uone maendeleo. Mch Msigwa mwaga nondo, mpaka 2015 lazima watanzania watakuwa wameamka na magamba yote lazima tuyapige chali. Hapana akili ndogo kuongoza akili kubwa mana ni sawa na kipofu kuongoza lazima mtadumbukia wote shimoni. shame on you magambas
 
Kwa wale ambao tuanweza kusikiliza mpate hapa

 
Last edited by a moderator:
Mhe. Msigwa(Rev), umenena,umesikika na umeeleweka. Hongera sana.

Hii ni kuthibitisha kwamba CHADEMA kina wabunge vichwa ambao wako makini sana.Najua wabunge mazezeta wa CCM kina Mwigulu,Bi Mkora Manyanya,Kapteni Komba a.k.a Mkata mauno,Wassira a.k.a Tyson wa usingizi n.k wanaweza wakabeza sana ukweli huu lakini haiwasaidii!

Kapteni Komba a.k.a. mkato mauno juzi alibwatuka na kusema wabunge wote wa upinzani ni vichaa wakapimwe akili Mirembe, sasa basi swali linakuja kwake Komba na majuha wenzake wa CCM, WA KUPIMWA AKILI HAPA NI NANI KATI YA KOMBA NA MHE.MSIGWA???Ni nani anayeongea points zenye mashiko?

Jibu mnalo.
 
Back
Top Bottom