MC Chitanda ni tapeli?

Yeboyebo,

Nakubaliana na wewe kuwa watu wasidharau kazi za wengine. Kama kuna makosa ya kimkataba hayo mliingia wenyewe na kama kuna breach yeyote sheria ichukue mkondo wake.

Kwa ujumla, kuna mdau amezungumzia suala muhimu kabisa la kulipa kodi. Nadhani kuna kazi za aina hii hii ambazo zinawaingizia watu pesa nyingi tu na hawalipi kodi. Tunaokatwa kodi ni akina sisi wenye kamshahara ka TGS D ka laki 2.

Kwa kifupi serikali na jamii yetu ni ya ajabu sana.
 
ma mc wengine wanachelewa unawapigia simu wanakuambia kuna foleni...foleni my *** kwani ndio ameijua leo na ina maana hakuwa na taarifa, kwa kweli wanakupa hasira...kama huyu makassy nusura tumtwange siku moja.
 
Jamani nimesoma threads zote kuhusu MC - mimi NAPENDA SANA KUWA MC na ndio najipanga kuingia kwenye fani hiyo - kama part time (apart from my permanent employment) nilishaongoza kasherehe kadogo ila sio kama MC - kama msemaji na nikashangaa watu walikuwa impressed sana wakasema inabidi niendeleze kipaji - yoyote anayejua kidogo jinsi ya kujipanga nitashukuru akinielimisha - hasa yale maneno mazuri ya hekima - wanayapata wapi? from books, news etc. vichekesho je? ASANTENI
 
Kijana hii kauli imetulia. Kwa kweli hata mimi nilishaamua...ikitokea hiyo harusi ikawepo..MC asahau pesa yangu. I agree..ni vema kutafuta mtu anayeweza kuchangamsha ukumbi kwa kutoa utani wenye message..Lakini mbona watu wa kawaida wanaweza? Lakini bongo bwana..harusi zimeshakuwa shughuli pevu inayohitaji substantial investment of resources..wanaogopesha vijana kuoa sasa..unakuta mdada/mkaka anataka harusi bab kubwa..kijana ndo akina Masanja hapa..choka mbaya.....Inabidi uingie mitini tuu...

Ndo maana nimemuomba Fundi aniambie anapatikana vipi. Fundi hope hutaingia mitini na kumtuma mwakilishi....I dont want "tired and recycled packaged jokes" za akina Chitanda, chumvi chumvi et al!

Mkuu Masanja. I am honoured kwa kunipa heshima hiyo. Bahati mbaya mimi na microphone hatuelewani. Kwa maneno mengine, I am a lousy public speaker. Lakini ukinikaribisha, nitakuja na nitachangia kwa kadri ya uwezo wangu.

Tatizo la bongo ni mob mentality. Watu wakianza kupelekana baharini basi wote wataenda huko. Tumefika mahali ambapo tunakodisha watu wakutuombolezea kwenye misiba. Tunawakodi wangoni kuja kutuimbia kwa vile kila mtu anafanya hivyo. Tunakodisha watu wa kutupikia kiasi kwamba tunakula chakula kile kile kila tuendapo! Kwa kufanya hivyo tunapoteza identity zetu. Kwa nini tusisherehekee na kuomboleza kivyetu? Kama ukoo una makabila mengi basi tuenzi kabila zote hizo na si hii biashara ya kuiga.

Amandla..........
 
Jamani kuna harusi na shughuli nyingi za matajiri zimefanyika without these MCs na hata the so called Matarumbeta na vikafana sana. Nakuhakikishia watoto wangu wakioa au kuolewa, we the parents tutawashauri vema, ni lazima tufanye kitu cha tofauti kwanza cost effective and excellent.

Kwanza kitchen party is fobbiden in my family. I prefer family dinner with close friends. Pia harusi nitashauri kwa upande wa pili tuchanganye, i.e siku ya harusi iwe ya parents wote pande mbili, kwa maana hiyo hakuna cha send off as I would like all close relatives, friends to attend the wedding of our kids na si kupewa tu kadi 20 ili uje na guest 40!!! And this too will be cost effective and excellent.

Na hapo si kwamba I am poor, no, only tu kuwa nataka kutojishughulisha na unnecessary masherehe. Pesa itakayobaki, for sure nina hakika nitachangiwa sana millions so tutawapa watoto wetu wakafanye investments, kama wanazo ni better ziwe banked (though hailipi) for our prospective grand children (assuming we will be blessed to have them).

Tuamke tuachane na sherehe za fuata upepo, hasa wasomi. Tufanya mambo kisomi.
 
Tatizo la bongo ni mob mentality. Watu wakianza kupelekana baharini basi wote wataenda huko. Tumefika mahali ambapo tunakodisha watu wakutuombolezea kwenye misiba. Tunawakodi wangoni kuja kutuimbia kwa vile kila mtu anafanya hivyo. Tunakodisha watu wa kutupikia kiasi kwamba tunakula chakula kile kile kila tuendapo! Kwa kufanya hivyo tunapoteza identity zetu. Kwa nini tusisherehekee na kuomboleza kivyetu? Kama ukoo una makabila mengi basi tuenzi kabila zote hizo na si hii biashara ya kuiga.

Amandla..........

Mkuu Fundi Mchundo,

Napingana na wewe kwenye hii hoja ya kuwa kwa kukodisha wapishi chakula huwa kinakuwa ni kile kile...!!! Mkuu, ukipata mpishi mzuri nina uhakika ataweza kuongeza au kupunguza "viungo" kwenye menu unayotaka. Sasa tatizo nyumbani wengi wakimpata mpishi wanasema tupikie chakula kama kile ulichopika kwenye harusi ya fulani..!! Kwa nini chakula kisifanane mkuu?
 
Jamani mnawatuamia hawa ma MC wakongwe wa nini. Wameshalewa sifa na sasa wamebaki majina tu. Kuna mmoja anaitwa Foma Foma yaani jamaa anakuja kalewa na anakuja na videmu vyake basi yeye yuko biiize na hicho kihawara. Na kila mnachomuagiza anafanya tofauti.

Nilikuwa Mwenyekiti wa kamati ya harusi fulani mwaka jana mwishoni karibu tupigane manake anaboa. Na kweli hawana jipya maneno yao ni yale yale tangu miaka ya tisini. TUACHANE NAO. Na kamchezo ka kukubali kazi then wanakuleteeni mtu mwingine wakidai wana udhuru ndio zao kumbe wana kazi nyingine mtu kapanda dau.

Chitanda umekuwa mtu mzima sasa acha hizo
 
Aisee Muzee unagusa maslahi ya watu:Hili suala la kodi si mchezo baba ukijifikiria haka kamshahara ketu ka kima cha chini harafu kanakatwa kodi,we acha kabisa harafu kodi zetu hawa jamaa wa TRA wanahonga mademu magari inaudhi yaani ni afadhari hii kodi ya mshahara ifutwe wandugu..Rais atakayefuta hii nitamfagilia sana au apunguze kwa wazawa.
Pili kuhusu hawa Ma MC aisee wanamake ile mbaya kwa wiki MC mmoja anaweza kuwa na tenda mbili hadi tatu na malipo yanategemea status ya harusi kama harusi ya kifisadi MC analamba hata M2 kwa sherehe moja.Imagine harusi moja juzi kati hivi budget ilikuwa M26! MC atalamba ngapi?
ila jamani kuna ma MC wengine ni wazuri wanajua nini wanachofanya naweza kuwataja kama mtu anaharusi yake nawapa tano
1.MC Mwakajumba sijui kama nimekosea jina lake,yeye anastaili ya kipekee hasa ya kufungua shampein ambapo hufungua kwa kuimbia shampein funguka na inafunguka bila kuigusa hii ni style ya pekee sijaona mwingine.
2.Sitaacha kumfagilia mwana mama ambaye anakuja kwa kasi hasa kwa beg part na kitchen part na hata harusi si mbaya anaitwa Jemima one-number yake ni 0784349570...huyu anajua kufunda nishawahi kuona akimfunda mwana mmoja jinsi ya kumtreat mke wake.
3.mwingine nishawahi kumuona ni MC kinyau nyau kikia cha pweza,huyu jamaa naye si mbabaishaji anajua kazi yake cheki naye-0713421617

4.Kuna MC anaitwa MC Makasi Junior naye ni mkali hasa style yake ya kupiga kinanda huku akiimba nyimbo zake.

5.Na kibonde yule mtangazaji naye si mbaya amejiingiza kwenye hiyo fani na anaiweza,nishawahi kuomuona akikamua vilivyo.

Na kama kuna watu wanajua ma MC wengine na contact zao ni vyema waziweke wazi kwani itawasaidia wanaotaka kuoa kupata ma MC wasio matapeli kama Chitanda,Charles,Double K na wengine wengi
 
Mkuu Fundi Mchundo,

Napingana na wewe kwenye hii hoja ya kuwa kwa kukodisha wapishi chakula huwa kinakuwa ni kile kile...!!! Mkuu, ukipata mpishi mzuri nina uhakika ataweza kuongeza au kupunguza "viungo" kwenye menu unayotaka. Sasa tatizo nyumbani wengi wakimpata mpishi wanasema tupikie chakula kama kile ulichopika kwenye harusi ya fulani..!! Kwa nini chakula kisifanane mkuu?

Mwanzo wake ndiyo huo. Ninavyojua mimi hao wapishi wakukodi wanakuwa na standard menu zao. Na hizi hazitofautiani. Kutokana na hili, ofa ya vyakula inakuwa limited. Lakini wakati tulipokuwa tukijipikia, tulikuwa tukipika chakula tulichozoea na chenye heshima katika jumuia au kabila letu. Ilikuwa vigumu wakati ule mtu kusema nataka chakula kama nilichokula kwenye harusi fulani maana wapishi walikuwa wengi! Hii vile vile ilijenga familia. Maana ni familia ndiyo ilihusika kuanzia kupanga menu, kuazimana masufuria na sahani, kwenda kununua chakula na viungo, kuchambua mchele au kumenya ndizi, kupika, kugawa, kukusanya vyombo na kuviosha. Mote humu tulishirikiana na tulifanya kwa kadri ya uwezo wetu. Huku kuiga mambo ya wenzetu ndiko ninakopinga.

Amandla..........
 
2.Sitaacha kumfagilia mwana mama ambaye anakuja kwa kasi hasa kwa beg part na kitchen part na hata harusi si mbaya anaitwa Jemima one-number yake ni 0784349570...huyu anajua kufunda nishawahi kuona akimfunda mwana mmoja jinsi ya kumtreat mke wake.

Beg pati tena ndiyo nini?

Haya ya kufunda ndiyo ninayoyalalamikia. Hata kufunda tunategemea wageni? Hao wakina shangazi wako wapi? Mimi nilidhani kufunda kunahusisha pia mila za kabila ulilotoka na desturi za familia yenu! Huyu mgeni atazijuaje zote hizo? Si ndio maana yanakuwa yale yale na ritual nzima kupoteza muelekeo na dira. Kufunda ni serious business na si ya kufanyia mzaha.

Amandla.......
 
Mwanzo wake ndiyo huo. Ninavyojua mimi hao wapishi wakukodi wanakuwa na standard menu zao. Na hizi hazitofautiani. Kutokana na hili, ofa ya vyakula inakuwa limited. Lakini wakati tulipokuwa tukijipikia, tulikuwa tukipika chakula tulichozoea na chenye heshima katika jumuia au kabila letu. Ilikuwa vigumu wakati ule mtu kusema nataka chakula kama nilichokula kwenye harusi fulani maana wapishi walikuwa wengi! Hii vile vile ilijenga familia. Maana ni familia ndiyo ilihusika kuanzia kupanga menu, kuazimana masufuria na sahani, kwenda kununua chakula na viungo, kuchambua mchele au kumenya ndizi, kupika, kugawa, kukusanya vyombo na kuviosha. Mote humu tulishirikiana na tulifanya kwa kadri ya uwezo wetu. Huku kuiga mambo ya wenzetu ndiko ninakopinga.

Amandla..........

Mkuu, haya ya kuajiri wapishi na wataalamu wa menu ndio maendeleo yenyewe haya.

Hayo yote uliyasema hapo juu "kuazimana masufuria na sahani, kwenda kununua chakula na viungo, kuchambua mchele au kumenya ndizi, kupika, kugawa, kukusanya vyombo na kuviosha" yamepitwa na wakati. Tena, ili mradi uchumi unaruhusu nisingependa turudi huko.

Yote yaho yalikuwa yanafanywa na kina mama, matokeo yake wakina mama ambao walitakiwa wakae wajumuike kwenye sherehe ya binti yao kuolewa wanakuwa wako busy kazini kuhudumia wageni wengine hasa wa kiume...hilo mimi nalipinga kabisa.

Wakina mama nao wanatakiwa watumie muda huo wa kupika kujipamba na kuburudika kwa nguvu badala ya kuwa wako kazini.
 
Yebo Yebo.

Si dhambi kuwa nostalgic. Tatizo naona tumekuza hizi sherehe kupita kiasi. Hata kwa wenzetu waliotupita hawafanyi hivi ukiondoa ma-nouveau riche. Kwa wengi harusi bado inafanyika kifamilia. Hawa tunaweza kuwamudu bila kuchelewa kwenye hizo sherehe.

Mara nyingi tunayoyaita maendeleo ni ulimbukeni. Mambo yote kwa wenzetu si kama Sweet Sixteen Party ya MTV!

Amandla.......
 
Mwanzo wake ndiyo huo. Ninavyojua mimi hao wapishi wakukodi wanakuwa na standard menu zao. Na hizi hazitofautiani. Kutokana na hili, ofa ya vyakula inakuwa limited. Lakini wakati tulipokuwa tukijipikia, tulikuwa tukipika chakula tulichozoea na chenye heshima katika jumuia au kabila letu. Ilikuwa vigumu wakati ule mtu kusema nataka chakula kama nilichokula kwenye harusi fulani maana wapishi walikuwa wengi! Hii vile vile ilijenga familia. Maana ni familia ndiyo ilihusika kuanzia kupanga menu, kuazimana masufuria na sahani, kwenda kununua chakula na viungo, kuchambua mchele au kumenya ndizi, kupika, kugawa, kukusanya vyombo na kuviosha. Mote humu tulishirikiana na tulifanya kwa kadri ya uwezo wetu. Huku kuiga mambo ya wenzetu ndiko ninakopinga.

Amandla..........

.....Those were the days. Those were the wedding celebrations!
 
Mkuu, haya ya kuajiri wapishi na wataalamu wa menu ndio maendeleo yenyewe haya.

Hayo yote uliyasema hapo juu "kuazimana masufuria na sahani, kwenda kununua chakula na viungo, kuchambua mchele au kumenya ndizi, kupika, kugawa, kukusanya vyombo na kuviosha" yamepitwa na wakati. Tena, ili mradi uchumi unaruhusu nisingependa turudi huko.

Yote yaho yalikuwa yanafanywa na kina mama, matokeo yake wakina mama ambao walitakiwa wakae wajumuike kwenye sherehe ya binti yao kuolewa wanakuwa wako busy kazini kuhudumia wageni wengine hasa wa kiume...hilo mimi nalipinga kabisa.

Wakina mama nao wanatakiwa watumie muda huo wa kupika kujipamba na kuburudika kwa nguvu badala ya kuwa wako kazini.

...Nakubaliana nawe, Mkuu! lakini usisahau pia kuwa na wanaume nao walikuwa na kazi ya kufukuzana na kuku wa kuchinja, halafu si unawajua wale kuku wa enzi hizo walivyokuwa wanajua kuingia mitini? Usisahau pia kulikuwa na shughuli nzito ya kumuangusha ng'ombe na kumchinja, kumchuna ngozi, kumtengeneza, mbali ya kwenda, kwa mfano kule kwetu, kukata migomba na matawi ya maua kwa ajili ya kupamba eneo litakalofanyikia harusi!! Ninachokumbuka ni kuwa at a certain time watu wazima wote, wababa kwa wamama, walipata muda wa kujiandaa na kushiriki kikamilifu sherehe ya harusi na shughuli ya kugawa chakula na mambo mengine ikaachiwa mabinti wa pande zote mbili!! Sijui, wakati mwingine napenda kudhani kuwa pengine ni mambo ya kifamilia kama haya yaliyofanya ndoa zilizofungwa kwa namna hii kudumu....!
 
Angalia basi tunavyo-complicate mambo. Kuna sherehe ya kuposa. Halafu sherehe ya kutambulishana. Halafu sherehe ya kupokea mahari. Hizi kwa bahati nzuri sehemu nyingi bado hazijawa corrupted.Baada ya tarehe ya harusi kutajwa ndipo fujo zinapoanza.

Tunaanza na Kitchen Party. Hii imekuwa corrupted. Badala ya kuwa ya kifamilia, kumfunda mwanao, kumpa vifaa vya nyumbani n.k. sehemu kubwa imewekwa kwenye mafunzo ya kujamiana. Imefika mahali tunakaribisha mashoga kutoa shule! Mafunzo yaliyokuwa na umuhimu katika jamii sisi tunayafanyia mas'hara! Hii vile vile imekuwa sehemu ya wakina mama kutambiana. Na kwenyewe tunakodi kila kitu maana hakuna mwenye sherehe, wote ni waalikwa wasiotaka kuchafuka siku ya sherehe.

Halafu tuna send-off. Hii nayo imekuwa corrupted. Badala ya kuwa sehemu ya ndugu za binti kumuaga ndugu yao imekuwa siku ya kuwaonyesha wanaotaka kuoa jinsi alikotoka binti kulivyo maji marefu. Hizi nazo zimekuwa ni reception bila harusi. Na kwenyewe hakuna mwenye shughuli. Wote ni waalikwa wasiotaka kuchafua pamba zao! Wazazi wakiwa na bahati wanapewa nusu dakika kumuasi binti yao maana MC anaenda na time na watu wengi walichofuata ni ulabu, muziki na vichekesho vya Mc na si nasaha za wazazi.

Siku ya harusi, ndiyo tusiseme. Hasira zote za kunyimwa kadi kwenye send-off tunamalizia hapa. Na penyewe cha muhimu ni kuwaonyesha watu jinsi tunavyoweza kula, kunywa na kusaza. Sifa imekuwa ni ufunguaji wa champeni na si nasaha za wazazi. Ndugu ambao hawakuwa na uwezo wa kuchanga ndiyo walie. Viti vya heshima vinapewa kwa hao wenye deep pockets, hata kama uhusiano nasi ni mdogo. Hapa tena mkazo si kwenye kushiriki bali ni kuonekana. Na penyewe hamna mwenye shughuli. Wote ni wageni. Wote wanaingia kwa kadi maana kamati ya harusi haina mashara. Hela zote zilizochangwa ni lazima watu wagide. Hakuna free loaders hapa hata kama wanaooana ni wapwa wao. Ngoma za asili nazo zinapewa dakika mbili maana ratiba ilichelewa kwa sababu maharusi walienda kupiga picha bich au Mlimani City! Maharusi wanatangulizwa na matarumbeta. Chakula ni kile kile, chips kidogo, wali, shingo la kuku, kipande cha chapati, mboga zilizochoka na ndizi zisizojulikana zilikotoka! Tunajipanga kupeleka hzawadi zetu za bilauli zilifungwa kwenye mabox na makaratasi mazuri. Maharusi wanacheza rumba moja kutoka katika muziki kutoka ughaibuni. DJ kuonyesha uzalendo anapiga Chakacha, bongo flava n.k. Wacheza ngoma za kitamaduni wako hoi maana hakuna aliyekumbuka kuwapa chakula. Watu wanatapika, wanajisaidia hovyo halafu wanaondoka wakisifia harusi.

Baada ya wiki mbili, tunavunja kamati. Hapo napo tunaelezwa kuwa kuna mbinamu wa Bwana harusi nae anakusudia kuoa hivi karibuni. Kamati inaundwa upya. Mchezo unaanza tena. Ndiyo maisha yetu. Ndiyo maendeleo yetu.

Count me out!

Amandla........
 
Last edited:
Mimi nilimwamini sana MC Chitanda. Kwani mavazi yake yanavutia awpo kwenye kazi yake. Huwa anapendelea kuvaa kama Mnaigeria. Nashukuru kwa kunipa alivyo Mc huyu. Inabidi tumuogope na kumwepuka kama ukoma.
 
Kumbe Chihanda alipendwa kwa vile anavaa kama wanaijeria? Nazidi kusononeka.
 
....ME, too!
 
Kumbe Chihanda alipendwa kwa vile anavaa kama wanaijeria? Nazidi kusononeka.

Fundi,

Utafanyaje tena ndiyo "idiocracy" yenyewe hiyo sasa inatawala. Tungojee tu tuambiwe MC amekodiwa kutoka Muscat, Paris au New York, complete with a guaranteed featuring in some celebrity magazine.

Au hata wabeba majeneza wanaotoka Hollywood, complete with some weird costume.

Ndiko tunakoelekea huko, ni swala la degree ya upuuzi huu tu.
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom