MC Chitanda ni tapeli? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

MC Chitanda ni tapeli?

Discussion in 'Celebrities Forum' started by Kimambo, Apr 14, 2009.

 1. K

  Kimambo Member

  #1
  Apr 14, 2009
  Joined: Mar 31, 2008
  Messages: 76
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 15
  Wandugu naomba kuwasilisha, tabia za baadhi ya ma MC zimekuwa ni mbaya sana hata kusababisha watu na sherehe zao kujikuta kwenye taharuki kubwa.

  Ukweli ni huu:

  MC Chitanda ambaye ni mfanyakazi wa ATC alibukiwa kwa ajili ya sherehe ya harusi ya rafiiki yangu toka November mwaka jana shuguli ambayo ilikuwa ni ya mwezi wa nne tarehe 18 April 2009 na alipewa advance amount toka December 2008 cha ajabu baada ya muda akapotea kabisa akitafutwa anazima simu na hakutoa ushirikiano wa kutosha, ilipofika tarehe saba april 2009 akatafutwa ili akonfirm akaconfirm na kuwashukuru wajumbe kwa kumkumbusha, cha ajabu kesho yake akaomba kukutana na wanakamati alipofika akatoa tarifa kuwa anasikitika kuwa kamati haijambuku tarehe hiyo na ila amebukiwa kwa sherehe ya tahe 16 may 2009.

  Tafrani iliotokea hapo hailezeki, ila busara za mwenyekiti ilibidi zimokoe kutoka kipigo cha wanakamati, alipobanwa akakiri kupata kazi nyingine mahali pengine, jamani ndugu wa karibu nae muonyeni huyu bwana asiharibie watu starehe zao na mjihadhari nae pia si mwaminifu na ni tapeli kwani amegoma kurudisha hata hela ya advance aliochukua akisema ameishiwa.

  Jamani msaidieni kwa nia njema.....
   
 2. Bill

  Bill JF-Expert Member

  #2
  Apr 14, 2009
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 4,167
  Likes Received: 1,251
  Trophy Points: 280
  Hakika huu ni wizi, huyu Chitanda sasa anakoelekea ni kubaya. Cha Msingi ikiwa alichukua pesa kwa maandishi na alijua kabisa yuko booked kwa sherehe hiyo akaamua kuchua pesa kwingine, huu ni utapeli na ni wizi. Anastahili kuburuzwa courtin.

  Huu nao ni aina ya ufisadi, huyu jamaa angekuwa serikalini kwenye nafasi nyeti angeiba sana. Hafai tuanze kujiepusha naye
   
 3. J

  Jafar JF-Expert Member

  #3
  Apr 14, 2009
  Joined: Nov 3, 2006
  Messages: 1,138
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Tatizo kubwa ninaloliona ni kuwa malipo mengi kwa ajili ya gharama mbalimbali hufanywa bila ya maandishi.(non receipts). Hivyo basi hutoa nafasi kwa watu (ma-MC na wengine) wenye roho nyepesi kukana pindi wanapotakiwa kuthibitisha. Ni vigumu kumchukulia mtu hatua na ikafanikiwa kama huna receipts.
   
 4. BelindaJacob

  BelindaJacob JF-Expert Member

  #4
  Apr 14, 2009
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 6,060
  Likes Received: 476
  Trophy Points: 180
  Mc Chitanda tumemtumia sana kwenye shughuli mbalimbali za familia na alikuwa mwajibikaji mzuri tu na kazi yake miaka ya nyuma kidogo!

  Hivi karibuni sijapata kusikia habari za kazi zake mpaka kwenye hii thread. Kama Chitanda kafanya hivyo ajirekebishe maana nawezekana akapoteza jina lake kwa tukio kama hilo na siku hizi kuna MCs wengi sana kwahiyo akaondoka taratibu kwenye hiyo kazi kwa aibu.

  Ukifanya kazi nzuri watu wanawaambia na wengine na unazidi kujulikana na kupata kusherehesha ila kama yeye yuko hivyo ni noma kwakweli.

  Ajirekebishe mapema kama ana nia ya kundelea na ushereheshaji!..
   
  Last edited: Apr 14, 2009
 5. K

  Kyachakiche JF-Expert Member

  #5
  Apr 14, 2009
  Joined: Feb 16, 2009
  Messages: 911
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 45
  Hivi bado ofisi yake bado iko magomeni?
   
 6. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #6
  Apr 14, 2009
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Lakini hivi kweli tunahitaji mc? Kwa nini tusianze kubeba huu mzigo wenyewe halafu tuone jamaa watakimbilia wapi! Vichekesho ni vile vile, hadithi ni zile zile sasa kinatushinda nini? Tuefika mahali hata kwenye basdei na misiba na kwenyewe tunakodi em si! Au ndio status symbol ya siku hizi?

  Amandla........
   
 7. k

  kosamfe Member

  #7
  Apr 14, 2009
  Joined: Apr 14, 2009
  Messages: 71
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nadhani hii si kwa Chitanda peke yake ni karibu ma MC wote hasa wale maarufu, pindi wanapopata kazi ya hela nyingi zaidi ya ile ya awali hutelekeza na kutoa visingizio visivyo vya kweli. Nina mifano hai mingi nikiwa pia ni mmoja wa waathirika wa utapeli huo wa ma MC.

  Felix KOSAMU
   
 8. Masanja

  Masanja JF-Expert Member

  #8
  Apr 14, 2009
  Joined: Aug 1, 2007
  Messages: 3,595
  Likes Received: 3,763
  Trophy Points: 280


  FUNDI,

  Nataka niku-"book" rasmi uwe MC kwenye harusi yangu ambayo sijui itakuwa lini. What does it take kuwa na mtu kama wewe? Maana najua wageni wangu wanaweza faidika na busara za mwenyekiti Fundi..Nakuaminia kaka.....
   
 9. m

  mzee wa pwani New Member

  #9
  Apr 14, 2009
  Joined: Apr 10, 2009
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wandugu napenda kuchangia kuhusu hili,

  Kuna MC mmoja tulimbook maarufu kama Double K naye ni TAPELI Alishawahi kulamba advance yetu na siku za mwisho akaja kuchukua full na kwa maandishi kabisa lakini cha kushangaza siku ya tukio alituletea MC mwingine sijui mjomba wake aisee yaani alituboa mwanzo mpaka mwisho wa shuguli inatuuma mpaka leo hatusahau.

  Vile vile kuna ka MC kamoja kanachipukia ni kabitoz kanajiita MC charles kalitoboa siku moja kwenye sherehe kameingia saa 2 ukumbini na kuingia tu vyombo vya mziki havifanyi kazi MIC ilibidi aazimwe na mchizi mmoja hivi na huyo mchizi aliidai hiyo MIC kabla ya shughuli kumalizika kwa kuwa jamaa hakumtoa mchizi shughuli iliisha watu hata kucheza mziki hawakucheza...huyu jamaa naye aogopewe kama ukoma anaharibu shughuli za watu.
   
 10. Katikomile

  Katikomile JF-Expert Member

  #10
  Apr 14, 2009
  Joined: Jul 12, 2007
  Messages: 473
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  Nashukuru hili suala limekuja hapa!

  Sasa wakati umefika kwa hawa watu wajulikane kwenye idara muhimu za serikali (BRELA, TRA n.k) ili kodi husika zilipwe. Ukipiga hesabu ya kila tukio, say shs 300,000 na wastani wa matukio 2 kwa wiki, hiyo ni shs 600,000, kwa mwezi net of 2.4Mil, tax free. Sina uhakika kama hili TRA wameishalifanyia kazi, they real have a challenge on approaching the matter!

  Chitanda ndio mwisho wa safari yake ya kutengeneza untaxable money, itabidi aanze kutunza vizuri mshahara wake wa ATC (am not sure of his level of education anyway). Na anaposema hali ni mbaya hawezi kurudisha advance, has it to do with ATC credit crunch??????????????

  NI HAYO TU!
   
 11. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #11
  Apr 14, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  This is just a case of the chicken coming home to roost.

  Wanaom-book MC wanataka mtu mwenye manjonjo, madoido mengi, anayeweza kui hype shughuli kuliko hata ilivyo kikweli (mambo mengine yanayosemwa na kufanywa na hawa ma MC ni aibu kwa mtu mwenye maadili yake)mtu tapeli tapeli hivi.

  Kwa hiyo haishangazi sana mtu kama huyo akianza mtini, akifanya deliberate double bookings etc.

  Kama alivyosema Fundi, badala ya kumchukua MC ambaye most probably hata hawajui maharusi, ingependeza kuwa na mtu wa karibu anayeweza kuifanya kazi hii ambaye mara nyingi anaweza kuweka personal and real anecdotes za maisha ya maharusi, badala ya kutegemea tired and recycled packaged jokes.
   
 12. Masanja

  Masanja JF-Expert Member

  #12
  Apr 14, 2009
  Joined: Aug 1, 2007
  Messages: 3,595
  Likes Received: 3,763
  Trophy Points: 280

  Kijana hii kauli imetulia. Kwa kweli hata mimi nilishaamua...ikitokea hiyo harusi ikawepo..MC asahau pesa yangu. I agree..ni vema kutafuta mtu anayeweza kuchangamsha ukumbi kwa kutoa utani wenye message..Lakini mbona watu wa kawaida wanaweza? Lakini bongo bwana..harusi zimeshakuwa shughuli pevu inayohitaji substantial investment of resources..wanaogopesha vijana kuoa sasa..unakuta mdada/mkaka anataka harusi bab kubwa..kijana ndo akina Masanja hapa..choka mbaya.....Inabidi uingie mitini tuu...

  Ndo maana nimemuomba Fundi aniambie anapatikana vipi. Fundi hope hutaingia mitini na kumtuma mwakilishi....I dont want "tired and recycled packaged jokes" za akina Chitanda, chumvi chumvi et al!
   
 13. BabaDesi

  BabaDesi JF-Expert Member

  #13
  Apr 14, 2009
  Joined: Jun 30, 2007
  Messages: 2,795
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Umenena Vyema.

  Ukweli ni kwamba haya mambo mengine tunajitakia tu. Shughuli hizi zamani, tena si zamani kihivyo, alipewa mtu wa familia na akaweza kuisherehesha vyema sherehe. Lakini cha ajabu siku hizi Watu wanataka mtu anayebwabwaja ovyo kiasi cha kusema 'Bwana harusi amesoma Vyuo Vikuu vyote Vya dunia' na ndugu wa bwana harusi wanashangilia kwa nguvu zao zote huku wakijua wazi kuwa ndugu yao kaishia kidato cha nne F! Sijui ndio kujenga prestige, au ni Ujinga tu!

  Tatizo lingine ni njaa ya watanzania, utakuta mtu kwenye kamati anampigia debe MC fulani ama Mpishi fulani ama Mpambaji fulani ama Mshoot video fulani kwa sababu tu anajua huyo mtu akichaguliwa atampa ten Percent! wizi Mtupu!

  Nimemuambia First Born wangu kuwa harusi yake sitachangisha mtu zaidi ya kile tulichonacho na watakacholeta ndugu, MC atakuwa baba yake mkubwa, Wapishi watakuwa ni shangazi zake, mama wakubwa na mama wadogo zake ambao pia watakuwa wapambaji na mchukuaji wa video atakuwa mdogo wake, harusi imefanyika!
   
 14. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #14
  Apr 14, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Hahahah hii nimeipenda sana no MC's
   
 15. BelindaJacob

  BelindaJacob JF-Expert Member

  #15
  Apr 14, 2009
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 6,060
  Likes Received: 476
  Trophy Points: 180
  Plan imetulia, Na Iwe Mkuu!...
   
 16. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #16
  Apr 14, 2009
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 2,141
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Wakuu,

  Kwa sababu tu MC Chitanda ameharibu majukumu yake...ndio sasa mnakuja hapa kudharau fani nzima ya MC...??!!

  Kuwa MC ni fani, kazi na inahitaji kipaji kama ilivyo Music, Sinema, Soka, Uanasheria, Upigaji Picha, Uhasibu n.k. MC mzuri akipewa kazi anajipanga kabla ya siku kufika, anawatembelea maharusi na kukaa nao ili kuwafahamu, anajua ni watu wa aina gani, wanapendelea au hawapendi vitu gani n.k. Iwapo Chitanda ameharibu acheni ku-generalise kuwa kazi ya MC sio kazi muhimu na kwamba haihitaji kipaji.

  Ikitokea wajomba na baba zenu wadogo wana vipaji na uwezo wa kuwa MC's, kheri yenu. Kazi ni kazi, kujua kuongea haimaanishi unaweza kuwa MC mzuri, acheni roho za kimaskini; kama uchumi unaruhusu ajiri MC, Mpiga picha, Wapishi, Wahudumu n.k au nyie mlidhani ajira zinatokaga mbinguni. Ebo....
   
 17. BabaDesi

  BabaDesi JF-Expert Member

  #17
  Apr 14, 2009
  Joined: Jun 30, 2007
  Messages: 2,795
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  ...Usikimbie kivuli chako, Mkuu!

  Hakuna aliyesema ama anayetaka kudharau kazi ya MC! Swali ni je ina ulazima sana katika sherehe ya harusi?

  Wazazi wangu na wazazi wako walipofunga ndoa yao walikuwa na MC? Kama hawakuwepo, je sherehe ya ndoa yao haikufana sawa na ya watoto wao miaka 40 baadaye iliyokuwa na MC? Je harusi ambazo hazikuajiri MC, pamoja na family zao kuwa na kipato cha kutosha tu, hazihesabiwi kufana kwa vile ziliamua kuwa MC awe baba mdogo wa Bwana Harusi??

  Mkuu, Ni Kweli kazi ya MC ni fani, lakini kama ilivyo kwenye music, sinema, soka, uanashera nk sio kila anayeshiriki kwenye fani hizo basi na ana Kipaji na fani husika, wengine walipaswa kuwa watizamaji tu!!!

  All in All, yapo maeneo mengi tu katika jamii yetu ambayo maMc wanaweza kupata ajira, mikutano, makongamano, semina, graduations na kadhalika na kadhalika! In my Son's wedding I can do without them...and I will!!! That is my right, Isn't it??
  After all, wedding ceremonies are just for celebrating the joining together of Two Persons in Love and should not be eneo la watu kujipatia ajira...!!!

  Are you One of them, Brother? teh teh. Jas' kiddin'!
   
 18. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #18
  Apr 14, 2009
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 2,141
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0

  BabaDeci,

  Mimi sio MC na wala sitakuja kuwa MC..!!

  Unaposema iwapo MC ni muhimu kwenye harusi...sijui una maana gani kwa mapana. Hebu tujiulize, kuna umuhimu wa kuwa na bia kwenye sherehe za harusi?? Nimehudhuria harusi nyingi ambazo hakukuwa na pombe kabisa, lakini hizo harusi zilifana pengine kuzidi hata baadhi ya zile zilizokuwa na pombe nyingi za kila aina.

  Hoja yangu ni kuwa, swali la iwapo MC ni muhimu au la halina mantiki. Yote inategemea uchumi na mapenzi ya wenye harusi...lakini pia humo humo kunapatikana ajira kwa Watanzania wengine wenye vipaji vya u-MC.

  Tuzungumzie namna ya kuboresha mikataba ya aina hii kati ya wenye harusi/ sherehe/misiba n.k na ma-MC, wapiga picha n.k

  Haki ya kutokuwa na MC kwenye harusi ya mwanao unayo mkuu wala sina nia ya kukupinga..ila siku ya siku ikifika natumaini mwanao atakubaliana na wewe..!!
   
 19. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #19
  Apr 15, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,572
  Likes Received: 5,759
  Trophy Points: 280
  lipwaa mpaka sasa.....
   
 20. Iteitei Lya Kitee

  Iteitei Lya Kitee JF-Expert Member

  #20
  Apr 15, 2009
  Joined: Jan 2, 2008
  Messages: 589
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  kwa nini kung'ang'ania MC mmoja?Ma MC si wapo wengi hapa mjini?
  Kama hawezi kazi anyang'wanye then apewe mtu mwingine plz.
   
Loading...