Mbwembwe za mabinti ukweni kabla ya ndoa

Mbwembwe za mabinti ukweni kabla ya ndoa

Amoxlin

JF-Expert Member
Joined
May 30, 2016
Posts
3,782
Reaction score
4,118
Amani iwe nanyi ndugu zangu JF,

Poleni kwa pilikapilika za maisha na matamko/miluzi mingi inayoibuka kila kukicha.Leo hii nataka tutathimini hizi mbwembwe wanazokua nazo akina dada kwa wachumba zao na hasa ukweni wanapotambulishwa kabla ya ndoa.

Pindi tu wanapotambulishwa ukweni huwa na heshima nzuri kupita kiasi, yani unaweza kujiuliza binti huyu amezaliwa au kashushwa toka mbinguni?
Anazungumza kwa heshima na adabu zote kila wakati na huwa mnyenyekevu kwa watu wote sambamba na kuwa mtiifu kwa kila atakachoambiwa.

Anaamka asubuhi na mapema kuliko hata alivyozoea na hufanya kazi zote peke yake mpaka nyote mnasema yes huyo ndo binti wa kuoa/kuolewa na mwanangu. Kila kazi anataka aifanye yeye mwenyewe bila hata kusaidiwa.

Katika kipindi hiki mwanaume na ndugu zake wanakua na furaha na taswira mpya akilini mwao bila kujua wayaonayo ni mbwembwe za muda mfupi tu zisizo na uhalisia. Umeona wapi mtu anafanya kazi kama mashine pasi kupunzika?

Picha linabadilika baada ya ndoa, hapo ndipo utaifahamu tabia halisi ya mkeo/mkaza mwana. Atachelewa kuamka, atafanya kazi akijisikia na ataleta mapozi mpaka kwa watu muhimu kwako.Haya yote nimeshuhudia mara kadhaa, sasa najiuliza na huko kwenu yapo au ni huku kwetu tu?
 
Amani iwe nanyi ndugu zangu ktk Jf.

Poleni kwa pilkapilka za maisha na matamko/miluzi mingi inayoibuka kila kukicha.

Leo hii nataka tutathimini hizi mbwembwe wanazokua nazo akina dada kwa wachumba zao na hasa ukweni wanapotambulishwa kabla ya ndoa.

Pindi tu wanapotambulishwa ukweni huwa na heshima nzuri kupita kiasi, yani unaweza kujiuliza binti huyu amezaliwa au kashushwa toka mbinguni?

Anazungumza kwa heshima na adabu zote kila wakati na huwa mnyenyekevu kwa watu wote sambamba na kuwa mtiifu kwa kila atakachoambiwa.

Anaamka asubuhi na mapema kuliko hata alivyozoea na hufanya kazi zote peke yake mpaka nyote mnasema yeeees huyo ndo binti wa kuoa/kuolewa na mwanangu. Kila kazi anataka aifanye yeye mwenyewe bila hata kusaidiwa.

Katika kipindi hiki mwanaume na ndg zake wanakua na furaha na taswira mpya akilini mwao bila kujua wayaonayo ni mbwembwe za muda mfupi tu zisizo na uhalisia. Umeona wapi mtu anafanya kazi kama mashine pasi kupunzika?

Picha linabadilika baada ya ndoa, hapo ndipo utaifahamu tabia halisi ya mkeo/mkaza mwana. Atachelewa kuamka, atafanya kazi akijiskia na ataleta mapozi mpaka kwa watu muhimu kwako.

Haya yote nimeshuhudia mara kadhaa, sasa najiuliza na huko kwenu yapo au ni huku kwetu tu?

kuna makundi ya wanawake wanaoigiza tabia njema na wenye tabia njema hivyo basi tabia ya kuigiza huwa haidumu hata kidogo

tabia ya mtu ni kama ngozi ni ngumu sana kuibadili
 
Maigizo ni hatari sana. Mwisho wa siku kweli ukibainika afadhali kukaa na shetani!!!! (Magufuri, 2016)
 
hivi ni kweli wanawake wote walioolewa wana tabia kama hizo ?
Wapo ambao uchapakazi ni asili yao ila 100% kubwa wanaigiza ili wapate watakacho.
 
Maigizo ni hatari sana. Mwisho wa siku kweli ukibainika afadhali kukaa na shetani!!!! (Magufuri, 2016)
Kweli kabisa, afadhali aoneshe makucha yake toka mwanzo ili ufahamu utakabiliana nayo vipi mpaka uyakate kuliko kuja kivingine kimbe sivyo alivyo.
 
Hata ningekuepo mimi obviously ningejitahid ilimradi wasinijue udhaifu wangu.. ni mme wangu tuu ndo anatakiwa kuujua ubovu wa mwanamke wake Na kukabiliana nae
[emoji15] [emoji15] tatizo wanaporudi ukweni kusalimia wanakua washasahau maigizo yao ya awali.
Unakuta kila kitu hovyo, analala kama kapigwa 1/2 kaputi.

Kuna shemeji yangu sasa nyumba inakua chafu mpaka naamua kupiga deki mwenyewe na yeye yupo tu.
 
Nashukuru Mungu sikupitia hayo maana akili yangu inatafsiri vibaya, haya wenye vifungo vya maisha mkuje mtiririke humu, ngoja nielekee kwa masinia maseja.
Utakuwa huna fursa hii, unajifariji..!
 
Unajua suala linakuja pale ambapo wao hawanipokei km mtoto wa familia yao wanataka niendelee kuenyeka tu hawana huruma na mimi. Kumbe ifike sehemu wanione km mwanao tu
Tatizo ni pale ambapo wewe unachapa kazi kupita uwezo wako na kujifanya tofauti na watu wengine.
Wakishakuzoea hivyo watapenda kukuona hivyo wakati wote.
 
Mie hata kuigiza siwezi am really...na amka mda nilio zoea, nafanya shughuli za ndani ya uwezo wangu nikichoka napumzika

chakujifanya Mie ni trekta natafta nini..kuigiza siwez mama mkwe nipende jinsi nilivyo
 
Back
Top Bottom