kilimasera
JF-Expert Member
- Dec 2, 2009
- 3,068
- 268
Shirikisho la Soka nchini (TFF) limesema kuwa mshambuliaji Mbwana Samatta ni wa klabu ya Simba kwakuwa klabu hiyo ilifuata taratibu zote za uhamisho wake kutoka African Lyon mwanzoni mwa msimu uliomalizika.
Akizungumza na NIPASHE jana, Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah, alisema kuwa kutokana na kumbukumbu walizo nazo, Samatta si mchezaji wa Lyon na kwamba Simba wana haki ya kumuuza.
Simba wameafiki kumuuza Samatta kwa mabingwa mara mbili mfululizo wa Afrika, TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Osiah alitoa ufafanuzi huo kufuatia uongozi wa klabu ya Lyon kukaririwa ukidai kuwa wao (Lyon) ndio wamiliki halali wa mchezaji huyo na kwamba wanastahili kupokea fedha zote za usajili wa mchezaji huyo kutoka TP Mazembe.
"Simba walifuata taratibu zote za kumsajili Samatta kutoka Africa Lyon na ndio maana TFF ilimuidhinisha mchezaji huyo kuichezea Simba katika msimu uliomalizika," alisema Osiah.
Alisema kuwa hata kama kuna malipo kwa mchezaji au klabu hiyo hayajakamilishwa na Simba, bado jambo hilo haliwezi kuifanya TFF ione kwamba Samatta ni wa Lyon.
Simba imeripotiwa kumuuza mchezaji huyo Mazembe kwa ada ya uhamisho wa dola za Marekani 100,000 ambazo ni sawa na Sh. Milioni 150.
Baada ya kusajiliwa na Simba akitokea Lyon mwanzoni mwa msimu ulioisha, Samatta aligoma kuichezea klabu hiyo ya Msimbazi hadi alipotimiziwa sharti la mkataba wake la kupewa gari.