Mbwana Samatta

ETi timu ya ya jeshi la polisi imepani kusajili msimu ujao na kumuahidi kumpa ajira kwa mujibu wa kipindi cha michezo radio one jana na pia TP Mazembe wameonyesha nia kuwa watamsajali tusubiri kuona
 
Hao akina Samatta wapo wengi sana Bongo, na wapo wakali zaidi ya Samatta.
Walivyotokea akina Ngassa nao walisifiwa hivyo hivyo.
Dawa sio kumkimbiza Samatta nje ya nchi, tuanze kwanza kuijenga soka nzima ya Tanzania.

Ngasa alibaniwa na Yanga kwenda Norway. Westham ilikuwa klabu kubwa sana kwa Ngasa kuanzia kucheza soka Ulaya. Tunatumaini akilinda kipaji chake Simba hawataweza kumbania kuendeleza kipaji chake kwenye timu kubwa zaidi hata kama ni Mazembe
 
Kwe..kwe..kweeeee............

Iliandika historia ya kuwaletea watani zetu yule kipa anayesota baada ya timu yake kupata bao ili nao wamuone,bila hivyo wangeendelea kumsikia tu, na tukaruhusu magoli ili waone jinsi anavyosota.
 
Iliandika historia ya kuwaletea watani zetu yule kipa anayesota baada ya timu yake kupata bao ili nao wamuone,bila hivyo wangeendelea kumsikia tu, na tukaruhusu magoli ili waone jinsi anavyosota.


Dihile mlishampa chake kwa game ya leo?Maana Kado aliwagomea.
 
kuna wachezaji Tanzania akicheza mechi mbili tatu kwa kiwango cha juu basi yeye ndiyo atajiona Ronald....Mfano kuna mcheza wa simba Humdu alikuwa mtwa sugar kiwango chake kilikuwa juu mno tulipo cheza na Ivory coast baada ya hapo akajiona amemaliza leo anasugua bechi....
 
Ngasa alibaniwa na Yanga kwenda Norway. Westham ilikuwa klabu kubwa sana kwa Ngasa kuanzia kucheza soka Ulaya. Tunatumaini akilinda kipaji chake Simba hawataweza kumbania kuendeleza kipaji chake kwenye timu kubwa zaidi hata kama ni Mazembe
Nasikia kaitwa timu ya chini ya miaka 23...sisi watanzania kwa uongo yaani baada ya sakata la Nurdin bakari hawaja koma...Leo tunaambiwa Ngasa yuko chini ya miaka 23
 
Hao akina Samatta wapo wengi sana Bongo, na wapo wakali zaidi ya Samatta.
Walivyotokea akina Ngassa nao walisifiwa hivyo hivyo.
Dawa sio kumkimbiza Samatta nje ya nchi, tuanze kwanza kuijenga soka nzima ya Tanzania.
jaribu kuweka pembeni upenzi wako wa yebo yebo, mpira wa Ngassa na Samatta ni vitu viwili tofauti...na wanatofautiana kwa vitu vingi sana ngasa wakati ana wika sana mpira wake ulikuwa washule na kukimbila kimbia ndiyo maana Maximo alimkataa mwanzoni...Mbwana Samatta ana kila kitu kinacho takiwa kwa mshambuliaji...
 
Samata anatakiwa aondoke kabisa Simba na Tanzania kama anataka kuendelea... Ajaribu kwenda nchi zinazoheshimika kwa kukuza vipaji kama belgium, France

Kwakweli he is a gem na movement zake kama ni darasani tungesema ni mtaalam wa physics ya kufa mtu

the boy is a superstar

Hiyo ndiyo inatuonyesha kuwa hata hawa mawakala wa wachezaji tulionao ni feki! kwa kiwango kile Mbwana Samata alitakiwa kuwa tayari angalau amefanya majaribio huko majuu. Mpaka sasa hatujasikia chochote wakati ki ukweli kiwango chake siyo cha hapa Bongo. Wanafuatilia mpira wa Kibongo hata hao akina Nonda hawakuwa na kiwango kizuri kama hiki. Tuamke.
 
Mbwana mkali ile mbaya wachezaji kama huyo dogo ni adimu sana nchini kwetu utasema yote ukweli utakuwa palepale na dogo atapata mafanikio makubwa kimpira na kimaisha tumwombee asimame kiushindani .
 
SHIRIKISHO la Soka Tanzania, TFF,
limesema klabu ya Simba inaweza
kufanya lolote kwa Mbwana Samatta
kwa kuwa ni mchezaji halali wa klabu hiyo.
Kauli ya TFF imekuja baada ya African
Lyon kutaka simba iwape fedha zote
za usajili wa mchezaji huyo aliyeko
katika majaribio nchini DR Congo.
Simba ilimchukua mchezaji huyo kutoka African Lyon.
Lyon waliibuka baada ya klabu ya TP
Mazembe ya DR Congo kumnunua
mchezaji huyo kwa dola 100,000
(sh150mil) ambazo Simba
imekubaliana na Mazembe huku African Lyon wakidai kuwa fedha hizo
hazikustaili kwenda Simba kwa kuwa
mchezaji huyo alienda Simba kwa
mkopo.
Mwenyekiti wa kamati ya Mashindano
ya TFF, Saad Kawemba alisema kuwa kwa upande wao hawana mkataba
wa African Lyon na Samatta bali wana
nakala ya mkataba wa Simba
unaoeleza kuwa Samatta ni mchezaji
wao halali.
Alisema kama mchezaji huyo angekuwa sio halali kamati hiyo
ingeinyang'anya Simba pointi zote
ambazo walipata katika michezo yote
ambayo Mbwana alicheza kwa mujibu
wa kanuni zinavyoeleza.
Alisema na kama mchezaji huyo asingekuwa halali na kama usajili
wake ungekuwa na mashaka basi
Simba isingeruhusiwa kumtumia
mpaka pale watakapomalizana na
klabu husika ambayo mchezaji huyo
katoka. Wakati hayo yakiendelea kushika
kasi, Vicky Kimaro anaripoti kuwa
uongozi wa Afrika Lyon unapanga
kulifikisha suala lao Shirikisho la Soka
bAfrika (CAF) na lile la kimataifa, FIFA
kutokana na kutumia ubabe kumuuza mchezaji wao.
Akizungumza na Mwananchi kiongozi
wa juu wa klabu hiyo alisema mbali na
Simba pia wataishtaki TFF kwa kitendo
chao cha kupuuza barua zao za
malalamiko walizowaandikia TFF mwaka jana.
"Hakuna mkataba wowote kati ya
Afrika Lyon na Simba ambao
ulikubaliana Samata na Rashid Gumbo
kuichezea Simba, hakuna hata mali
kauli si uongozi wetu wala ule uliopita, na hili suala tuliwaandikia TFF barua
kama nane hizi hapa,(alionyesha)
wakati Kayuni anakaimu nafasi ya
katibu mkuu lakini hakuna hata moja
aliyoifanyia kazi,"alisema kiongozi
huyo "Tangu tumeichukua Afrika Lyon
tumekuwa tukiwandikia TFF barua
mara kwa mara kuwakumbusha
kuhusu wachezaji wetu, chochote
kitakachotokea tusibebeshwe lawama
na kesho (leo) tutaweka wazi mikataba ya wakina Samata na barua
zote ambazo tuliwaanindikia TFF na
hawakuchukua hatua yoyote,"
alisema.
Hata hivyo, habari zilizopatikana
baadaye jana jioni zilisema kuwa Katibu Mkuu wa Lyon, Brain Ernest
alisema kuwa wanachodai Simba ni
fedha za usajili ambazo klabu hiyo
haikumalizia katika usajili wake.
Katika hatua nyingine viongozi wa
Simba wameanza kufanya mazungumzo na mshambuliaji wa
Yanga, Samte Ally ili aweze kuichezea
Simba msimu ujao wa ligi kuu
Tanzania bara.
Habari ambazo zilipatikana jana
kutoka kwa moja wa viongozi wa Simba zilieleza kuwa Kamati hiyo ya
usajili imeanza mazungumzo na
mchezaji huyo tangu wiki iliyopita
lakini kumekuwa na kutokubaliana
kwa baadhi ya wajumbe wa kamati
hiyo wakidai kuwa mchezaji huyo amekuwa na utovu wa nidhamu kwa
muda mrefu.
Mpaka sasa Simba imekwishanasa
saini za Obadia Mungusa, Mwinyi
Kazimoto,salum Machaku na Patrick
Mafisango, Godfrey Katerega (Atraco) na Ulimboka Mwakingwe.
 
Kwani simba wao hawataki wachezaji wazuri?
Kwanini wamuuze Samata wakati huyo ndie mchezaji kinara wa simba
 
haa haaaaaaa!maskini African lyon yaani baada ya kusikia mapesa ndio sasa mnamkumbuka Samatta kuwa mchezaji wenu halali?sasa mimi nashindwa kuwaelewa viongozi wa African lyon hivi huyu si ndiye Samatta ambaye wamekuwa wakimuona akicheza ligi mpaka imekwisha akiwa halali kwa simba?walikuwa wapi kumwekea pingamizi?kusikia hela tu basi midomo ishajaza mate.Ama kweli mfa maji.........!!
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom