Mbwana Samatta Man of the Match achemka kutema Ung'eng'e

Taifa Stars imefuzu kucheza Nusu fainali baada ya kuivurumisha Uganda, na mtu aliye teuliwa man of the Match ni Mbwana Samatta ana hojiwa na Ssport kwa kimombo akashindwa na kuomba kuhojiwa kiswahili
kwa hili la Samatta ni dhahiri shahiri wanatakiwa kupelekwa twishen ya kidhungu ili wawe realy Profeshenal

Muwe na tabia ya kuthamini michango ya wenzenu, mwenzetu amepambana kwa ajili ya nchiyake mpaka amekua man of the match na timu yetu tumeshuhudia ikipata ushindi kwa kazi nzuri ya vijana wetu kwa ujumla.
 
alichemsha Anelka lugha ya Malkia sembuse Samata,mimi nimemkubali dogo kwa kutujali hata sisi tusiojua kithungu ambao tulikuwa tukimtizama ktk luninga
 
Acha uzembe wewe sio unaandika tu vitu kama Elton John huyo Tevez yuko uingereza na hajui kingereza
 
sasa yeye kingereza akijue ili iweje na kina msaidia nn mzee au unaropoka tu uonekane umo na wewe MESSI anajua kingereza yule na nimchezaji bora duniani.....msiwe mnaleta mambo ya ki Elton John hapa
 
Kithungu ni lugha yake ya pili. Kule Congo wanaongea kiswahiki na vilugha vya huko. Hivyo wachezaji wanatakiwa wakifika hapa wajue lugha nyingi. Japo ni sawa kama amependa kuongea kiswahili.
 
Ni kweli Samata hajui Kiingereza. Sasa? Mtu achekwe kwa kutojua lugha yake ya Kiswahili sio Kizungu. Safi M.SAMATA
 
Hata mchezaji bora wa dunia-Lionnel Messo kama angehojiwa kwa Kimombo, naye angeomba ahojiwe kwa lugha ya kwap, hakuna cha ajabu hapo.
 
kujitambua kama huku ndio kutamfanya dogo afike mbali. Big up Mbwana
 
Chezeiya Lugha ya Malkia wewe kidhungu kimekuja na Meli achana nacho kabisa

wao ndo wamekosea mbona kuna Audio alternative on Dstv hasa za hapa Afrika Mashariki ni Kiswahili au Kiingilishi basi walibidi wamuhoji kwa Kibantu aka Kiswahili bhana.
 
inaelekea hufatilii mpira wachezaji wengi maarufu wasiotoka uingereza wengi hawajui kiingereza kuanzia amerika kusini mpaka nchi za ulaya kama hispania,ufaransa,ujerumani,italia na ureno.
Lugha ni biashara badala ya kumlaumu tungemsifia kwa kutukuza lugha kitu ambacho hata rais na wabunge wetu wameshindwa kukifanya
 
mbona ukushangaa kwa robinho na gaucho kutokujua english na interview zao zote wanaomba kuongea kwa kireno?
 
Taifa Stars imefuzu kucheza Nusu fainali baada ya kuivurumisha Uganda, na mtu aliye teuliwa man of the Match ni Mbwana Samatta ana hojiwa na Ssport kwa kimombo akashindwa na kuomba kuhojiwa kiswahili
kwa hili la Samatta ni dhahiri shahiri wanatakiwa kupelekwa twishen ya kidhungu ili wawe realy Profeshenal

Wewe mwenyewe kindengeloeko hicho haukijui nini maana ya profeshenal.....? Tangu nidhaliwe cjwahi muona raisi wa china akiongea kidhugu.
 
Taifa Stars imefuzu kucheza Nusu fainali baada ya kuivurumisha Uganda, na mtu aliye teuliwa man of the Match ni Mbwana Samatta ana hojiwa na Ssport kwa kimombo akashindwa na kuomba kuhojiwa kiswahili
kwa hili la Samatta ni dhahiri shahiri wanatakiwa kupelekwa twishen ya kidhungu ili wawe realy Profeshenal

mbona wachezaji wengi ambao ni wakulipwa ulaya hawajui english?
 
Taifa Stars imefuzu kucheza Nusu fainali baada ya kuivurumisha Uganda, na mtu aliye teuliwa man of the Match ni Mbwana Samatta ana hojiwa na Ssport kwa kimombo akashindwa na kuomba kuhojiwa kiswahili
kwa hili la Samatta ni dhahiri shahiri wanatakiwa kupelekwa twishen ya kidhungu ili wawe realy Profeshenal

Wewe
Jamaa ni wa OVYO SANA.
 
wao ndo wamekosea mbona kuna Audio alternative on Dstv hasa za hapa Afrika Mashariki ni Kiswahili au Kiingilishi basi walibidi wamuhoji kwa Kibantu aka Kiswahili bhana.

alfanya hivo kwakuwa samatha ni international player kumbe yeye anajua comma titapeli tu kidhungu sio kiivo na mbona meya wa mombasa kaongea kibantu tu ushamba ndo unatuzuzua waafrika wa tz..
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom