Mbwana Samatta Man of the Match achemka kutema Ung'eng'e

jamani nipeni matokeo mwenzenu nipo huku Israel haifa. Sijui lolote kuhusu mechi yetu na Uganda na nipo tumbo joto kweli. Ngapi ngapi?

huku mambo yamebadilika mkuu, kutuma matkeo unachajiwa, nitumie salio nikutumie matokeo
 
Taifa Stars imefuzu kucheza Nusu fainali baada ya kuivurumisha Uganda, na mtu aliye teuliwa man of the Match ni Mbwana Samatta ana hojiwa na Ssport kwa kimombo akashindwa na kuomba kuhojiwa kiswahili
kwa hili la Samatta ni dhahiri shahiri wanatakiwa kupelekwa twishen ya kidhungu ili wawe realy Profeshenal

Kuwa really professional ni kujua english??
Dah kweli upumbav.u ni kipaji!

Lugha ni chombo cha mawasiliano tu wala sio ufahari!
 
Mwarabu naona kimbelembele kimeisha baada ya kula sita za Ghana
Sawa kaka Mavotah... Tumekubali kwa roho ya michezo !! Lakini usisahau VIKOMBE VIKUBWA VIWILI vimo ndani ya kabati !! Fundisha watoto hawa kucheza!!
AL-AHLY - MISRI bingwa African Champion
SFAXEIN - TUNIS bingwa wa African Confederation Cup
_71452102_sfaxien.jpg
 
Mbona wana JF tunasahau haraka hivi. Si kwenye mjadala wa juzi tu kuhusu kocha wa Azam kutojua Kiswahili wala Kiingereza tulikubaliana kwamba mpira una lugha moja tu? Iwe kwa maneno ya Kiswahili au Kiingereza. MS alihojiwa kwa lugha ya kimpira, akajibu kwa lugha ya kimpira. La ajabu ni lipi hapo?
 
Taifa Stars imefuzu kucheza Nusu fainali baada ya kuivurumisha Uganda, na mtu aliye teuliwa man of the Match ni Mbwana Samatta ana hojiwa na Ssport kwa kimombo akashindwa na kuomba kuhojiwa kiswahili
kwa hili la Samatta ni dhahiri shahiri wanatakiwa kupelekwa twishen ya kidhungu ili wawe realy Profeshenal

wakati watu wanajitahidi kukijua kichina Duniani, wewe unang'ang'ania Kiingereza! Jitahidi kukipenda kiswahili na kukikweza kiwe juu kama wengine wanavyofanya kwao. Usiwe mtumwa wa kifikra
 
sawa inawezekana ni mzalendo lakini jua kwamba , mtanzania yeyote akiwa anaongea kiingereza ujue angalau ukungu wa kielimu kautoa , ingawa mbele tunakoenda haita kuwa hivyo , samantha hakusoma na ndiyo hivyo

Wewe uliyesoma una kitu gani cha kumzidi Samatta?
 
Wewe uliyesoma una kitu gani cha kumzidi Samatta?
nina maarifa ingawa sina hela kama zake , hela bila maarifa usije ukamshangaa siku moja akawa maskini kupindukia , mkabaki kumshangaa tu elimu ndiyo mambo yote
 
Haya ni maswali magumu sana kwa wakenya flani kutoa jibu linaloridhisha.

cc: Jammu Africa, Dhuks, Kabaridi, Koborer, lawmaina78,

Ukitaka kuongeza upeo wako lazima ujue kuna ligi ndogo na kubwa, kama watania kufanya biashara yako na mawasiliano yako yote kijijini, lugha ya mama inafaa, kitaifa inabidi kiswahili kitumike, kimataifa ni kingereza na ikibidi kichina, kijerumani, kifaransa nk.
kusema tukuze moja sababu ya uasili ni kujidunisha.
 
Taifa Stars imefuzu kucheza Nusu fainali baada ya kuivurumisha Uganda, na mtu aliye teuliwa man of the Match ni Mbwana Samatta ana hojiwa na Ssport kwa kimombo akashindwa na kuomba kuhojiwa kiswahili
kwa hili la Samatta ni dhahiri shahiri wanatakiwa kupelekwa twishen ya kidhungu ili wawe realy Profeshenal
ningemshangaa sana kama angeshindwa kuzungumza Kiswahili, kama bado Kiswahili anakikumbuka, licha ya kuishi Lubumashi, sioni shida yoyote
 
Waswahili bwana shida sana.Mbona Kiingereza ni lugha tu kama Kigogo.Kwani kuna mchezaji wa MAN anayejua Kiswahili.Acha mawazo ya kitumwa wewe.
Taifa Stars imefuzu
kucheza Nusu fainali baada ya kuivurumisha Uganda, na mtu aliye teuliwa
man of the Match ni Mbwana Samatta ana hojiwa na Ssport kwa kimombo
akashindwa na kuomba kuhojiwa kiswahili
kwa hili la Samatta ni dhahiri shahiri wanatakiwa kupelekwa twishen ya
kidhungu ili wawe realy Profeshenal
 
Taifa Stars imefuzu kucheza Nusu fainali baada ya kuivurumisha Uganda, na mtu aliye teuliwa man of the Match ni Mbwana Samatta ana hojiwa na Ssport kwa kimombo akashindwa na kuomba kuhojiwa kiswahili
kwa hili la Samatta ni dhahiri shahiri wanatakiwa kupelekwa twishen ya kidhungu ili wawe realy Profeshenal

Watanzania bhaana je angehojiwa kwa kiswahili halafu ajibu kwa kiingereza mngekaa kimya?:usa::usa:
 
Ukitaka kuongeza upeo wako lazima ujue kuna ligi ndogo na kubwa, kama watania kufanya biashara yako na mawasiliano yako yote kijijini, lugha ya mama inafaa, kitaifa inabidi kiswahili kitumike, kimataifa ni kingereza na ikibidi kichina, kijerumani, kifaransa nk.
kusema tukuze moja sababu ya uasili ni kujidunisha.
Sawa, lakini kuna wakenya flani wanataka eti hata wakiongea na wakenya wenzao watumie kiingereza. Hata hapa jukwaani utawaona tu!
 
Kizungu sio lazima hata kwenye ligi za kama England inatokeaga wachezaji wasioongea English wanasema neno moja wanahoji mwingine na anapongezwa kama kawa na hawasemi vibaya.

Usiwe na wasi ndugu yangu weye endelea na kucheza mpira, kiingereza sio lazima labda kama unakihitaji.

Watakupa translator mambo yataendelea, hata UN wanaongeaga lugha zao kama kawa kwenye mikutano wa nchi nyingi tu. Hata maraisi kutoa hotuba.
 
Taifa Stars imefuzu kucheza Nusu fainali baada ya kuivurumisha Uganda, na mtu aliye teuliwa man of the Match ni Mbwana Samatta ana hojiwa na Ssport kwa kimombo akashindwa na kuomba kuhojiwa kiswahili
kwa hili la Samatta ni dhahiri shahiri wanatakiwa kupelekwa twishen ya kidhungu ili wawe realy Profeshenal

kimombo ni tatizo la wengi cuz sio lugha yetu,hebu msikilize huyu mhishimiwa na kimombo chake cha kuandikiwa na kukariri ndio utaelewa ukubwa wa tatizo.

Last edited by a moderator:
hata huko mazembe wanazungumza france sio ajabu yy kushindwa english
mazembe wanasema sana kiswahili na lingala kidogo,watu wa lubumbashi lugha yao ni kswahili hata hiyo lingala wanaijua wachache lakini swahili ile ya congo ndio lugha yao kuu pale,lingala ni lugha ya kinshasa ambako pia hawasemi kifaransa watu wengi,isipokuwa wachache walioenda shule ambao nao hawakitumii sana kama lingala.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom