Mbwana Samatta Man of the Match achemka kutema Ung'eng'e

Mbwana Samatta Man of the Match achemka kutema Ung'eng'e

Sawa, lakini kuna wakenya flani wanataka eti hata wakiongea na wakenya wenzao watumie kiingereza. Hata hapa jukwaani utawaona tu!

Wakenya waliosoma shule za upili na kuendelea hujieleza vizuri zaidi kwa kingereza kuliko kiswahili, tatizo tu ni kwa matamshi; hii inatokana na kingereza kuwa lugha ya lazima shuleni.

Sioni tatizo lolote la kutumia lugha ya kingereza kwa mawasiliano, kama mtu hana ufasaha wa lugha atafanyeje?
 
Kiingereza na mpira wapi na wapi?hvi mwombeki wa simba na elimu yake ya marekani anamzidi nni samatta..?kujua lugha. Katika futbal ni uamuzi wa mtu tu.. kama unajuakuucheza hata mkalimani ataletwa..

itasaidia kuepuka mikataba mibovu
 
tukubaliane iwe isiwe ung'eng'e unasaidia kuna wakti atahitajika acheze pale Ze Blues unadhani itakuwaje dimbani,
hao mnao wataja wooooote wanaudhuria kozi fupi za lugha
uko hapooo?
 
Dogo ni muungwana, amesema ukweli kuwa hafahamu vizuri Kiingereza. Kocha wa Simba Milovan alikiri mbele ya kamera ya SS9 kuwa 'my English is not good'. Former RC Kigoma Mhe. Simbakalia licha ya kukijua sana kimombo, akiwa Burundi aligoma kuhojiwa kwa Kiingereza na BBC na akatiririka kwa Kiswahili. Sote tunakumbuka Mar. Kanumba alivyojichanganya kuongea Kiingereza huko bondeni. Samatta ni mkweli, tumpongeze kwa hili.
 
Daaaah,kwahiyo kujua ki ingereza ndo nini!!mbona ni vitu viwili tofauti sana kwenye kipaji,nakumbuka mwaka jana au juzi Nadir Haroub nae alihojiwa na hao hao Super Sport,watu wakamponda sana alichoongea,na hata Ulaya wapo Professional wengi tuu hawaijui hyo lugha na hawana mpango nayo tena wapo pale pale kwa Queen but mzgo wanaopga kila mtu anawakubali#Tujikubali#

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Mbona ma star wengi tu Ulaya hawaongei kizungu?

Mwite Lionel Messi uanze nae mahojiano ya kizungu halafu ulete suggestion yako ya twisheni.
 
acha uzumbukuku,ushaona Ronaldo de Lima anaongea kiingereza???kiingereza sio issue
Taifa Stars imefuzu kucheza Nusu fainali baada ya kuivurumisha Uganda, na mtu aliye teuliwa man of the Match ni Mbwana Samatta ana hojiwa na Ssport kwa kimombo akashindwa na kuomba kuhojiwa kiswahili
kwa hili la Samatta ni dhahiri shahiri wanatakiwa kupelekwa twishen ya kidhungu ili wawe realy Profeshenal
 
Mbwana Samatta alionyesha uzalendo kwa taifa lake la Tanzania kutokubali kuhojiwa kwa kiingereza.alikitangaza kiswahili barabara!Big up MS.
 
Messi alipokuwa anachukua tuzo ya mwanasoka bora wa DUNIA,kule jiji Zurich Uswiss mbele ya watu wakubwa kibao,alitoa historia,shukrani,maoni na mambo yake mengijne yote kwa lugha ya kwao!Vivyo hivyo kwa Ronaldinho,Ronaldo de Lima, na wengine ambao dunia inawakumbuka kwa kufanya makubwa katika soka walitumia lugha yao.
Sasa leo hii katumia Mbwana Samatta lugha ya kwao unaanza kumsema na kumuona hafai.
Kumbuka huyo huyo Samatta ndio alikuwa mtanzania wa kwanza kuibuka mfungaji bora katika fainali za kombe la shirikisho barani Africa...Najivunia kuwa na mtu kama huyu katika nchi yangu.
Shame on you mtoa mada.

"Nlikuwepo":bolt:
 
kihiyo yeyote huamini kiingereza ndio kila kitu,
Kuna watu maarufu kibao hawajui hiyo lugha na wana make money na kuwasiliana kama kawa;
Koffi Olomide,cabo snoop nk mbona hawajui lkn maisha yanakwenda na umaarufu unazidi kuongezeka.
Ndio hao huwapeleka watoto wao medium school ili wajue kiingereza na si kingine.
 
Taifa Stars imefuzu kucheza Nusu fainali baada ya kuivurumisha Uganda, na mtu aliye teuliwa man of the Match ni Mbwana Samatta ana hojiwa na Ssport kwa kimombo akashindwa na kuomba kuhojiwa kiswahili
kwa hili la Samatta ni dhahiri shahiri wanatakiwa kupelekwa twishen ya kidhungu ili wawe realy Profeshenal
haya ndio matatizo tunayo kuna kosa mtu atake aongee kiswahili? Lugha zetu zinatushinda kurukia ya watu wakati huijui usilazimishe sana ongea yako MWANANYAMALA weeeee! Sio tusi chunguza ujue maana yake.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom