Mbwa atelekezwa na mkoba wake Uingereza

Mbwa atelekezwa na mkoba wake Uingereza

Herbalist Dr MziziMkavu

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
43,092
Reaction score
34,902
150106142225_scottish_dog_640x360_spca_nocredit.jpg


Watetezi wa wanyama wameonywa watu kutowafuga wanyama makwao wakati hawawezi kuwatunza.

Shirika moja la kutetea wanyama nchini Uingereza linamtafuta mmiliki wa Mbwa aliyepatikana akiwa ametelekezwa katika kituo cha treni nchini Scotland.

Inaarifiwa Mbwa huyo alipatikana akiwa ametelekezwa na vitu vyake ndani ya mkoba uliokuwa kando yake.
Jibwa hilo dume aina ya (Shar-Pei), lilipatikana wiki jana likiwa limefungwa kwa mnyororo katika chuma kimoja ndani ya kituo hicho.

Kando yake ulikuwa mkoba ambao ndani yake kulikuwa na mto wa kulalia wa mbwa huyo, kifaa chake cha kuchezea, bakuli alilokuwa anatumia kwa chakula pamoja na chakula chake.

Shirika hilo la kutetea maslahi ya wanyama, limewaonya wamiliki wa wanyama kutowatelekeza wanyama wao likisema ni hatia na pia kuwasahi watu kutowanunua wanyama kama vile Mbwa kwa sababu ya kutaka kuonekana tu kuwa na Mbwa nyumbani kwao.


Chanzo:
BBC
 
wenzetu walisha endelea sana yani mbwa ametelekezwa tu inatangangazwa dunia nzima imeonekana ajabu sana wakati ss huku kwetu kawaida ss kufikia huko sio leo labda miaka 150 mbele
 
Ilo shirika la kutetea haki za wanyama siku wakijichanganya kukanyaga Iringa watapata kichaa maana uyo ana hadi mto wa kulalia na begi weeeeee duh.
 
He looks so sad jamani. Kweli mmiliki amefanya kosa, aadhibiwe. The dog looks so sad and in a deep depression ::thumbdown:
 
Ilo shirika la kutetea haki za wanyama siku wakijichanganya kukanyaga Iringa watapata kichaa maana uyo ana hadi mto wa kulalia na begi weeeeee duh.

PETA Wakienda Iringa serikali yetu yote itashitakiwa!
 
Back
Top Bottom