Watoto wake walishasema kuwa, wakati wa kulala wakishafunga milango, mlinzi huwafungulia. Alfajiri sana, huwafungia bandani. Hao mbwa walikuwa hawamfahamu!
Yote kwa yote, kwa mchango wake kwa Nchi hii, si yeye, wala mke wake tiba zao zingeishia Muhimbili tu! Serikali ingepaswa kuwatafutia tiba hata nje ya Nchi! Na si hivyo tu, hata bendera ya taifa, ilipaswa imlilie kwa nusu mlingoti, hata kwa siku moja, kama si tatu!
Tusilione hili ghorofa ( Tanzania) limesimama hivi, wapo waliojitolea kulijenga!
Kuwa nje ya KIJANI, si sababu ya kunyimwa haki yake!