Kowalski
JF-Expert Member
- Jun 25, 2011
- 348
- 111
- Thread starter
- #21
Kuna Mh.Mkuchika akimtaka Mkosamali afute kauli yake ya kulikebehi jina la Mh.Rais wakati akijadili ofisi ya Rais.Mh. Mkosamali hakutaja jina la Mh.Kikwete kabisa,bali ametaja jina la Taasisi yaani Rais.Mwenyekiti akimtaka mkosomali afute lakini kwa hoja alizozitoa mkosamali mwenyekiti alishindwa.
Mkosamali>> Kwanini Taasisi mbalimbali ziwe chini ya Rais? Kwanini TAKUKURU iwe ofisi ya Rais na isiwe chini ya Waziri Mkuu Hizi Taasisi za Ofisi ya Rais ndio zina njaa kwelikweli.. ukiona TAKUKURU inafeli maana yake Rais hana utashi wa kisiasa wa kupambana na Rushwa.. Awamu ya nne imeshindwa kupambana na Rushwa, mnakusanya kodi hamna uwezo wa kutekeleza vitu hivi >> Mbunge Felix Mkosamali.
Akasimama Waziri Mkuchika >> Kwa mujibu wa kanuni inayosema Mbunge hatotumia jina la Rais kwa dhihaka katikka mjadala au kwa madhumuni ya kulishawishi Bunge.. Mkosamali ameeleza Rais hana utashi wa kisiasa wa kupambana na Rushwa.. Kiustaarabu afute tu hiyo kauli>>
Mkosamali akaendelea >> Nitafutaje wakati ndio hali halisi.. Juzi Katibu Mkuu amesafisha watu.. Kesi zote zikichunguzwa DPP anazifuta mbona yako wazi>>
Akasimama Mbunge Innocent Sebba >> Niwashukuru Mawaziri wanaohusika na Ofisi ya Rais.. Pamoja na kelele zinazopigwa hawa wenzetu tunawaita ni wapiga debe sio wasafiri.. Wanaosafiri
Baadae akapata nafasi Waziri Mark Mwandosya >> Hoja ya leo inamzungumzia Ofisi ya juu kabisa katika nchi.. unapokizungumzia chombo hiki kipe heshima inayohitajika.. Huwezi ukamzungumzia Rais kama unavyomzungumzia Mbunge wa Rungwe>>