Mbunge wetu John Mnyika thubutu utatue kero ya maji jimboni mwako!

kwanini aliwadanganya wananchi?. Why?!!.

Aliwaambia wananchi wake atalimaliza tatizo la maji. Atalimaliza vipi, kama sio jukumu lake!

Alijuwa kuwa angeweza kuifuatilia serikali itekeleze majukumu yake lakini kumbe serikali yenyewe imeweka big G masikioni.
 
Alijuwa kuwa angeweza kuifuatilia serikali itekeleze majukumu yake lakini kumbe serikali yenyewe imeweka big G masikioni.

Mkuu unaloongea ni sahihi, hao wengine wasikutoe kwenye mstari. Pamoja na utoaji wa ahadi utekelezaji unaendana na utashi zaidi ambao kuna post mdau kaonyesha jinsi hatua za Mnyika zilipopitia na zilipokwamia japo kwa plan A, so tusubiri plan B ya mbunge! Lakini kuna suala la katiba, nalo ni la msingi,.
Nadhani hlo ndilo unalolisisitiza kaka.
 
Hivi afanye nini tofauti na ufuatiliaji tu! yale maandamano yasiyo rasmi na madiwani wote kwenda dawasa ni moja katika hatua alizochukua hata miaka miwili hajapita mmeanza kumuhukumu? kuna mradi gani wa maji unaweza kuisha ndani ya mwaka mmoja.
 
Jamani, mnataka kunambia wananchi wote wa Ubungo ndo waende kwa mwandosya? Nini maana ya mbunge au mwakilishi wa wananchi? Na km ilikuwa kazi ya mwandosya kuangalia kero za wanaubungo incliuding hiyo ya maji, ilikuweje mnyika aliweke hilo ktk kitabu chake cha ahadi?
 
Hivi afanye nini tofauti na ufuatiliaji tu! yale maandamano yasiyo rasmi na madiwani wote kwenda dawasa ni moja katika hatua alizochukua hata miaka miwili hajapita mmeanza kumuhukumu? kuna mradi gani wa maji unaweza kuisha ndani ya mwaka mmoja.
Mbona nyie mnadai Dubai yenu huko Kigoma?
 
Tatizo la watanzania ni wepesi wa kuamini, hivi leo wakiambiwa mabomba yote yatatoa juice ya passion basi watu watatayarisha madrum.
 
Alijuwa kuwa angeweza kuifuatilia serikali itekeleze majukumu yake lakini kumbe serikali yenyewe imeweka big G masikioni.

Mwita ukweli unabaki pale pale MNYIKA katupiga changa la macho wana UBUNGO badala ya kujikita kwenye hoja zenye mvuto kwa wapiga kura wake yeye AMEJIKITA kudai masuala ya kitaifa zaidi kama siyo kushabikia maandamano ya CDM.

Mnyika litoa ahadi tema peupe, mchana wakati wa kampeni kuwa: MKINICHAGUA, JIMBO LA UBUNGO TATIZO LA MAJI LITAKUWA HISTORIA. Sasa leo wala hajafanya lolote, yeye kazi yake kufukuzia mshiko wa vikao vya kamati za bunge. Pia anatumia muda mrefu akiwa jimboni kiuzunguka huku akipewa majungu na wana magwanda.
 
kwanini aliwadanganya wananchi?. Why?!!.

Aliwaambia wananchi wake atalimaliza tatizo la maji. Atalimaliza vipi, kama sio jukumu lake!
Kweli kazi tunayo, naomba nitoe ufafanuzi ufuatao;
1) Mnyika aligombea huku akitarajia kuwa sisi chadema bila uchakachuaji wa wazi tungechukua manispaa ya kinondoni ili tupange vipaumbele kulingani na ilani ya chadema na vipaumbele vya Mbunge. CCM wamchukua manisipaa, bajeti ya majoho ya madiwani ktk kitabu cha bajeti ya manisipaa ni Tsh Bil 1.2. Kaangalie maji imepewa sh ngapi? Uone aibu. Mnyika angefanya nini wakati chadema haikusanyi kodi?

2) Imeshaelezwa kuwa Kongamano la maji liliitishwa na Mbunge, CCM wakalihujumu, si tu kwamba dawasco hawakuja lakini hata wadau wengine muhimu au viongozi wa serikali wahusika hawakuja. Angefanya nini?

3) Mimi nawashangaa sana ccm, wanauwezo mdogo sana wa kufikiri nadhani. Wanadhani kwamba wakimhujumu mbunge mwaka 2015 ataanguka. Wanasahau kwamba kati ya mwaka 1995 na 2000 walimhujumu Dr Slaa kupitia madiwani wao wengi. Mwaka 2000 Dr Slaa akawaambia ahadi zangu zote zimehujumiwa na madiwani. Karatu wakamchagua Dr Slaa na madiwani wengi sana wa Chadema.Ahadi za Chadema zikatekelezwa, Mpaka kesho ccm haitarajii kurudi karatu. Subiri mwaka 2015 ubungo. Tutashinda kwa kishindo zaidi.
 
Kweli kazi tunayo, naomba nitoe ufafanuzi ufuatao;
1) Mnyika aligombea huku akitarajia kuwa sisi chadema bila uchakachuaji wa wazi tungechukua manispaa ya kinondoni ili tupange vipaumbele kulingani na ilani ya chadema na vipaumbele vya Mbunge. CCM wamchukua manisipaa, bajeti ya majoho ya madiwani ktk kitabu cha bajeti ya manisipaa ni Tsh Bil 1.2. Kaangalie maji imepewa sh ngapi? Uone aibu. Mnyika angefanya nini wakati chadema haikusanyi kodi?

2) Imeshaelezwa kuwa Kongamano la maji liliitishwa na Mbunge, CCM wakalihujumu, si tu kwamba dawasco hawakuja lakini hata wadau wengine muhimu au viongozi wa serikali wahusika hawakuja. Angefanya nini?

3) Mimi nawashangaa sana ccm, wanauwezo mdogo sana wa kufikiri nadhani. Wanadhani kwamba wakimhujumu mbunge mwaka 2015 ataanguka. Wanasahau kwamba kati ya mwaka 1995 na 2000 walimhujumu Dr Slaa kupitia madiwani wao wengi. Mwaka 2000 Dr Slaa akawaambia ahadi zangu zote zimehujumiwa na madiwani. Karatu wakamchagua Dr Slaa na madiwani wengi sana wa Chademoaa.Ahadi za Chadema zikatekelezwa, Mpaka kesho ccm haitarajii kurudi karatu. Subiri mwaka 2015 ubungo. Tutashinda kwa kishindo zaidi.

We bwana ni mmoja wa watu mnaompotosha mbunge wetu. Usilete utetezi usio na tija juu ya kushindwa kutekeleza ahadi ambazo mlizitoa kwa wananchi. Tunashukuru siku hizi umehama Ubungo hivyo ushauri wako kwa mheshimiwa umepungua!!. Tuwe wawazi MHESHIMIWA MNYIKA JIMBO analiweka rehani; kuna kila dalili atashindwa kulikomboa 2015. Sie wenye nia nzuri na mbunge tunamkumbusha akae kitako na kurejea ahadi zake ikibidi arudi tena kwa wapiga kura atueleweshe kwanini hajatekeleza hata AHADI moja.
 
Jamani,

Hebu tuwe wakweli, Mnyika ndo kwanza tuseme anamaliza mwaka mmoja tangu achukue jimbo la Ubungo. Leo tayari kuna wadau wanataka tatizo la maji liwe limeisha!!???. Hii ni ajabu sana.

Miaka yote CCM wamekuwepo wameshindwa kulimaliza leo mnataka ndani ya mwaka 1 mh Mnyika awe amemaliza hili tatizo sugu.!!.Jamani tumpe muda basi angalau nusu ya kipindi chake ndiyo tuweze kumpima. Sasa hivi mambo bado hayajatulia kihivyo. Kumbuka ccm walipinga ushindi wake mahakamani, hivyo haya ni kati ya mambo yanayomchukulia muda wake wa ku deal na kero za wananchi.

Mwambieni huyo mama akafute kiyo kesi mahakamani, vinginevyo Mh Mbunge anachukua muda mwingi kufikiria hiyo kesi isiyokuwa na ushahidi.
 
MWANANCHI
Pamela Chilongola

BAADHI ya wananchi wa Ubungo katika Manispaa ya Kinondoni, jana wavamia Ofisi za Kampuni inayosambaza maji katika Jiji la Dar es Salaam na baadhi ya maeneo ya Mkoa wa Pwani (Dawasco), kulalamikia kukosa huduma za maji. Katika tukio hilo, wananchi hao waliongozwa na mbunge wao John Mnyika na kwa mujibu wa maelezo yao, hatua hiyo ilikuja baada ya kampuni hiyo kutowapa majibu kuhusu malalamiko ya kukosa huduma .

Walisema miezi nane iliyopita, waliiandika kampuni hiyo kutaka kujuia sababu za wao kukosa huduma za maji katika maeneo yao, lakini hawakujibiwa. Mmoja wa wananchi hao Msafiri Shabani wa Mabibo, alielezea kushangazwa kwake na hatua ya wananchi katika eneo hilo kukosa maji wakati huko nyuma walikuwa wanapata huduma.

“Huko nyuma tulikuwa tunapa huduma angalau wiki mara tatu lakini kwa sasa tunapata mara moja na yanafunguliwa kwa saa mbili tu, nadhani kuna mchezo fulani unafanyika, ili tukosema maji,” alisema. Akijibu tuhuma hizo Mkurugenzi Mtendaji wa Dawasco, Mhandisi Jackson Midala alikiri ofisi yake kupokea malalamiko ya wananchi hao kuhusu kukosa huduma ya maji, lakini alisema hiyo inatokana na upungufu wa maji yanayohitajika.

Alisema si kweli kwamba Dawasco inashirikiana na watu wanaodaiwa kuuza maji na hivyo wakati mwingine kukuta wakiwafungia watu mabomba ili wafanye biashara.

Kuhusu suala la mabomba maarufu ya kichina ambao ni mradi uliotekelezwa na Wachina, alisema ni kweli baadhi ya sehemu hayatoi maji, lakini wanakwenda hatu kwa hatua ili hatimaye waweze kutoa huduma za ukakika.. Hata hivyo alisema hawezi kuzungumzia tuhuma zilizotolewa na wananchi hao dhidi ya meneja wa Dawasco Boko, lakini akasema kwamba inabidi azifanyie kazi .

Kuhusu mgawo wa maji alisema hauepukiki kwani wakati mwingine wanaamua kufanya mgawo wa maji mfano Manzese siku tatu ili wengine pia wapate mwisho
---------------------------------------
 
Mnyika aandaa kongamano la maji Ubungo

na Edward Kinabo

Mbunge wa Jimbo la Ubungo, John Mnyika, ameandaa kongamano la maji katika jimbo hilo ambalo limepangwa kufanyika Januari 31 mwaka huu katika ukumbi wa Chuo cha Maji Rwegarulila (Water Resource Institute) kilichoko katika Manispaa ya Kinondoni.

Kongamano hilo litakuwa na mada kuu mbili, moja ni sheria na mikakati ya sekta ya maji safi na maji taka- fursa na changamoto kwa wananchi wa Jimbo la Ubungo na mada ya pili ni hali halisi ya upatikanaji wa maji jimbo la Ubungo na wajibu wa wadau mbalimbali katika kukabiliana na upungufu wa maji.

Takriban wadau 300 wanatarajiwa kushiriki kongamano hilo linalolenga kujadili hatua zinazoweza kuchukuliwa katika kukabiliana na kero zinazohusu sekta hiyo katika muda mfupi, muda wa kati na muda mrefu.

"Jimbo la Ubungo lina rasilimali zote muhimu za kuwezesha kukabiliana na matatizo ya maji; mabomba makuu ya maji yanapita jimboni humu, Wizara ya Maji ina ofisi zake katika jimbo hili na Chuo cha Maji kiko kwenye jimbo hili; huu ni wakati muafaka wa kuunganisha nguvu za pamoja katika kuondokana na kero hiyo, kongamano hilo litatupa mwelekeo na kuhamasisha ushirikiano wa wananchi na wadau wote," alisema Mnyika.

Katika kongamano hilo mbunge huyo, viongozi mbalimbali na DAWASCO watapata fursa pia ya kuwasikiliza wananchi na kutoa majibu kuhusu kero mbalimbali katika sekta ya maji.

Mnyika alitoa wito kwa wananchi wa jimbo hilo na wadau wengine wa sekta ya maji walioko katika Mkoa wa Dar es salaam kujitokeza kushiriki kongamano hilo kwa kuthibitisha kushiriki kupitia Ofisi ya mbunge huyo.
 
Mbunge awataka DAWASCO kutoa maelezo kuhusu kero ya maji
MBUNGE AWATAKA DAWASCO KUTOA MAELEZO KUHUSU HATUA AMBAZO WAMEZICHUKUA KATIKA KUSHUGHULIKIA MATATIZO YA UPATIKANAJI WA MAJI KATIKA MAENEO MBALIMBALI YA JIMBO LA UBUNGO

Mbunge wa Ubungo, John Mnyika ameandikia barua Kampuni ya Maji Safi na Maji taka Dar es salaam (DAWASCO) kuwataka kutoa maelezo kuhusu hatua ambazo wamezichukua katika kushughulikia matatizo ya upatikanaji wa maji katika maeneo mbalimbali ya jimbo la Ubungo.

Mnyika amesema kwamba iwapo DAWASCO haitatoa maelezo mapema ataeleza hatua za kibunge ambazo atazichukua ili kuhakikisha kampuni hiyo inatimiza wajibu wa kushughulikia kero ya maji katika kata mbalimbali za jimbo hilo.

Ifuatayo ni nukuu ya baadhi ya maelezo yaliyo katika barua ya Mbunge kwa DAWASCO:
"Tarehe 19 Januari 2011 niliiandikia barua ofisi yako yenye kumbu. Na. OMU/ MJ/004/2011 kuwaalika DAWASCO kuja kushiriki na kutoa mada katika Kongamano la Maji Jimbo la Ubungo; hata hivyo hakuna mtendaji yoyote toka ofisi yako aliyefika kutimiza wajibu husika wala barua tajwa kujibiwa.

Tarehe 15 Machi 2011 niliandika tena barua kwa ofisi yako kuwasilisha Ripoti ya Kongamano husika na kutoa mwito kwa hatua kuchukuliwa; hata hivyo ofisi yako mpaka sasa haijaeleza hatua ambazo imechukua au walau kutambua kupokea ripoti husika.
Tarehe 27 Februari 2011 na tarehe 6 Machi 2011 nilifanya mikutano na wananchi katika kata ya Goba kuhusu maji; pamoja na kuwa mradi katika eneo hilo uko chini ya wananchi vielelezo vilitolewa vya malalamiko ya muda mrefu kutaka hatua kuchukuliwa na DAWASCO kuhusu uharibifu wa mita na pia mapendekezo ya kutaka huduma katika eneo husika kutolewa na DAWASCO moja kwa moja.

Tarehe 26 Machi 2011 nilifanya ziara kata Kata ya Makuburi katika Mitaa ya Makoka, Muongozo na Kibangu na kubaini kwamba wananchi wa maeneo husika wamekuwa na ukosefu wa maji kwa miezi kadhaa hata katika maeneo ambayo hapo awali yalikuwa yakipata maji na hivyo kutoa mwito kwa DAWASCO kuchukua hatua za haraka.

Tarehe 7 Mei 2011 nilifanya ziara kata ya Kimara na kubaini kwamba ujenzi wa visima katika mitaa iliyoanishwa na DAWASCO kwa mujibu wa ahadi ya Rais Kikwete ya tarehe 24 Mei 2010 haujakamilika kwa maeneo mengi.

Tarehe 8 Mei 2011 nilifanya ziara katika kata za Mbezi na kubaini upungufu mkubwa wa maji wakati kukiwa na upotevu wa maji katika maeneo ya Msigani.

Tarehe 22 Mei 2011 nilifanya ziara katika kata za Mabibo na Manzese na kubaini ukosefu wa maji katika maeneo ambayo yalikuwa yakipata maji awali ikiwemo upungufu wa maji katika magati ya DAWASCO.

Tarehe 29 Mei 2011 nilifanya ziara kata ya Saranga na kubaini malalamiko ya muda mrefu ya wananchi kuhusu kero ya maji ikiwemo kutokujulikana ama kutokufuatwa kwa ratiba ya mgawo wa maji.

Aidha katika kipindi husika nimepokea barua toka wateja na wananchi kuhusu maombi mbalimbali ambayo wameyawasilisha kwenu bila hatua stahiki kuchukuliwa au walau kupatiwa majibu kwa ukamilifu.

Mathalani maombi ya kuunganishiwa maji ya wananchi wa eneo la Burula (katika barabara ya Kimara Suca kuelekea Golani- barua yao ya tarehe 9 Agosti 2010), Mbezi Msakuzi (Hatua za utekelezaji baada ya barua ya DAWASCO/WSP/187/Vol III/42 ya 25/03/2009; Wananchi wa Msigani kwa ajili ya Wakazi wa kwa Mjanja ( Barua ya S/M/MSG/KN/001/2011 ya tarehe 10/01/2011 ambayo ilieleza mapendekezo yao mahususi kuhusu hatua zinazopaswa kuchukuliwa na kuomba mkutano kati yao na DAWASCO ili kujadili maombi yao), Wananchi wa Malambamawili (kwa barua yao SM/MSG/MWL/KN/DWSC/02/2011 ya tarehe 3/2/2011).

Naelewa kwamba utatuzi wa kero ya maji katika Mkoa wa Dar es Salaam ikiwemo jimbo la Ubungo unahitaji hatua za muda mrefu, muda wa kati na muda mfupi. Hata hivyo, zipo hatua ambazo zingeweza kuchukuliwa kwa haraka kuhusu mapendekezo yaliyotolewa na wananchi katika Kongamano na pia maombi ambayo yamewasilishwa DAWASCO bila kupatiwa majibu yoyote.

Nataka kupatiwa maelezo kuhusu shughuli ambazo zimetekelezwa na DAWASCO katika kipindi cha kuanzia mwezi Januari 2011 mpaka Mei 2011 katika kuboresha upatikanaji wa maji kwenye maeneo mbalimbali ya jimbo la Ubungo ikiwemo kuelezwa hatua mahususi ambazo zimechukuliwa kufuatia ripoti ya Kongamano na barua za wananchi."

Pamoja na kuwa zipo hatua ambazo zimefanyika katika kupunguza kero ya maji katika maeneo kadhaa ya Jimbo la Ubungo kufuatia Kongamano la Maji lililoitishwa na Mbunge tarehe 31 Januari, 2011; bado hali kwa ujumla wake hairidhishi suala ambalo limemfanya Mbunge kutaka maelezo ya kina kutoka DAWASCO kama sehemu ya kutimiza wajibu wake wa kusimamia serikali.
 
Mchango wangu Bungeni kuhusu Mpango
MCHANGO WANGU BUNGENI TAREHE 14 JUNI WAKATI WA KUJADILI RASIMU YA MPANGO WA TAIFA WA MIAKA MITANO

MHE. JOHN J. MNYIKA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa nafasi hii ya kuwasilisha mapendekezo ya mabadiliko ya kwenye Mpango kwa mujibu wa Kanuni ya 57 na Kanuni ya 58 ya Bunge.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mujibu wa Katiba yetu, Ibara ya 63, Bunge ndiyo chombo kikuu kwa niaba ya wananchi chenye wajibu wa kuishauri na kuisimamia Serikali na katika kutekeleza wajibu huu, Ibara ndogo ya (3) inatamka kwamba, kazi mojawapo ni kujadili na kupitisha mipango ya muda mfupi na muda mrefu na huu ndiyo wajibu tulionao mbele hivi sasa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitajielekeza kwenye maeneo mahususi ambayo nimewasilisha mabadiliko ambayo nitaomba yazingatiwe kwa mujibu wa Kanuni ya 57 na 58 kwenye hoja iliyo mbele yetu. Kwanza ni eneo ambalo liko ukurasa wa 117 wa nyaraka hii wa mpango wa miaka mitano. Hili ni eneo linalohusu miradi ya maji, sababu ya kuwasilisha mabadiliko haya ni kwamba huko nyuma kumekuwepo na miradi ya maji ikiwemo miradi mbalimbali katika Jimbo ambalo wamenituma kuwawakilisha la Ubungo. Miradi ambayo ilihusisha ulazaji wa mabomba ambayo yanajulikana zaidi kama mabomba ya Wachina, lakini pamoja na mabomba kuwekwa kwa muda mrefu, wananchi wa maeneo mengi sana ukienda King'ong'o, Mbezi, Mavurunza, Makoka na kwingineko. Serikali imetumia pesa nyingi sana ikiwa kiasi kikubwa ni mkopo kutoka Benki ya Dunia, lakini maji hayatoki.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa hapa kuna mpango ambao unalenga kuchangia katika kurekebisha kasoro zilizotokea kipindi cha nyuma, lakini mpango wenyewe kama ukiachwa kama ulivyo utarudia kasoro za kipindi cha nyuma na kasoro kubwa iliyoko kwenye mpango huu ni kwamba ukitazama kwenye hilo jedwali la miradi hii ya maji ya Ruvu juu, Ruvu chini pamoja na ujenzi wa mabwawa Kidunda na visima Kimbiji na Mpera ambayo yangeongeza vilevile uzalishaji wa maji Dar es Salaam, yamegawanywa rasilimali zake katika kipindi cha miaka mitano. Kwa hiyo, ukianza utekelezaji mpaka utakapokamilika, kitakachotokea ni kama kinachoendelea sasa Ubungo, mradi wa mabomba wa Benki ya Dunia umewekwa, maji hayafiki, mabomba yameanza kuharibika, miundombinu imeanza kuharibiwa kwelikweli.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa nafahamu, ndani ya Baraza la Mawaziri, ndani ya Serikali, baada ya mijadala ya umma na sisi kule Ubungo tulifanya kongamano la wananchi la maji, Serikali ikaamua kwamba miradi hii ya Ruvu juu, Ruvu chini, ujenzi wa bwawa Kidunda na visima Kimbiji, Mpera ikamilike kwa ukamilifu wake ifikapo mwaka 2013 na Serikali kwa maana ya Rais akatoa kauli, Waziri wa Maji akatoa kauli hadharani, sasa kilichopo kwenye mpango, kinapingana na Kauli ya Waziri na Rais ya kumaliza miradi hii ifikapo mwaka 2013.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mapendekezo yangu ya mabadiliko kwenye kifungu hiki ili kurekebisha hii hali, rasilimali zilizotengwa hapa kwa mwaka wa fedha 2014/2015 na mwaka wa fedha 2015/2016 zipunguzwe bila kuathiri jumla, zirudishwe nyuma kwenye miaka mitatu ya kwanza na nimewaeleza kwenye mapendekezo ambayo Wabunge mnayo nakala yake, kiwango cha pesa kinachopaswa kuhamishwa ili miradi ikamilike kwa wakati kuepusha hasara kama iliyoko hivi sasa kutokana na mradi wa mabomba ya Wachina na ili kutimiza kauli ya Rais na Waziri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kinyume cha mapendekezo haya ni kutengeneza bomu lingine la wakati la kutumia rasilimali nyingi sana, lakini mradi ukachukua miaka mingi kukamilika, miundombinu ikaanza kuharibiwa kabla hata maji kuanza kupatikana. Kwa hiyo, naomba Waheshimiwa Wabunge hii ni kauli ya Mheshimiwa Rais, Waziri na Wabunge. Humu kuna Wabunge wa Majimbo mbalimbali ili si kwa ajili ya Jimbo la Ubungo tu, kuna Wabunge wa Mkuranga, Kigamboni, Wabunge wote wa Dar es Salaam na Wabunge wa maeneo mbalimbali ambao wanaamini katika usimamiaji wa kauli hizi kwa ukamilifu wake. Kwenye eneo hili nitaomba niishie hapa nihamie eneo lingine la mabadiliko ninayoyapendekeza. Hili lilikuwa linahusu ukurasa wa 147 kifungu cha A.1.4 ambacho kinahusiana na Kifungu cha 3.4.4 cha Mpango.

Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo la pili liko ukurasa wa 127 ambao ni kifungu cha A1.2.2 ambacho kinatokana na Kifungu cha 3.4.1.1 cha kuhusiana na kupunguza foleni Dar es Salaam. Kwa mujibu wa Mpango huu, yale mapendekezo ambayo wadau wamekuwa wakiyatoa na tumekuwa tukiyatoa kwa muda mrefu kwamba ili kupunguza foleni Dar es Salaam, lazima kuwekeza sana kwenye barabara za pembezoni. Humu kuna barabara zimeingizwa, mapendekezo yale yamekubalika, barabara ya kutoka Goba mpaka Mbezi, Mbezi Malambo Mawili mpaka Kinyerezi, Changanyikeni kwenda Chuo Kikuu kupitia Msewe na nyinginezo. Kabla sijasema pendekezo mahususi ambalo liko hapa kuhusiana na hii barabara nyingine, niombe tu katika kutekeleza Mpango huu ili jambo liharakishwe kwa haraka sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna tatizo kubwa litalikumba jiji la Dar es Salaam wakati wa utekelezaji wa mradi wa mabasi yaendayo kasi utakapoanza. Barabara ya Morogoro itakapoanza kutengenezewa njia maalum ya mradi wa mabasi yaendayo kasi, foleni ambayo itakuwepo kwenye barabara ya Morogoro, itakuwa ni foleni ya kihistoria kwa sababu barabara ni nyembamba lakini kutaanza construction pale.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, maamuzi ya kujenga barabara za kuchuja magari, barabara ya kutoka External kupitia Kilungule mpaka Kimara na nyinginezo inabidi yaharakishwe, naelewa kwamba hizi barabara zote zimeshafanyiwa upembuzi yakinifu, nipendekeze katika utekelezaji tathmini ya fidia ufanyike haraka ili zoezi lifanyike haraka kabla ya kuanza kwa ujenzi wa mabasi yaendayo kasi. Lakini kuna hoja mahususi iko hapa mbele ya barabara hii ambayo naomba iingizwe kwenye schedule, barabara ya kutoka Kimara kwenda Mavurunza mpaka Bonyokwa mpaka Segerea. Hii barabara ni muhimu iingizwe kwenye schedule hii niliyoisema ya barabara, katika ukurasa wa 127, kuna orodha ya barabara na hii barabara haipo, iingizwe kwa sababu ni ahadi ya Rais ya tarehe 24 Mei 2010 alivyokwenda kutembelea Mavurunza na alisema kwamba barabara hii ndani ya miaka mitano itajengwa kwa kiwango cha lami ili kupunguza foleni.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa isipokuwepo kwenye mpango wa miaka mitano maana yake ni kwamba hii ahadi itakuwa ni ahadi hewa. Sasa ninachosema tu hapa ni kwamba, wengine wanachambua, wanasema ahadi zote za ujumla za Rais zinafikia takriban trilioni 95, sasa hizi za hapa jumla ni trilioni kama 42 plus. Sasa ili kupunguza ule mzigo wa lawama kwamba kuna ahadi nyingi ambazo haziko kwenye Mpango, naomba kutoa pendekezo hapa kwa mabadiliko kwamba barabara hii ya kutoka Kimara kupitia Bonyokwa mpaka Segerea ambayo itaunganisha Majimbo haya mawili na kupunguza foleni iingizwe kwenye hii orodha kama ambavyo nimewasilisha kwenye jedwali la mabadiliko.

Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo lingine ni suala la nishati, Kifungu cha 3.4.1, kuna mambo mengi ambayo tungeweza kuzungumza kuhusu nishati, lakini hapa kuna pendekezo mahususi sana kwenye ukurasa wa 135, kwenye ile miradi ya umeme. Kuna mradi mmoja ambao Mheshimiwa Rais aliuzungumza Bungeni na baadaye aliuzungumza alipotembelea Wizara na baadaye kukatangazwa kuundwa Kamati ya kushughulikia mradi huo, mradi wa Stigler's Gorge, lakini mradi huu pamoja na kutangazwa kwamba ndani ya miaka hii mitano utekelezaji wake unaanza, mradi huu kwenye miradi ya umeme inayozungumzwa haupo kwenye orodha ya miradi. Kwa hiyo, mabadiliko ninayoyapendekeza hapa ni kwamba, kwa ajili ya uzalishaji mwingi wa umeme wa Taifa letu na huu ni mradi mkubwa sana utekelezaji wa mradi huu, maandalizi yake ya kirasilimali na kifedha uingizwe ndani ya mpango huu wa miaka mitano ili tuweze kuhakikisha kwamba mradi huu unatekelezwa kwa wakati.

Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo lingine ni ukurasa wa 112, mabadiliko mahususi yanahusiana na uzalishaji, manufacturing ya Kifungu 3.4.3, lakini hapa narejea kifungu 1.12, kwanza nashukuru kwamba concept ya Special Economic Zone imeingizwa kwenye Mpango. Nitaomba tu katika utekelezaji wake huko nyuma tumewahi kuwa na mipango ya kuanzisha viwanda, tukiondoa hivi viwanda ambavyo vina motisha maalum na Ubungo ni moja kati ya maeneo ambayo yalikuwa industrial area yaani ukizungumza kuhusu viwanda vya Dar es Salaam unazungumza UFI, uzalishaji wa Zana za Kilimo, unazungumza Ubungo Maziwa, uzalishaji wa maziwa, Ubungo Garment, Urafiki na kadhalika lakini viwanda vile vingi vimefungwa, vingine vinafanya biashara tofauti, hatimaye watu wanakosa ajira. Sasa wakati tunafufua vile viwanda tumeanzisha mkakati mwingine wa maeneo maalum ya viwanda likiwemo hili la Benjamin Mkapa Special Economic Zone lililopo pale Mabibo na kule kuna viwanda vinakusudiwa kuanzishwa. Sasa naomba, vitakapoanzishwa vichangie kwenye ajira lakini tufufue viwanda vile vile vilivyokufa ndani ya Jimbo la Ubungo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini hapa kuna hoja mahususi sana ambayo naomba izingatiwe ni sehemu ya 1.1.2 ambapo ndani ya Mpango huu inakusudiwa kama sehemu ya Benjamin William Mkapa Special Economic Zone kujenga bomba maalum la mtaro kutoka eneo la viwanda kupeleka kwenye mabwawa ya kumwaga uchafu yaliyoko pale Mabibo yanaitwa Mabibo oxidization ponds. Sasa naomba hili pendekezo lizingatiwe, hii hoja ni hoja hatari sana. Kwa sababu kwa mtu anayefahamu jiografia ya Dar es Salaam, mabwawa yale ya Mabibo yameshazusha zogo sana kutokana na uchafuzi wa mazingira usio wa kawaida. Sasa hii ni waste ya kawaida tu imezusha zogo, fikiria uwe na eneo la viwanda lenye viwanda zaidi ya kumi, halafu industrial sewage ijengewe bomba lipeleke kwenye mabwawa ambayo yako katikati ya community ya watu ni janga litakalokuja kutokea baadaye.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Sasa hoja yangu ninayopendekeza hapa ni kwamba, mabadiliko yafanyike kwenye hiki kifungu na nimeandika text ya Kiingereza sitasoma kwa Kiingereza iingie kwenye rekodi rasmi kwa sababu ni nyaraka rasmi, lakini hoja yangu ni kwamba huu mtaro wa maji machafu uelekezwe, uungane na sewage system inayo-service viwanda badala ya kupelekwa Mabibo oxidization ponds na kwa kiwango cha pesa kilichotengwa technicalities, tutazungumza baadaye, ni jambo ambalo linawezekana ili kuepusha hiyo hatari ya baadaye.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa hivi kwenyewe kuna uchafuzi mkubwa wa mazingira kwenye mto unaoitwa Mto Ubungo pale eneo la Kisiwani kutokana na uchafu wa majitaka kutoka Hosteli za Mabibo kuishia njiani na kumwagwa mtoni badala ya kumwagwa kwenye mabwawa kwa sababu ya huo udhaifu wa mtandao wa sewage system. Kwa sasa kama hali iko hivyo, je, itakuwaje kama industrial waste ikienda kuelekezwa kwenye eneo kama hilo?

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sababu ya muda nimalizie rekebisho lililoko kwenye ukurasa wa 146, linahusu kifungu cha…

(Hapa kengele ya pili ililia kuashiria kwisha kwa muda wa mzungumzaji)

Mheshimiwa Mwenyekiti, iingie kwenye kumbukumbu rasmi kwa sababu nimeshawasilisha kuhusu Chuo cha Butiama ambacho kipo kwenye hotuba ya Waziri kwamba kitajengwa Chuo cha Butiama, lakini kwenye Mpango wa miaka mitano hakipo. Kwa hiyo, naomba kutoa hoja kwamba hicho Chuo nacho kiingizwe kwenye Mpango pamoja na maelezo mengine ambayo nimeyatoa lakini kutokana na Kanuni…

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru.
 
Yapo maeneo ya kata ya saranga, mabibo, kimara, na ubungo ambayo kwa zaidi ya miaka mitatu walikuwa hawana hata ratiba ya mgawo wa maji lakini kwa sasa wanapata maji mara 2 mpaka 3 kwa wiki kutokana na juhudi zilizofanywa na Mbunge. Na bado taratibu zinaendelea ambapo mwanzoni mwa Nov Mkurugenzi wa Dawasco pamoja na Mbunge watakuwa na ziara kwenye kata tano ili kuona namna ya kulitafutia ufumbuzi tatizo la maji. Sasa sijui wale wanaotaka Mbunge afanye Lobbying kwa kiasi gani.
 
kuna watu wana chuki binafsi na mbunge wetu, katika wabunge wanaofanya kazi zao vizuri ndani ya bunge na nje ya bunge huyu Jamaa hakosekani. hawa wanaomlalamikia nahisi waliahidiwa ukatibu wa yule mwanamama kama angeshinda ubunge!
 
Mie mpiga kura wa Ubungo nachukua fursa hii adimu kukukumbusha ahadi yako kuwa utatatua kero ya maji mara utakapokuwa mbunge. Ni sekunde, dakika, saa, siku na miezi imepita haujafanya lolote la maana kukuhusiana na utatuzi wa kero ya maji jimboni mwako!!!! KULIKONI.

Kupitia JF nakuomba chonde chonde rejea kitabu chako cha AHADI, sie kazi yetu ilikuwa ni kukupa kura, nawe ni kutekeleza uliyoahidi.
Pia mbunge wetu uwe karibu na wapiga kura wote ACHA Ubaguzi wa kuwa karibu na wana magwanda tu. Kumbuka wewe ni mbunge wa wote,

Nawasilisha!!!

Mafililili,

Nashukuru kwa kunikumbusha suala ambalo sio tu kwamba nalikumbuka bali lipo katika mawazo, maneno na matendo yangu mara kwa mara katika utumishi wa umma. Hata hivyo, ulichokieleza sicho ambacho niliahidi katika kitabu changu kama ambavyo umesema; naomba urejee mkataba wangu na wapiga kura wenzangu wa jimbo la Ubungo ukumbuke nini ambacho nilikisema kuhusu maji. Kwa kumbukumbu za haraka nilizirudia tena hapa: https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/91961-ujumbe-wa-mbunge-shukrani-twende-kazi.html

Ahadi zangu kubwa kwa wananchi wa Ubungo ni mbili kuhusu maji: Kusimamia uwekaji mabomba kwenye maeneo yaliyorukwa na kuhakikisha DAWASCO inatimiza wajibu wake wa kuhahakikisha maji yanatoka wakati wote. Kuhamasisha ujenzi wa visima katika maeneo ambayo hayafikiki kirahisi na mtandao wa bomba kama suluhisho la mpito wakati tukifuatiia suluhisho la kudumu.

Mwezi Novemba 2011 nitatimiza mwaka mmoja toka kuchaguliwa; nakusudia wakati huo kueleza kwa kina mpaka sasa tumefanya nini katika kutimiza hizo ahadi mbili pamoja na hatua za ziada ambazo tumezichukua ambazo hazikuwepo katika ahadi. Baadhi ya mambo ambayo mpaka sasa tumefanikiwa ni DAWASCO kueleza kwamba maeneo ambayo yalirukwa yataanza kuwekewe mtandao mwezi Novemba, pia baada ya ufuatiliaji wa mwaka mzima katika vipindi mbalimbali kwa kwenda DAWASCO, kuandikikiana nao barua kuhoji bungeni, kufanya kongamano na hatimaye kufanya maandamano baadhi ya maeneo ambayo awali maji yalikuwa hayatoki pamoja na kuwa na mabomba yameanza kutoka maji haya ni kwa mfano Kimara Suca, Baruti, Stop Over, mabibo nk. Pia, miradi ya benki ya Dunia na WSSD ambayo kwa miaka mingi ilikuwa ni maneno bila matendo kupitia hatua ndani ya manispaa visima vimeanza kuchimbwa. Aidha, visima ambavyo vitakuwa na mitandao ya maji ya kuhudumia kaya mbalimbali vya Kilungule, Mavurunza, King'ong'o nk vilikuwa vimesimama muda mrefu toka ahadi ya Rais Kikwete alipokwenda Kimara nimetimiza wajibu wa ubunge wa kufuatilia na kusimamia na tayari vimeshachimbwa; vikiwa katika awamu tofauti, vipo ambavyo TANESCO wanashughulikia kuweka umeme hivi sasa, vipo ambavyo sasa viko hatua ya matanki kujengwa na vipo ambavyo sasa unawekwa mtandao wa mabomba. Nitawakumbusha DAWASA, kufuatilia kwa karibu zaidi na hatimaye Wizara ya Maji ije kufanya uzinduzi; cha Mburahati tayari kilishazinduliwa wakati wa wiki ya maji. Kwa upande mwingine, miradi ya maji ya BTC ili kupeleka maji Kwembe na Kibwegere kwa upande wa Kibamba inakwenda vizuri kwa fedha za wadau wa maendeleo na michango ya wanananchi nikiwemo mimi. Pia, hatimaye DAWASCO wametujibu barua zetu ambapo pamoja na mambo mengine tuliomba ratiba ya mgawo wa maji ili kila eneo kupata maji kwa wakati kwa mujibu wa ratiba; tumepatiwa ratiba tutaitangaza na kuendelea kufuatilia utekelezaji. na Mkurugenzi wa DAWASCO atafanya ziara jimbo la Ubungo. Ya mengine zaidi tutayaeleza wakati wa kueleza utekelezaji wa mwaka mmoja. Nashukuru wote jimboni na serikalini tulioshirikikiana kufikia tulipofika.

Pamoja na mafanikio hayo; bado siridhiki na hatua ambayo imefikiwa, natamani tungekuwa na serikali tungeweza kwenda kwa haraka zaidi. Mifumo yetu ina urasimu mwingi na ubadhirifu pia. Kwa wale ambao wamefuatilia michango yangu bungeni kuhusu masuala ya maji watanielewa nasema nini. Tuna changamoto na matatizo na tunahitaji hatua za haraka zaidi kuhusu maji. Ndio maana sikukubaliana na kauli ya serikali bungeni kuwa kero ya maji DSM itapungua 2014, naamini tunaweza kabisa kuipunguza sana mwaka 2012 na kuimaliza mwaka 2013. Hivyo, nitaendelea kuisimamia serikali ili ujenzi wa Bomba jingine Ruvu Juu ufanyike haraka zaidi pamoja na ujenzi wa Bwawa la Kidunda na uchimbaji wa visima vya Kimbiji na Mpera. Yapo maeneo ya Ubungo ambayo bado yanashida kubwa hususani ya pembezoni kama Msumi, Mpiji Magohe (hapa kisima kikubwa kimeanza kuchimbwa), Msakuzi, Msuguri/Msingwa, Makoka, na Goba (hapa kuna tatizo la mradi wa maji, kwa mwezi mzima sasa hakuna maji kwa kuwa mabomba yamefukuliwa kutokana na uhakiki unaoendelea wa watu waliounganishiwa kinyemela na matatizo mengine ya kiutawala. Nimewashauri pamoja na zoezi linaloendelea waruhusu maji yaendelee kwenda kwa wananchi kwa kuwa tayari mfuko wa Jimbo ambao mimi ni mwenyekiti wake umeshatoa milioni tatu za kulipa sehemu ya deni la maji), Golani ya Msewe (hapa napo kuna tatizo la mradi) nk.

Kwa ujumla matatizo mengi ni ya kimfumo ambayo usimamizi na ufuatiliaji wa mtu mmoja hauwezi kuyamaliza kwa haraka, katika kipindi cha mwaka mmoja tumesogea lakini naelekeza nguvu zaidi katika kuisamia serikali na taasisi zake ili zitimize wajibu wa kutumia vizuri kodi zetu na fedha toka kwa washirika wa maendeleo zinazokuja kwa ajili yetu kwenda mbele zaidi. Sisi jimboni tutaendelea kuunganisha nguvu ya umma na ya wadau wengine ikiwemo wa sekta binafsi kwenda mbele zaidi. Hata hivyo, yanahitajika mabadiliko makubwa DAWASCO, DAWASA, Wizara ya Maji na Idara ya Maji ya Manispaa ya Kinondoni tuweze kuongeza nguvu zaidi. Pia, maji yasingenunuliwa kwa bei mbaya huko mitaani kama EWURA ingefanya kazi yake ya kutengeneza kanuni za viwango na bei ya maji ikiwemo katika sekta binafsi kama ambavyo sheria inahitaji. Mambo yakueleza kuhusu maji ni mengi, tutaendelea kuelezana kwenye taarifa ya mwaka mmoja nitakayotoa. Tuendelee kushirikiana, kidole kimoja hakivunji chawa

JJ
 
Mnyika nakupongeza kwa maelezo mazuri nina mansion yangu pale kimara temboni huwa nanunua maji dumu 500,ninaamini unauwezo wa kufuatilia mambo ndio maana ukapewa nafasi ccm ndio tatizo hapo ubungo kwani walikuwa miaka yote na ni upuuzi mtupu waliofanya.
 
Well said....ila naomba uwe unajitokeza humu jamvini kujibu baadhi ya hoja.Ubungo hatukufanya makosa.
 
Back
Top Bottom