Mbunge wetu John Mnyika thubutu utatue kero ya maji jimboni mwako!

Mkuu J. Mnyika uwe unajitahidi kujibu hoja mapema kabla hujatukanwa na kuchafuliwa. Ona sasa watu wamekunangaaa weee halafu ndiyo unajibu hoja. Mwenzako Zitto ni mwepesi sana kujibu hoja, jaribu kumuiga.
 
Kazi ya mbunge ni kufuatilia utekelezaji wa serikali na siyo kuleta maendeleo yeye kama yeye. Sasa ukishangaa ya Mnyika je ukisikia ya JK ya kuigeuza Kigoma kuwa Dubai si utazimia kabisa? Na huyo ndiyo yupo kwenye maamuzi ya juu!

mwita25 umeniacha hoi ulivyo nikimbusha ahad ya m.k.w.e.r.e ya kigoma kuwa Dubai.... Atleast mnyika follow up znaonekana bt The Corruptd System ndo inayo mwangusha...
 
We bwana ni mmoja wa watu mnaompotosha mbunge wetu. Usilete utetezi usio na tija juu ya kushindwa kutekeleza ahadi ambazo mlizitoa kwa wananchi. Tunashukuru siku hizi umehama Ubungo hivyo ushauri wako kwa mheshimiwa umepungua!!. Tuwe wawazi MHESHIMIWA MNYIKA JIMBO analiweka rehani; kuna kila dalili atashindwa kulikomboa 2015. Sie wenye nia nzuri na mbunge tunamkumbusha akae kitako na kurejea ahadi zake ikibidi arudi tena kwa wapiga kura atueleweshe kwanini hajatekeleza hata AHADI moja.

mwenzio kajibu hoja with clear explainatn za sababu n' what ve bn done, na mifano nk.. Wewe unamjibu kwa porojo., kaz kweli kweli, Nape inabid afanye usahili upya...
 
Mnyika baada ya kuwa Mbunge aliitisha Kongamano la lililowahisisha Wadau Mbalimbali wa Jimbo la Ubungo, lengo likiwa ni Kubrainstorm nini Kifanyike ili kuweza kuondoa Tatizo la Maji. Kwangu mimi that was a Scientific approach ambayo ni sahihi kabisa katika kumaliza Matatizo mbalimbali yanayotukabili " Yaani kwanza tukae bila kujali viwanngo vya Elimu vyetu tujadili Matatizo yetu na Tupendekeze Njia za Kuyatatua".

Ikumbukwe kwamba Mnyika si Mkurugenzi wa Dawasco lakini katika Kongamano hilo Walialikwa Watu wa DAWASCO lakini " Kwa Sababu Kongamano liliandaliwa na Mbunge kutoka Kambi ya Upinzani" Jamaa wa DAWASCO HAWAKUTOKEA na Hata walipopelekewa Ripoti ya Mapendezo ya Kongamano hilo " Kwa Sababu tu Ripoti ilitokana na Kongamano lililoitishwa na Mbunge kutoka chama cha Upinzani" Jamaa wa DAWASCO wakaiweka Kapuni.

Nadhani ingekuwa Fair kumuuliza Mnyika juu ya yaliyojadiliwa pale Chuo cha Maji na Kama DAWASCO wamedharau Mapendekezo ya Wadau waliokusanyika na Kutoa Mawazo yao ni anapanga Kukifanya

mnacho nifurahisa ni kuona how intellectual wana cdm are, wa2 wanajibu hoja kwa facts kama wewe mkuu, badala na wenyewe kugonga nondo wanakaa kupiga porojo... Kaz sana...
 
Mafililili,

Nashukuru kwa kunikumbusha suala ambalo sio tu kwamba nalikumbuka bali lipo katika mawazo, maneno na matendo yangu mara kwa mara katika utumishi wa umma. Hata hivyo, ulichokieleza sicho ambacho niliahidi katika kitabu changu kama ambavyo umesema; naomba urejee mkataba wangu na wapiga kura wenzangu wa jimbo la Ubungo ukumbuke nini ambacho nilikisema kuhusu maji. Kwa kumbukumbu za haraka nilizirudia tena hapa: https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/91961-ujumbe-wa-mbunge-shukrani-twende-kazi.html

Ahadi zangu kubwa kwa wananchi wa Ubungo ni mbili kuhusu maji: Kusimamia uwekaji mabomba kwenye maeneo yaliyorukwa na kuhakikisha DAWASCO inatimiza wajibu wake wa kuhahakikisha maji yanatoka wakati wote. Kuhamasisha ujenzi wa visima katika maeneo ambayo hayafikiki kirahisi na mtandao wa bomba kama suluhisho la mpito wakati tukifuatiia suluhisho la kudumu.

Mwezi Novemba 2011 nitatimiza mwaka mmoja toka kuchaguliwa; nakusudia wakati huo kueleza kwa kina mpaka sasa tumefanya nini katika kutimiza hizo ahadi mbili pamoja na hatua za ziada ambazo tumezichukua ambazo hazikuwepo katika ahadi. Baadhi ya mambo ambayo mpaka sasa tumefanikiwa ni DAWASCO kueleza kwamba maeneo ambayo yalirukwa yataanza kuwekewe mtandao mwezi Novemba, pia baada ya ufuatiliaji wa mwaka mzima katika vipindi mbalimbali kwa kwenda DAWASCO, kuandikikiana nao barua kuhoji bungeni, kufanya kongamano na hatimaye kufanya maandamano baadhi ya maeneo ambayo awali maji yalikuwa hayatoki pamoja na kuwa na mabomba yameanza kutoka maji haya ni kwa mfano Kimara Suca, Baruti, Stop Over, mabibo nk. Pia, miradi ya benki ya Dunia na WSSD ambayo kwa miaka mingi ilikuwa ni maneno bila matendo kupitia hatua ndani ya manispaa visima vimeanza kuchimbwa. Aidha, visima ambavyo vitakuwa na mitandao ya maji ya kuhudumia kaya mbalimbali vya Kilungule, Mavurunza, King'ong'o nk vilikuwa vimesimama muda mrefu toka ahadi ya Rais Kikwete alipokwenda Kimara nimetimiza wajibu wa ubunge wa kufuatilia na kusimamia na tayari vimeshachimbwa; vikiwa katika awamu tofauti, vipo ambavyo TANESCO wanashughulikia kuweka umeme hivi sasa, vipo ambavyo sasa viko hatua ya matanki kujengwa na vipo ambavyo sasa unawekwa mtandao wa mabomba. Nitawakumbusha DAWASA, kufuatilia kwa karibu zaidi na hatimaye Wizara ya Maji ije kufanya uzinduzi; cha Mburahati tayari kilishazinduliwa wakati wa wiki ya maji. Kwa upande mwingine, miradi ya maji ya BTC ili kupeleka maji Kwembe na Kibwegere kwa upande wa Kibamba inakwenda vizuri kwa fedha za wadau wa maendeleo na michango ya wanananchi nikiwemo mimi. Pia, hatimaye DAWASCO wametujibu barua zetu ambapo pamoja na mambo mengine tuliomba ratiba ya mgawo wa maji ili kila eneo kupata maji kwa wakati kwa mujibu wa ratiba; tumepatiwa ratiba tutaitangaza na kuendelea kufuatilia utekelezaji. na Mkurugenzi wa DAWASCO atafanya ziara jimbo la Ubungo. Ya mengine zaidi tutayaeleza wakati wa kueleza utekelezaji wa mwaka mmoja. Nashukuru wote jimboni na serikalini tulioshirikikiana kufikia tulipofika.

Pamoja na mafanikio hayo; bado siridhiki na hatua ambayo imefikiwa, natamani tungekuwa na serikali tungeweza kwenda kwa haraka zaidi. Mifumo yetu ina urasimu mwingi na ubadhirifu pia. Kwa wale ambao wamefuatilia michango yangu bungeni kuhusu masuala ya maji watanielewa nasema nini. Tuna changamoto na matatizo na tunahitaji hatua za haraka zaidi kuhusu maji. Ndio maana sikukubaliana na kauli ya serikali bungeni kuwa kero ya maji DSM itapungua 2014, naamini tunaweza kabisa kuipunguza sana mwaka 2012 na kuimaliza mwaka 2013. Hivyo, nitaendelea kuisimamia serikali ili ujenzi wa Bomba jingine Ruvu Juu ufanyike haraka zaidi pamoja na ujenzi wa Bwawa la Kidunda na uchimbaji wa visima vya Kimbiji na Mpera. Yapo maeneo ya Ubungo ambayo bado yanashida kubwa hususani ya pembezoni kama Msumi, Mpiji Magohe (hapa kisima kikubwa kimeanza kuchimbwa), Msakuzi, Msuguri/Msingwa, Makoka, na Goba (hapa kuna tatizo la mradi wa maji, kwa mwezi mzima sasa hakuna maji kwa kuwa mabomba yamefukuliwa kutokana na uhakiki unaoendelea wa watu waliounganishiwa kinyemela na matatizo mengine ya kiutawala. Nimewashauri pamoja na zoezi linaloendelea waruhusu maji yaendelee kwenda kwa wananchi kwa kuwa tayari mfuko wa Jimbo ambao mimi ni mwenyekiti wake umeshatoa milioni tatu za kulipa sehemu ya deni la maji), Golani ya Msewe (hapa napo kuna tatizo la mradi) nk.

Kwa ujumla matatizo mengi ni ya kimfumo ambayo usimamizi na ufuatiliaji wa mtu mmoja hauwezi kuyamaliza kwa haraka, katika kipindi cha mwaka mmoja tumesogea lakini naelekeza nguvu zaidi katika kuisamia serikali na taasisi zake ili zitimize wajibu wa kutumia vizuri kodi zetu na fedha toka kwa washirika wa maendeleo zinazokuja kwa ajili yetu kwenda mbele zaidi. Sisi jimboni tutaendelea kuunganisha nguvu ya umma na ya wadau wengine ikiwemo wa sekta binafsi kwenda mbele zaidi. Hata hivyo, yanahitajika mabadiliko makubwa DAWASCO, DAWASA, Wizara ya Maji na Idara ya Maji ya Manispaa ya Kinondoni tuweze kuongeza nguvu zaidi. Pia, maji yasingenunuliwa kwa bei mbaya huko mitaani kama EWURA ingefanya kazi yake ya kutengeneza kanuni za viwango na bei ya maji ikiwemo katika sekta binafsi kama ambavyo sheria inahitaji. Mambo yakueleza kuhusu maji ni mengi, tutaendelea kuelezana kwenye taarifa ya mwaka mmoja nitakayotoa. Tuendelee kushirikiana, kidole kimoja hakivunji chawa

JJ

Hongera mheshimwa kwa kuwa karibu na matatizo ya wananchi. Nawashangaa kwanini wabunge wa Ilala, Kinondoni, Segerea, Ukonga, Temeke na Kigamboni hawataki kujifunza kutoka kwako?? Ama huwa ni mchoyo wa kuwagawia namna ya kutenda kazi za wananchi. BIG UP JJ!!!
 
Msiyeyushe hii thread ina mshiko. Mnyika tumekupa ubunge uwe spika yetu huko wizarani watuletee maji fullstop. Umefanya kazi, umechimba visima tanesco wanasuasua kupeleka umeme kwenye visima lakini mpaka matank yamejengwa na tunayaona. Ushauri: mbunge wetu tafuta njia nzuri ya kutoa feedback kwa mambo unayofanya na speed pia iongezeke. Mwisho wa siku ili ueleweke watu wanataka maji na barabara haya mengine yatafuata baada ya hili.
 
Mie mpiga kura wa Ubungo nachukua fursa hii adimu kukukumbusha ahadi yako kuwa utatatua kero ya maji mara utakapokuwa mbunge. Ni sekunde, dakika, saa, siku na miezi imepita haujafanya lolote la maana kukuhusiana na utatuzi wa kero ya maji jimboni mwako!!!! KULIKONI.

Kupitia JF nakuomba chonde chonde rejea kitabu chako cha AHADI, sie kazi yetu ilikuwa ni kukupa kura, nawe ni kutekeleza uliyoahidi.
Pia mbunge wetu uwe karibu na wapiga kura wote ACHA Ubaguzi wa kuwa karibu na wana magwanda tu. Kumbuka wewe ni mbunge wa wote,

Nawasilisha!!!
Yaani thread yako imekaa kinafkinafki kama walivyo magamba.
 
Msiyeyushe hii thread ina mshiko. Mnyika tumekupa ubunge uwe spika yetu huko wizarani watuletee maji fullstop. Umefanya kazi, umechimba visima tanesco wanasuasua kupeleka umeme kwenye visima lakini mpaka matank yamejengwa na tunayaona. Ushauri: mbunge wetu tafuta njia nzuri ya kutoa feedback kwa mambo unayofanya na speed pia iongezeke. Mwisho wa siku ili ueleweke watu wanataka maji na barabara haya mengine yatafuata baada ya hili.
kwani kazi ya mbunge ni kuleta maji au kusimamia maji ya yapatikane? na pia nakushauri ungefuatilia na ahadi za rais wako.
 
Mie mpiga kura wa Ubungo nachukua fursa hii adimu kukukumbusha ahadi yako kuwa utatatua kero ya maji mara utakapokuwa mbunge. Ni sekunde, dakika, saa, siku na miezi imepita haujafanya lolote la maana kukuhusiana na utatuzi wa kero ya maji jimboni mwako!!!! KULIKONI.

Kupitia JF nakuomba chonde chonde rejea kitabu chako cha AHADI, sie kazi yetu ilikuwa ni kukupa kura, nawe ni kutekeleza uliyoahidi.
Pia mbunge wetu uwe karibu na wapiga kura wote ACHA Ubaguzi wa kuwa karibu na wana magwanda tu. Kumbuka wewe ni mbunge wa wote,

Nawasilisha!!!

mkuu kumbe ulimkumbusha miaka takribani minne nyuma? Kweli sikio la kufa halisikii dawa
 
mkuu kumbe ulimkumbusha miaka takribani minne nyuma? Kweli sikio la kufa halisikii dawa

Mie mpiga kura wa Ubungo nachukua fursa hii adimu kukukumbusha ahadi yako kuwa utatatua kero ya maji mara utakapokuwa mbunge. Ni sekunde, dakika, saa, siku na miezi imepita haujafanya lolote la maana kukuhusiana na utatuzi wa kero ya maji jimboni mwako!!!! KULIKONI.

Kupitia JF nakuomba chonde chonde rejea kitabu chako cha AHADI, sie kazi yetu ilikuwa ni kukupa kura, nawe ni kutekeleza uliyoahidi.
Pia mbunge wetu uwe karibu na wapiga kura wote ACHA Ubaguzi wa kuwa karibu na wana magwanda tu. Kumbuka wewe ni mbunge wa wote,

Nawasilisha!!!
Tutaanza kufichua mabilioni yaliyotengwa kwa ajili ya maji yanavyotumika vibaya.

Kwanza kuna pesa za MCA (Milennium Challenge AccounT) kama ambavyo mradi unajieleza kwenye website ya serikali.
attachment.php


Hizi ilipewa wizara ya fedha moja kwa moja. Je, Mnyika atafute nyingine na kuanza project mpya?

Alipopelekwa hoja yake binafsi ya kufuatilia mradi huu, Waziri alimzima, wote tunakumbuka.

Waziri mwenyewe alituambia kuwa kuna fedha hii kwenye bajeti ya 2012/13 Namnukuu hapa

Serikali yatenga mabilioni kugharimia maji.WIZARA ya Maji jana iliwasilisha makadirio yake ya matumizi kwa mwaka 20012/2013 bungeni ambayo yanaonyesha kuwa imetenga Sh465.756 bilioni kwa ajili ya miradi ya maendeleo.Akiwasilisha bajeti hiyo, Waziri wa Maji, Profesa Jumanne Maghembe alisema kati ya fedha hizo, Sh140.015 bilioni ni za ndani na Sh325.740 ni fedha kutoka nje.
Profesa Maghembe alisema kwa ujumla wake, wizara yake inakusudia kutumia Sh485.898 bilioni, kati ya hizo matumizi ya kawaida ni Sh20.142 bilioni.
Alisema miongoni mwa kazi ambazo wizara hiyo imepanga kuzitekeleza ni pamoja na maeneo yanayofaa kuchimba visima virefu na kusimamia uchimbaji kwa maeneo 630 katika sehemu mbalimbali nchini.
“Mwaka 2012/2013, kupitia Bajeti ya Serikali, Sh51.9 bilioni kutoka mfuko wa pamoja zimepangwa kugharimia ujenzi wa miundombinu ya maji, kujenga uwezo wa watekelezaji wa programu, uhamasishaji, kutoa elimu ya usafi na mazingira, ufuatiliaji na kulipa wataalamu washauri kwa ajili ya usimamizi wa makandarasi,” alisema Profesa Maghembe na kuongeza:
“Kiwango hicho cha fedha kilichotengwa ni sehemu ya Sh81.8 bilioni ya mchango wa Serikali na ahadi ya Washirika wa Maendeleo.”
Alisema Serikali inaendelea kutekeleza Mpango wa Dharura wa Kuboresha Huduma ya Maji katika Jiji la Dar es Salaam na Miji ya Kibaha na Bagamoyo ambao unalenga kuongeza uwezo wa uzalishaji wa maji kutoka mita za ujazo 300,000 kwa siku hadi mita za ujazo 710,000 siku ifikapo 2014.
Profesa Maghembe alisema mpango huo unatekelezwa kwa ushirikiano baina ya Serikali ya Tanzania na Shirika la Marekani la Changamoto za Milenia (MCC), Serikali ya Norway, Serikali ya India na washirika wengine wa maendeleo kupitia Mfuko wa Pamoja wa Maji.
“Utekelezaji wa Mpango huo ulianza rasmi Februari 2011 na umepangwa kukamilika Desemba 2014 na utagharimu Sh653.9 bilioni,” alisema Profesa Maghembe.
Watanzania tumekuwa wajinga. Mahali ambapo uzembe uko wazi tu, tunaleta siasa eti kuadhibu upinzania.

Mimi ntaanza kulikuza hili, nahisi kuna uchafu kama wa EPA na ESCROW.

Kwa nini Maghembe alizima hoja binafsi ya Mnyika?

Kwa nini team Lumumba inaitumia hii kama propaganda ya kumchafua Mnyika?

attachment.php

attachment.php


Tatizo si kuwa pesa hakuna, tatizo zimetumikaje?

Baada ya Escrow mnaonaje tulikuze hili limtikise Maghembe?

Kwa kweli Mnyika anachukiwa na CCM kwa jinsi anavyohoji mambo bungeni!!
 
mwita25 umeniacha hoi ulivyo nikimbusha ahad ya m.k.w.e.r.e ya kigoma kuwa Dubai.... Atleast mnyika follow up znaonekana bt The Corruptd System ndo inayo mwangusha...

Kumtetea mnyika kwa kumlinganisha na jk ambae alimwita dhaifu haisaidii.

hii manake mnyika ni dhaifu na ndo mana ahadi yake ya maji kashindwa kutimiza.

Waalah kura yangu haipati Tena Kama maji nisipoyaona ubungo
 
Back
Top Bottom