Charles Kimei awatoa hofu Wanavunjo utekelezaji wa ahadi ya hayati Magufuli ya Vunjo kupewa Halmashauri ya Wilaya

SautiYaMnyonge

JF-Expert Member
May 13, 2018
439
742
Na Mwandishi Wetu,

Moshi.

Mbunge wa jimbo la Vunjo Mhe Dkt Charles Stephen Kimei ameendelea kufuatilia kwa karibu ahadi zake binafsi, ahadi za hayati Rais Magufuli pamoja na utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM 2020-2025 kwa karibu ili kuhakikisha wanakidhi matarajio na matumaini makubwa ya wananchi waliyokuwa nayo wakati wanaichagua CCM katika uchaguzi mkuu Oktoba, 2020.

Moja ya ahadi iliyopokelewa kwa shauku kubwa ni ile ya kuipa halmashauri ya wilaya jimbo la Vunjo ombi ambalo liliwasilishwa serikalini tangu mwaka 2000 bila mafanikio mpaka alipokuja kuitoa hayati Rais Magufuli kuwa ikiwa wananchi wataichagua katika ngazi zote za udiwani, ubunge na urais hakuna sababu kwanini halmashauri hiyo isipatikane. Wananchi wa Vunjo nao sababu wanaitaka halmashauri ya wilaya wakaichagua CCM kwa ushindi wa kishindo kwa kuwachagua madiwani wa kata zote 16, Mbunge Dkt Charles Stephen Kimei alipata ushindi wa asilimia 74 huku urais hayati Magufuli alipata asilimia 84.5.

Mchakato wa kisheria kwa mujibu wa muongozo wa TAMISEMI wa kupandisha hadhi maeneo ya kiutawala tayari umeanza ambapo hoja binafsi iliwasilishwa kuhusu kuanzishwa kwa halmashauri ya wilaya ya Vunjo, ikapokelewa na kuungwa mkono na madiwani wote 42 wa halmashauri ya wilaya ya Moshi, mkurugenzi mtendaji akaunda kamati ya wataalam kufanya tathmini ya ombi hilo la Vunjo kuwa halmashauri ya wilaya, taarifa hiyo ikaonesha Vunjo inakidhi vigezo kwa zaidi ya asilimia 70, mikutano ya ukusanyaji maoni ya wananchi juu ya kutaka au kutokutaka kupewa hadhi hiyo ya halmashauri ya wilaya ambapo wananchi zaidi ya 35,000 waliunga mkono asilimia mia moja kupata halmashauri ya wilaya.

Taarifa hiyo iliwasilishwa kwenye baraza la madiwani la halmashauri ya wilaya ya Moshi na ilipokelewa na kuungwa mkono kwa asilimia mia moja. Kwa sasa hatua zinazofuata ni taarifa hizo kuwasilishwa kwenye baraza la ushauri la wilaya (DCC), baraza la ushauri la mkoa (RCC) na baadaye wizara ya TAMISEMI kwa hatua zaidi.

Hata hivyo Mbunge wa jimbo la Vunjo Mhe Dkt Kimei amesema wananchi waendelee kuwa watulivu kwani tayari Mhe Rais Samia Suluhu Hassan amekwishasema ahadi zote zilizotolewa na hayati Magufuli serikali anayoiongoza itazitekeleza kikamilifu.

"Ninawaomba wananchi wenzangu wa Vunjo kuwa watulivu na zaidi tuendelee kuiunga mkono serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe Rais Samia Suluhu Hassan kwani hakuna mashaka kuwa ahadi ya Vunjo kupata halmashauri ya wilaya kama alivyotuahidi hayati Rais Magufuli ataikamilisha."

Mbali na hili Dkt Kimei amesema wanavunjo wanapaswa kuona fahari na uongozi wa Rais Samia kwani katika kipindi kifupi serikali anayoiongoza imekwishatoa fedha nyingi za maendeleo katika jimbo la Vunjo kuliko wakati mwingine wowote muda kama huu.

"Tumepokea fedha za ujenzi na ukamilishaji wa madarasa, maabara, mabweni, nyumba za walimu, matundu ya vyoo, zahanati, vituo vya afya, miundombinu ya umwagiliaji, usambazaji umeme vijijini, uchongaji na ukarabati wa barabara, ujenzi wa vivuko na madaraja, uboreshaji wa miundombinu ya maji safi na salama. Miradi hii yote ipo katika hatua mbalimbali na mimi binafsi nimekuwa nikipita kuikagua na hata sasa baada ya kumalizika kwa bunge hili la bajeti nitakuwa jimboni kukagua miradi inayoendelea. Kwa hakika tunamshukuru sana Rais Samia na tunamuahidi ushirikiano wa hali ya juu."

Wananchi wengi wa jimbo la Vunjo kwa nyakati tofauti wameonekana kukiri mabadiliko katika utekelezaji wa miradi, utatuzi wa kero na hata utendaji wa wawakilishi wao katika nafasi za udiwani na hata ubunge zaidi wamemshukuru Rais Samia kwa kurejesha mahusiano na Kenya hali iliyopelekea kufunguliwa kwa mpaka wa Holili na sasa biashara ya mazao inafanyika vizuri.

IMG-20210106-WA0017.jpg
 
Basi sawa, Ila asiishie huko Vunjo tu, kwenye kampeni alisema Mwanza mjini kutaongezwa wilaya ziwe tatu, Tanga kuwe na mikoa miwili, Morogoro mikoa miwili, Katoro kuwa wilaya, Mbeya kuongeza wilaya Ila sasa sijui Kama wahusika wanafanyia kazi hizo Ahadi au wamejikausha kama vile hawajui.
 
Hivi sehemu inakuwa Wilaya kutokana na mahitaji au sababu fulani alitoa ahadi....

Kuna mambo ya ajabu ajabu sababu tumeyazoea tunaona ni ya kawaida...
 
Back
Top Bottom