Mbunge: wanawake mnamkosea Mungu

Mbunge: wanawake mnamkosea Mungu

EMT

Platinum Member
Joined
Jan 13, 2010
Posts
14,477
Reaction score
15,357
MBUNGE wa Konde, Khatibu Said Haji (CUF) amesema wanawake wameadhibiwa na Mungu katika maandiko matakatifu na kuhoji hawaoni kuwa harakati zao za kudai haki sawa, ikiwemo uwakilishi wa asilimia 50 kwa 50 katika nafasi za uamuzi kuwa ni kuingilia adhabu hiyo halali.

Alisema hayo jana bungeni mjini Dodoma, kwenye swali la nyongeza baada ya Mbunge wa Viti Maalumu, Leticia Nyerere, kuomba Serikali ipeleke muswada wa sheria bungeni, utakaowalazimisha waajiri kuajiri wafanyakazi kwa kuzingatia asilimia 50 wanaume na asilimia 50 wanawake.

Huku Naibu Spika, Job Ndugai, ‘akichomekea' kuwa hoja hiyo haiungwi mkono ndio maana hakuna makofi mengi ya wabunge. Leticia alisema kwa kuwa wako wanawake wenye uwezo, elimu na makini kuliko wanaume ni vyema sheria hiyo ifikishwe bungeni, ili kuwalazimisha waajiri kuifuata.

Akijibu hoja ya Khatibu, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba, alisema kama Mbunge wa Konde anazungumzia sheria ya dini, yeye ameisoma lakini haki za wanawake zilizopo katika sheria hiyo ya dini, zimekuwa zikidhulumiwa.

Alitoa mfano wa haki ya mwanamke aliyeolewa kufuliwa nguo na mumewe ambayo iko katika sheria ya dini, ambayo alisema mfano unaoonesha namna haki hizo za wanawake zilizopo katika sheria ya dini, zinavyodhulumiwa.

Baada ya kutoa jibu hilo, alisimama Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaaa (Tamisemi), Hawa Ghasia aliyesema kitabu kitakatifu cha Kurani, kimeweka wazi kuwa mwanamume ndiye mlinzi wa mwanamke na kufafanua kuwa katika hali ya kawaida, mlinzi ni mtu muhimu lakini anayelindwa ni kiongozi.

Hata hivyo Waziri Simba katika majibu, alisema Serikali imekuwa ikichukua hatua mbalimbali za makusudi kutimiza lengo la uwiano sawa kati ya wanawake na wanaume.

Akizungumza nje ya ukumbi wa Bunge, Mbunge Haji alifafanua adhabu aliyosema wanawake wamepewa na Mungu akinukuu kitabu cha Mwanzo katika Biblia kwamba mwanamke alipewa adhabu mbili; moja ya kuzaa kwa uchungu na ya pili ya kuwa chini ya mamlaka ya mwanamume.

Chanzo:Habari leo
 
Mkuu EMT, heshima kwako! Nahisi hi kitu ilipaswa kule kwenye lile jukwaa la pasua kichwa na sio humu, wenzio huku tunakujaga wakati tunataka ku-reflesh mind, hi nayo imekaa kipasua kichwa zaidi hi kaka.
 
Hapo ni kama signature yako inavosema,"poverty makes people do reckless things". Nadhani inahusika na umaskini wa akili pia.
 
Mkuu EMT, heshima kwako! Nahisi hi kitu ilipaswa kule kwenye lile jukwaa la pasua kichwa na sio humu, wenzio huku tunakujaga wakati tunataka ku-reflesh mind, hi nayo imekaa kipasua kichwa zaidi hi kaka.

Mi nadhani ilifaa kuwekwa kwenye Jukwaa la Jokes..
 
Hii nchi sijui tumerogwa na nani? Eti haki yakufuliwa nguo..waziri Mzima anaongelea hili..of all important issues to discus?
 
Hawa Ghasia is a very big disappointment......mwenzie karejea BIBLIA yeye anajibu kwa KORAN
 
[SUP][SUB]Tunasoma katika kitabu kitakatifu cha Biblia, 1 Timotheo 2:9-14
[/SUB]

9[/SUP]Vivyo hivyo nataka wanawake wajipambe kwa adabu na kwa heshima katika mavazi yanayostahili, si kwa kusuka nywele, kuvalia dhahabu, lulu au mavazi ya gharama kubwa, [SUP]10[/SUP]bali kwa matendo mazuri kama iwapasavyo wanawake wanaokiri kuwa wanamcha Mungu.
[SUP]11[/SUP]Mwanamke na ajifunze kwa utulivu na kwa utii wote. [SUP]12[/SUP]Simpi mwanamke ruhusa ya kufundisha au kuwa na mamlaka juu ya mwanaume. Mwanamke inampasa kukaa kimya. [SUP]13[/SUP]Kwa maana Adamu aliumbwa kwanza, kisha Eva. [SUP]14[/SUP]Wala si Adamu aliyedanganywa, bali ni mwanamke aliyedanganywa akawa mkosaji.

Mwenye masikio na asikiye neno hili Roho ayaambia makanisa.
 
Hii nchi sijui tumerogwa na nani? Eti haki yakufuliwa nguo..waziri Mzima anaongelea hili..of all important issues to discus?
Hawana jipya, bora mwenzao aliyejikita kwenye elimu kwa kujisajili kufanya Mitihani ya QT mwaka huu pale shule ya Sekondari Yemen.
 
Mimi kama mwanamke sina la kusema,Ila ile adhabu aliyopewa mwanamke ni kwaajili ya dhambi yake ya kukosa utii na aliambiwa tamaa yako itakuwa kwa mumeo naye atakutawala,hope huko kwenye taasisi za serikali na binafsi hakuna ndoa,namaanisha hakuna mume atakayemtawala mkewe.

Mtu apewe nafasi kulingana na uwezo wake,kama wapo wanawake wenye uwezo na sifa zinazostahili wapewe nafasi tu hata kama ni zote,kama wanaume wapo wenye uwezo huo wapewe tu hata kama ni zote,kila mtu apewe nafasi kulingana na uwezo pamoja na taaluma yake,mambo ya kubebana bebana yamepitwa na wakati.
 
[SUP][SUB]Tunasoma katika kitabu kitakatifu cha Biblia, 1 Timotheo 2:9-14
[/SUB]

9[/SUP]Vivyo hivyo nataka wanawake wajipambe kwa adabu na kwa heshima katika mavazi yanayostahili, si kwa kusuka nywele, kuvalia dhahabu, lulu au mavazi ya gharama kubwa, [SUP]10[/SUP]bali kwa matendo mazuri kama iwapasavyo wanawake wanaokiri kuwa wanamcha Mungu.
[SUP]11[/SUP]Mwanamke na ajifunze kwa utulivu na kwa utii wote. [SUP]12[/SUP]Simpi mwanamke ruhusa ya kufundisha au kuwa na mamlaka juu ya mwanaume. Mwanamke inampasa kukaa kimya. [SUP]13[/SUP]Kwa maana Adamu aliumbwa kwanza, kisha Eva. [SUP]14[/SUP]Wala si Adamu aliyedanganywa, bali ni mwanamke aliyedanganywa akawa mkosaji.

Mwenye masikio na asikiye neno hili Roho ayaambia makanisa.

Paulo naye ni roho????? Isitoshe hii ipo applicable huko makanisani sio bungeni au kwenye taasisi zisizo za kikanisa!
 
Mimi kama mwanamke sina la kusema,Ila ile adhabu aliyopewa mwanamke ni kwaajili ya dhambi yake ya kukosa utii na aliambiwa tamaa yako itakuwa kwa mumeo naye atakutawala,hope huko kwenye taasisi za serikali na binafsi hakuna ndoa,namaanisha hakuna mume atakayemtawala mkewe.

Mtu apewe nafasi kulingana na uwezo wake,kama wapo wanawake wenye uwezo na sifa zinazostahili wapewe nafasi tu hata kama ni zote,kama wanaume wapo wenye uwezo huo wapewe tu hata kama ni zote,kila mtu apewe nafasi kulingana na uwezo pamoja na taaluma yake,mambo ya kubebana bebana yamepitwa na wakati.

Very true! Wasiingize habari za ndoa, pale bungeni si taasisi ya ndoa!
 
yani hoja zilikosekana mpaka wakaanza kudiscus ndoa kweli kazi tunayo..
 
Uko sahihi sana. Tatizo wanawake tumesahau nafasi zetu. Ndo mana siku hizi kuna wachungaj wanawake while biblia inasema mchungaji awe mume wa mke mmoja. I HATE GENDER EQUALITY. Inawadanganya wanawake sana. Nafurahi kuwe mke ninaejua MY PURPOSE ON EARTH. Haijawah na haitotokea kuwa na usawa kati ya mke na mme. MWANAMKE UNAJILAZIMISHA KUTAFUTA KWA JASHO WAKAT MWANAUME HAZAI KWA UCHUNGU
 
Mimi kama mwanamke sina la kusema,Ila ile adhabu aliyopewa mwanamke ni kwaajili ya dhambi yake ya kukosa utii na aliambiwa tamaa yako itakuwa kwa mumeo naye atakutawala,hope huko kwenye taasisi za serikali na binafsi hakuna ndoa,namaanisha hakuna mume atakayemtawala mkewe.

Mtu apewe nafasi kulingana na uwezo wake,kama wapo wanawake wenye uwezo na sifa zinazostahili wapewe nafasi tu hata kama ni zote,kama wanaume wapo wenye uwezo huo wapewe tu hata kama ni zote,kila mtu apewe nafasi kulingana na uwezo pamoja na taaluma yake,mambo ya kubebana bebana yamepitwa na wakati.

Umenena
 
Sasa mbuzi jike nae aliadhibiwa manake akiwa anazaa anapiga kelele ile mbaya,
 
Back
Top Bottom