Sijui mimi ndie sielewi maana ya haki sawa!!!! Majukumu ya mwanamke na mwanaume yanajulikana, kuna kazi ambazo huwezi kumuachia mwanaume afanye kwasababu ya haki sawa.
Mimi binafsi, napenda haki sawa kwasabu nyingi ila kubwa ni kuwa;
Sisi ni masikini sana, ni lazima nguvu ya watu wengi iwepo. Maswala ya kulala nyumbani kumsubiri mume, yafanywe na wale walioridhika na uchumi wa taifa lao. Mwanamke anapaswa kuweka mchango wake katika sector ya uchumi.
Umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu. Mwanamke na mwanaume wote wanapaswa kujenga taifa letu kwa pamoja.
Ila uwa nashangaa wanawake wanaotafsiri haki sawa kwenye mashindano ya ajabu ajabu kama kufua ama kulala nje kisa mume alilala nje jana wakati kuna haki sawa...