Mbunge wa Nyamagana ashikiliwa na Polisi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbunge wa Nyamagana ashikiliwa na Polisi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Dec 16, 2010.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Dec 16, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  POLISI mkoani Mwanza Desemba 15 ilimshikilia kwa mahojiano Mbunge wa Nyamagana, Ezekiah Wenje (Chadema), kutokana na madai ya kutoa maneno ya uchochezi wakati alipohutubia wananchi hivi karibuni kwenye Uwanja wa Sahara jijini hapa.

  Mahojiano baina ya mbunge huyo na Jeshi la Polisi yalianza saa 11.30 jioni baada ya mbunge huyo kujisalimisha mwenyewe polisi akitokea Dar es Salaam.

  Wenje alikuwa ameambatana na wakili wake pamoja na Katibu wa Chadema Mkoa wa Mwanza, Wilson Mshumbusi.

  Gazeti hili lilifika polisi saa 12 jioni na hadi saa 1.15 usiku, mbunge huyo alikuwa bado akiendelea kuhojiwa.

  Katika mkutano huo, Wenje anadaiwa kuwahamasisha wananchi kufika kwa wingi katika ofisi za Halmashauri ya Jiji Mwanza leo kwenye uchaguzi wa Meya wa Jiji ili kuhakikisha Chadema inashinda kiti hicho huku akiwasisitiza kufanya kama vile walivyofanya wakati wa kutangaza matokeo ya ubunge.

  Wakati wa kutangaza matokeo ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 31, mwaka huu, vijana wanaodaiwa kuwa ni wafuasi wa Chadema walifanya uharibifu wa miundombinu pamoja kuchoma moto jengo la CCM na kutishia kuchoma moto ofisi za Halmashauri ya Jiji wakishinikiza msimamizi wa uchaguzi kutangaza matokeo.

  Hata hivyo, jeshi hilo limepiga marufuku wananchi ambao sio wafanyakazi wa halmashauri kufika katika jengo la Halmashauri ya Jiji la Mwanza kwa nia ya kufanya vurugu siku ya uchaguzi wa Meya.

  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Simon Sirro alithibitisha kushikiliwa kwa mbunge huyo na kueleza kuwa baada ya mahojiano, aliachiwa kwa dhamana.

  “Ni kweli tulimshikilia na kumhoji kwa saa takribani nne, lakini tulimuachia kwa dhamana baada ya kuandika maelezo yake,” alisema Kamanda Sirro na kuongeza kuwa mbunge huyo alikiri kuhamasisha wananchi kwenda jiji kusikiliza matokeo ya uchaguzi wa Meya.

  Hata hivyo, Kamanda Sirro alisema ushahidi kwa upande wa polisi umekamilika na kwamba faili limepelekwa kwa Mwanasheria wa Serikali kwa hatua zaidi za kisheria.

  Sirro alisema ofisi yake imekuwa ikipokea ushahidi kutoka kwa wananchi waliohudhuria mkutano wa Wenje juu ya kauli za uchochezi alizozitoa na hivyo waliona ni bora akakamatwa na kuhojiwa juu ya kauli hizo.
   
 2. Mhoja

  Mhoja JF-Expert Member

  #2
  Dec 16, 2010
  Joined: Aug 13, 2010
  Messages: 206
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Hizi ndiyo siasa za tanzania. Uhuru unahitajika, wenje anaonewa
   
 3. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #3
  Dec 16, 2010
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,326
  Likes Received: 1,792
  Trophy Points: 280
  Toka lini watu kudai haki yao ni uchochezi?
   
 4. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #4
  Dec 16, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  eti upelelezi umekamilika ..upumbavu mtupu
   
 5. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #5
  Dec 16, 2010
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Kama wanajua upelezi si watuambie wamiliki wa Richmond, kagoda,meremeta nk
   
 6. M

  Mwera JF-Expert Member

  #6
  Dec 16, 2010
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 968
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nimeona hapojuu wanasema uchaguzi wa meya wajiji la mwanza unafanyika leo je nani ameshinda?ni chadema matarajio itashinda je matokeo rasmi imekuaje?mwenye data atupatie jamani.
   
 7. The Planner

  The Planner JF-Expert Member

  #7
  Dec 16, 2010
  Joined: Dec 1, 2010
  Messages: 350
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Nadhani tunahitaji maana nyingine ya demokrasia hapa kwetu, Kama kuhamasisha watu kusikiliza matokeo ya uchaguzi ni hatia.,mmh!!
   
 8. shanature

  shanature JF-Expert Member

  #8
  Dec 16, 2010
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 718
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  Chuki tu uonevu tu hawakubali kushindwa hao akina cc
   
 9. samirnasri

  samirnasri JF-Expert Member

  #9
  Dec 17, 2010
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 1,377
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  CCM wameshajipanga kuchakachua matokea wako radhi kufanya kama baraza la katiba la cote d' ivoire lilivyofanya kupindisha matokeo ili wasilipoteze jiji hilo la pili kwa ukubwa nchini linalokua kwa kasi na lenye mapato mengi. Kutokana na hali hiyo ndio maana wameanza kutumia dola kutisha wananchi kwa sababu wanajua nini wamepanga kukifanya.. Najua kamanda sirro hataki kulaumia kama alivyolaumiwa wakati wa matokeo ya ubunge...
   
 10. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #10
  Dec 17, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,328
  Likes Received: 22,172
  Trophy Points: 280
  CCM HOYEEEEE. Nasikia TIDI MHANDO amefukuzwa kazi kwa sababu alitoa airtime kwa CHADEMA.
   
Loading...